MATAPELI: Tahadhari kwa wateja wa vodacom Tz

sumu-ya-panya

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
632
571
Hivi Leo nimepata Taarifa za kuthibitisha matapeli wanajitambulisha kama wafanyakazi wa Vodacom makao makuu Mlimani city. Watu hawa wanakutaarifu kua umejishindia Tecno Y2 pamoja na laki mbili (200,000) na promosheni ya Vodacom Nogesha upendo,na Bonasi ya mpesa.huwaambia wateja ilikuthibitisha wewe ndie mwenye akaunti hukuuliza kuhusu mpawa na mpesa salio lako miamala ulio kwisha fanya lengo likiwa ni kujua salio lako kisha wanakuambia ilikupata zawadi yako unapaswa kuwa na salio katika mpesa yako kiasi cha asilimia 40% ya zawadi unayoshinda.
ikiwa utaweka salio watakwambia utume neno TAYARI kwenda namba +255767245300 ambayo ndio wanayokupigia nayo.

jamaa angu kawakubalia kisha akapiga simu vodacom kuthibitisha promoshen na bonasi vodacom mhudumu toka namba 100 alisema si kweli hakuna promosheni na hawapigi simu unawekewa moja kwa moja.

basi jamaa akaamua kuwalia nyaro,akatuma neno TAYARI kwenda namba +255767245300. hata sekunde haija pita wakampigia simu.
wakamuuliza ameweka kiasi Gani jamaa akawaambia kaweka milioni mbili (2,000,000) mhudumu akahamaki kiasi kikubwa cha pesa alichoweka badala ya ile 40% ya laki mbili (80000) basi akamwambia kama anasimu nyingi apigiwe afate maelekezo,jamaa alisema hana hapo alipo, mhudumu alimwambia angali hata kama kuna mtu wa karibu wampigie jamaa akasema hana mtu yeyote anasafiri kulekea kenya na hapo alipo yupo kwa gari private. Mhudumu akasema basi angoje aunganishwe na upande wapili. jamaa akasema pesa nimeshaweka maelekezo yanini tena wakati pesa nshaweka ghafla simu ikakatwa. baada ya muda jamaa akapigiwa tena na namba +255743362563 ikijitambulisha imeunganishwa na upande wapili toka yule mhudum wa kwanza .akamtaka afate maelekezo jinsi ya kupata zawadi zake jamaa akamlia nyaro(kuvunga ka hajui) akamsikiliza kisha akamuuliza maelekezo labda yawe mi kupata iyo simu,kuhusu iyoi pesa basi itumwe kwa simu yake. ukazuka ubishi hapo jamaa akakata simu. mchezo ukaungua.

Tahadhari kwa Wateja wa vodacom Tanzania wasifute maelekezo yoyote wanayopewa na simu zinazopigwa wakijitambulisha ni wahudumu wa vodacom Tanzania.

vodacom hawana utaratibu wa kumpa mtu maelekezo ya kupata zawadi yake hasa fedha kwa njia ya simu bali humjulisha mteja au kumwekea papohapo na wasikupigie simu kabisa. mimi nishajishindia na vodacom.

namba ambazo atleast ni za vodacom tanzania ni
+255901761234
+25576670 - kwa masuala ya mpesa pekee.

asanteni
OKOA JAMII ZUIA UTAPELI
 
Mimi wala siwasikilizagi labda waniite offisini
 
Kinachonipa maswali ni hiki hivi hii mitandao ya simu kwa kushirikiana na polisi, tcra wameshindwa kuwakamata wahalifu hawa mbona wanaoitwa wachochezi hukamatwa?
 
Cyo rahisi, may be uwe umeibiwa uende polisi ufungue kesi ndo uende kampuni ya simu ndo wanaweza kukusaidia. Wezi ni wengi Na kampuni haiwez pokea taarifa zote za kutaka kuibiwa alafu wachukue hatua ya kumkamata mwizi akat hakuiba na ujue ni ngumu kiasi gani kumkamata mtu usiejua yuko wapi . So cha msingi Tu ni kuwa makini usiibiwe, ila ukiibiwa ndo ufwate taratbu nlizokwambia.
 
Back
Top Bottom