Matapeli hatari, chunga wasikudake


Nahisi hao jamaa baada ya kujaribu kunitaperi walikuja kwako maana maelezo yako ni copyright.
 

isee mkuu umenifunza kitu big up kiongozi
 

mkuu mt.j hii yako ilinikuta na mimi, ila wlibadili kidogo tu, mimi walinambia dawa ya kunyunyiza katika visima vya maji huko ktk migodi serengeti, ili maji yawe salama! tuliposhindwana ni pale nilipowaambia sina laki5 ya kumpa muhasibu anaetaka nimpe hela, anipe risit, tukaanza kutukanana!
 
Nasubiri nimpate aliyetapeliwa maana inaonekana nyote mlikuwa wajanja. Haiwezekani kwani kama hakuna ambao wanaingizwa mkenge wangeacha. Nasubiri sitoki
 
matapeli wako kibao siku hizi wengi wanaingizwa chaka kwa utapeli wa kimtandao siku hizi ukizubaa wanakulamba yaani
sijui hawa wasimamizi wa mitandao tcra wako wapi?
 
Pia wapo ambao wanakupia Kwa njia ya tango au Skype kuwa umeshinda dollar 1000 ktk Kampuni ya coca cola United Kingdom. Na kudai utume particular zako na account no ya bank isiyo na kitu. Ogopa sana.
 

daaa sitawasahau hawa viumbe.ila walinikosa
 
Nahisi hao jamaa baada ya kujaribu kunitaperi walikuja kwako maana maelezo yako ni copyright.
Ila wajanja kiasi. Maelezo yao yanashawishi kiasi fulani na ukichangia na shida za watu na kutamani pesa za chap chap nadhani kuna wanaowapata.
 
Ila wajanja kiasi. Maelezo yao yanashawishi kiasi fulani na ukichangia na shida za watu na kutamani pesa za chap chap nadhani kuna wanaowapata.

Mimi nilishituka mwishoni sana
 

hawa jamaa wamezidi, ukizubaa unaweza kuliwa. mimi pia waliwah kunipigia simu miezi sita ilopita. case ilikua hiyo hiyo ya pipes. jamaa alidai ananifahamu sana na tulivokua tukiongea alinishangaa sana kuona simfahamu/nimemsahau. Alidai yeye ananifahamu sana. s?kutaka kusumbuana nae kuhusu swala la kufahamiana nae. nilijifanya kumfahamu. Alinipa namba ya simu ya mzee ambaye ni dealer wa pipes anayeitwa Mzee Ramadhan mwenye duka la hivo vifaa maeneo ya Nyegezi stand. Akanambia nimpigie simu anipe maelekezo ya namna ya kumsaidia huyo jamaa [tapeli] kununua na kusafirisha hzo pipes. kuna mengi yaliendelea ambayo kwa mtu anayefikiri na kuchambua mambo vizuri atagundua kirahisi mchezo unaoendelea. Nilimkomesha pale nilipomwomba anisaidie vocha na nauli ya kuendea kwa mzee Ramadhani wakati huo nilikua maeneo ya Malimbe. Hakunisumbua tena.
 
Mimi nilishituka mwishoni sana

mkuu kambagasa, mi nilistuka mapema. alinambia kwamba kuna wafanyakazi wenzake wa hyo kampuni sijui ndo Pawaga ya Iringa wako mwanza kwenye semina na wanakaa Malaika Hotel. kwaio ninunue huo mzigo then niwapelekee huko then wao waondoke nao kurudi Iringa. akasema zinahtajika 50 pcs za hydraulic pipes na kila moja inauzwa 150,000/=. kwaio mara 50 ni sh7.5M. ila kwakua ni hela ya kampuni, mimi na yeye tutanua kwa bei mara mbili ya actual price per piece yaani 300,000 kwa kila pc mara 50 nr 15M ambazo nitakabidhiwa mimi na hao jamaa walokuja mwanza kwenye semina then nikalipie kwa mwuzaji. kwaio kuna 7.5m za bwelele. kwakua mi nimepigiwa pande tu aliahd kuniachia 2.5m akasema maisha ni kusaidiana. sasa nikajiuliza maswali mengi nikakosa majibu.
#kwanini asifanye hilo dili na hao wafanyakazi wenzake mpk mimi third part nihusike?
#hv inawezekana kwamba hakuna mfanyakazi hata mmoja kati ya hao wenzie anaejua bei za hzo pipes?
#nilipomwuliza katoa wapi namba yangu ya cm alinambia alikua nayo muda mrefu kwani yeye na mzee wangu wanafahamiana tangu ktambo walipokua wanafanya biashara Morogoro wakat mzee wangu hata huko moro ni mpita njia tu.
nilimkomesha kwa kumwomba nauli ya kufanyia hzo mishe zote akaona nimemshnda. alitoweka mwenyewe.
 
Nasubiri nimpate aliyetapeliwa maana inaonekana nyote mlikuwa wajanja. Haiwezekani kwani kama hakuna ambao wanaingizwa mkenge wangeacha. Nasubiri sitoki

si rahisi kuingia mkenge kama kwelu kukichwa kuko sawa. subiri labda kuna boya alikurupuka akapigwa za uso
 
mi walinipigia wakaniamnia habari za biashara.ya vinyago na wakataka nilipie laki nne ya kusafirisha vinyago vyenye thamani ya milion 10 halafu waulete mzigo kwangu ili mnunuaji aukute kwangu anipe hzo 10 miluon halafu nigawane nao wao wachukue 7 waniachie mimi 3 milion. nikawashtukia na nikawaambia hawawezi kuniibia. Baadaye jamaa aliyejiita dalali akaniambia nimpe namba ya mtu ninayemchukia ili wamtapeli.
 
Nishakumbana nao wakiniingia na dili la dawa za kuzuia dumuzi kwa ajili ya chakula cha wafungwa kambi za wakimbizi (UNHCR) wanaongea kiingereza balaaa!!!!

Milimwambia Nina Lak Mbl Na 94 Nmb Sasa Niko Mbl Na Mjin Na Nataka Kutoa Hla Kamil Naomb Unitmie Elfu 6 Ili Nkitma Nitme Tatu Kamil Kwa Njia Ya Mpesa Maana Kwny Mpesa Nina Elfu 9namia 3 Jamaa Akajikok Alvo Tma Tu Nkajiunga Bado La Wiki Afu Nkamtext Asanteee Kwa Kejel Alinitkana Kwenye Txt Yn Ofisi Nzma Ilikuwa Inafatilia Kwa Makin Tulicheka Sana, Hao Jamaa Wametapel Wat Weng Sana Na Inawezekan Huwa Wanaushrka Na Wat Wa Karbu Wanao Kufaham Maana Wanakujua Jna ,kaz Unayofanya Na Mahala Unapoish
 
matapeli wako kibao siku hizi wengi wanaingizwa chaka kwa utapeli wa kimtandao siku hizi ukizubaa wanakulamba yaani
sijui hawa wasimamizi wa mitandao tcra wako wapi?

bado walikuwa wanarahisisha uchaguzi.. sa sijui wamepoteleamo
 
ningeiona thread hii mapema labda nisingewaza sana
walikuja kwa gia ya kuwa ni ndgu yangu.. jina langu ni gumu sana lakini jamaa akalitaja vzuri sana akasema yeye ni ndugu yangu na alitaja hadi nilipo hapa sijui alijuaje akaanza saundi ooh nenda hospital ya meta kuna dili la wachina tununue mabunda ya neti ndg yangu. nimekuamini na blah blah kibao nikamuhoji wewe unasema ndgu yangu unaitwa nan? akaja kujichanganya kwamba eti tulikutana kwa mtogole wakati mimi hata sijawahi fika huo mtaa.. ndo ikawa pona yangu
 
Mkuu hiyo sentensi ya mwisho imeniacha hoi!
 

Duuh mi walishanipiga Znzbr na nikawataarifu rafiki zangu wrote baadae wakarudia tena nikapeleka taarifa zote Polisi. Madema znz. Polisi wakasema hawana msaada baadae nilifanikiwa kupata mwasiliano ya Mmoja wao akasema siwezi ua mtandao huo kwani wana watu wengi, na namna tofauti.
 

Haa haaa haaa...kati ya post zote hii ya kwako kali asee! eti uwape namba ya mtu unayemchukia wamtapeli!?!!?.....haaa haaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…