Matangazo ya kulipia yanakula sana pesa

Matangazo ya kulipia yanakula sana pesa

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,879
Reaction score
4,031
Usiwe mwekezaji wa fedha nyingi kwenye matangazo kabla hujajenga utambulisho wa biashara yako.

Katika biashara, watu hawahitaji tu kujua unachouza, wanahitaji pia kujua wewe ni nani, una utaalamu gani na kwa nini wanapaswa kukuamini.

Kabla ya kuanza kutumia fedha nyingi kwenye matangazo, jenga utambulisho wa biashara yako kupitia maudhui yenye thamani.

Unapokuwa unatoa elimu, kushirikisha maarifa na kutatua changamoto za wateja kupitia content:

  • Unajenga jina na utambulisho wa biashara.
  • Unatengeneza uaminifu kwa wateja watarajiwa.
  • Unawaonyesha watu thamani ya huduma zako.
  • Unarahisisha matangazo yako kuwafikia wateja wenye uelewa kuhusu biashara yako.

Kumbuka: Matangazo yanaweza kukufanya ujulikane, lakini uaminifu ndio unaoweza kumfanya mteja akupatie pesa yake.
 
Back
Top Bottom