njundelekajo
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 310
- 227
MATANGAZO YA BUNGE,UNAFIKI WETU NA UKAKASI WA FIKRA
Na Nguzo Noel .R.
Geneva Uswis tarehe 19/10/2006 kulikua na kongamano lililoandaliwa na The European Broadcasting Union(EBU) kwa kushirikiana na The Association of Secretaries General of Parliament (ASGP) mada ikiwa UMUHIMU WA KUTOA NA KUPANUA UWAZI KATIKA SHUGHULI ZA BUNGE kongamano hili kubwa kabisa lilihudhuriwa na washiriki 200 kutoka katika nchi 80 duniani.
Miaka 10 baadaye 2006-2016 Tanzania inakuja na mpango wa wenye tafsiri UMUHIMU WA KUZIBA NA KUBANA UWAZI WA SHUGHULI ZA BUNGE!!!! Dunia inapokwenda mbele sisi tunarudi nyuma!! Aina gani hii ya mwendo tulioamua kutembea?.Wanaoutafuta ukuu wa wilaya wanadai huu ndio mwendo hasa WA kutembea kisa HAKUNA NCHI YOYOTE DUNIANI INAYOONESHA BUNGE LIVE !!!alah
Mbona hakuna nchi yoyote duniani iliyounganisha nchi zake mbili na zikatoka serikali mbili? Ila Tanzania imeweza? Hivi kina Mtela Mwampamba nchi kuendelea ni kuiga tu bila kubuni?
UWONGO NI SEHEMU YA UTAMADUNI WETU?
Tar 17/6/2015 katika ukumbi wa Mwl Nyerere wakati wa kongamano la wiki wa utumishi wa umma ofisi ya Rais ikulu kitengo cha utawala bora ilidai kwamba moja ya hatua zilizochukuliwa na serikali katika kuimarisha uwazi serikalini ni pamoja na mikutano ya bunge kuoneshwa kwenye TV na wananchi kufuatilia mijadala na kusikia majibu ya utekelezwaji wa shuguli za serikali!!
Leo wananchi kufuatilia majibu ya utekelezwaji ni kupoteza muda na kutofanya kazi ni sawa na kucheza pool!!
KWA NINI BUNGE LIWE LIVE NA SI KUREKODIWA?
Bi Eve-Lise Blank mmoja wa washiriki WA kongamano la 19/10/2006 anasemaje wao ufaransa wanabunge Tv vipindi vyote vya BUNGE hurekodiwa na kurushwa bila kuhaririwa(editing) kama sehem ya communication lakini vipindi vya bunge vilivyohaririwa hurushwa vikiwa na lengo la kupeleka taarifa maalum za serikali(information)!! Kwa nini Nape anag'ang'ania aina ya pili ya lengo la kurusha vipindi vilivyohaririwa tu?
HAKUNA IMANI ?
Luka 16:10 "mtu ambaye ni mwaminifu katika mambo madogo atakua mwaminifu katika mambo makubwa,na mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo atakua si mwaminifu katika mambo makubwa"
Imam Ali(s.a)"ambaye siri yake haitofautiani na dhahiri yake na vitendo vyake havitofautiani na maneno yake basi atakua ametekeleza amana na amewafanyia ikhlasi waja"(ikhlas maana yake ni kua sawa ndani ya mwanadamu na nje yake ,kila kilicho ndani kinachoenda kinyume na nje ni batili)
Kabisa unaamini kwa matendo na tabia ya serikali ya c.c.m itakuonesha ufahamu mkubwa WA sheria WA Tundu Antipas Lissu?,unategemea hulka za Nape zitaruhusu vipindi vilivyorekodiwa zioneshe uwezo wa Peter Msigwa wa kujenga hoja?kabisa Ndugai akubali Mdee aliyemwita kituko ashushe takwimu zake kupitia luninga yako?
Means justify the end!!kama walitolewa nje mchana kweupee huku matangazo yakiwa live na waandishi wenye kamera tumia formula kupata watakachofanyiwa "gizani"
KWA NINI C.C.M WANAFANYA HIVI?
Abraham Maslow anasema "ukiwa na nyundo unaona kila kitu kama msumari" NI serikali yenye hofu ya kuumbuka tu kwa wizi,ufisadi inayoweza kuzuia bunge kuoneshwa live!!Ni wabunge na mawaziri tu wanaosinzia bungeni watakaofurahia bunge kutorushwa live,ni spika na manaibu spika watemi na wababe tu watakaotaka bunge lisioneshwe live
TUACHE AU TUPUNGUZE KABISA UNAFIKI
tar 21/9/2011 tulijiunga na MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI(Open Government Partnership O.G.P)
Kwa nini tulijiunga tukiwa hatuna dhamira ya kweli? Tulijiunga ili tupate wafadhili?
TUSIJE TUKAINGIA KWENYE RECORDS ZA VITUKO
Mobutu Seseko Rais wa zamani wa Zaire(sasa ni D.R.C) dunia haitomsahau kwa mambo mengi.Moja ya kituko alichowahi kufanya ni kutunga sheria ya kukataza televisheni za Zaire kutotaja jina la mtu yoyote kwenye TV isipokua jina lake tu!!
Sio kazi kufika halipofika Mobutu kama wote nia yetu ni kuzawadiwa ukuu wa wilaya!! Hakutokuwapo na wakosoaji hata wa makosa ya kawaida!!
Nelson Rolihlahla Mandela alipata kusema"nawapenda marafiki wenye Uhuru WA kufikiri kwakua wanakufanya ulione tatizo kwa upana zaidi" Endeeleni kusifia kila kitu tulio huru tutakosoa Mara zote inapobidi.
MWISHO
Tanzania ni mwanachama wa MPANGO WA AFRIKA WA KUJITATHIMINI WENYEWE(AFRICAN PEAL REVIEW MECHANISM{APRM} ) sio dhambi hata kidogo kama taifa tukajithimi katika hili LA bunge na tukakiri tulipotoka!!!!! TUNATAKA BUNGE LETU LIONESHWE LIVE
By Nguzo Noel .R.