Matajiri wa mali ni rahisi sana kuingia mbiguni kuliko mafukara (makapuku)

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,738
22,466
MARKO 10:25..Ni rahisi Ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme Wa Mungu..

Pasipo kuutafakali vizuri; Msitari huu watu wengi sana walio FUKARA Hujiliwaza Kwa kuamini kwamba wapo njia sahihi ya kuuona ufalme Wa Mungu, wengi huamini kwamba moja ya tiketi ni UFUKARA Ili kuuona ufalme Wa Mungu. (SI KWELI HATA KIDOGO).

KUANZIA LEO ISHI KATIKA KAULI IFUATAYO "NI RAHISI KWA MWENYE MALI KUUONA UFALME WA MUNGU KULIKO FUKARA KUINGIA MBINGUNI".

Fukara ni mtu wa lawama sana.
Fukara ni rahisi kuiba
Taifa la watu fukara limejaa wanafiki
Ufukara ndiyo mtego mkuu wa shetani.

KUMBUKA JAMBO HILI!
Fedha, mashamba, Magari, majumba na vyooote uvionavyo ni Mali ya Mungu!
Sasa kwanini ufe Ufukara? Yaani mlima mlefu Africa upo Tanzania, mbuga, bahari, wanyama, ardhi nzuuri ya kijani na mambo kedekede yapo Tanzania halafu wewe ufe na ufukara kweli? HAPANA KWA KWELI!

Kwanza tambua hili;

Msije mkono mitupu madhabahuni pa Mungu, hapo ni Fedha.
Sadaka kanisani ni fedha!
Kujenga kanisa au msikiti ni fedha!

Sasa iweje tajiri asiingie katika ufalme Wa Mungu kirahisi? Fedha ni sabuni : fedha huleta amani, njaa peke yake huwapotosha watu!

Nafahamu ya kuwa katika Mathayo 5:3, Yesu Kristo alisema; “Heri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Watu wengi wanapousoma mstari huu, wanadhani Yesu Kristo alisema “Heri walio maskini wa mahitaji ya MWILI; maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Lakini Kristo hakusema hivyo.

Mtu maskini maana yake ni mtu mhitaji. Yesu Kristo aliposema “Heri walio maskini wa roho …….”

Alikuwa ana maana ya kusema ‘Heri walio wahitaji wa mambo ya rohoni; maana ufalme wa mbinguni ni wao. Ndiyo maana aliongeza kusema, “Heri wenye njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa" (Mathayo 5:6).

Sasa kamwe usijifariji kwa ufukala wako hapa duniani, waweza kuwa fukara duniani na mbinguni ukachomwa!
 
Soma uelewe context ya andiko! Kama huelewi ni hivi: mali (iwe ndogo au nyingi) au kitu chochote ukikiweka nafasi ya kwanza katika maisha yako badala ya Mungu inakuwa ibada ya sanamu.
Pia kuna suala la upatikanaji wa mali hiyo. Wengine huipata kwa njia zifuatazo:
1. Wizi
2. Rushwa
3. Waganga na kafara
4. Dhuluma
5. Kukwepa kodi
Kwa namna hizi, wewe endelea kujifariji na mali zako!
 
Makanisani kwenyewe ukiwa kapuku hata wachungaji hawakuangalii hehe....wanashobokea wenye mkwanja tuu
 
Makanisani kwenyewe ukiwa kapuku hata wachungaji hawakuangalii hehe....wanashobokea wenye mkwanja tuu
Hao ni wachungaji wapiga dili au ndio wale waliozungumziwa katika bible,wachungaji wa siku za mwisho.
 
Upo sahihi kabisa hata ukisoma warumi kuna sehem kabisa inasema mungu hakuweka agano na masikini.kwa maana ukiweka agano na masikini ni rahisi sana kulubuniwa.ni wakati sasa watu wanatakiwa wasome biblia na kuielewa vzuri.hata yesu alifanya huduma kamilifu ya kiroho na kimwili sasa wahubiri wengi wanabase kwenye kiroho ambayo ni makosa makubwa uyo mtu akiwa hana chakula atakuja kusali,.ukisoma matendo yoote ya yesu utaona mfano kisa cha mama mjane na mafuta,ulimwengu ni nuru na chumvi nk.watu saiv lazima wajue kufanya huduma kamilifu
 
Dah, nikajua unajua maana ya andiko ulilolileta, kumbe nawe ni hamnamo kabisa, hata ukiwa fukara na ukamsahau Mungu, akategemea akili na fikra zako mwenyewe, basi wewe ni Tajiri, hiyo haizungumzii utajiri wa mali za kidunia mkuu!
 
Hata mapepo, huwa hayaendi kwa mtu tajiri/mwenye mali. Makanisani na misikitini wanawasujudu wenye pesa. Kama unabisha, jitengenezee utaratibu wa kujitoa sana katika events na projects mbalimbali katika Kanisa/Msikiti unaoabudia then utaona impact yake.
 
Umebishana na Magufuli weee ukachoka sasa umeamua kubishana na Yesu, sivyo? Eidha umechanganyikiwa na hii hali ngumu ya maisha au una ujasiri sana.
 
Kama huna hela, huna chako duniani mpaka mbinguni.
Wewe lazima uwe mfuasi wa Mwingira wa EFATHA! Ndivyo wanaefatha wanavyohubiriwa na mitume wao wa pesa, pesa wanazopata kwa kuchangiwa na hao hao waumini fukara. Anayetoa pesa anazidi kuwa fukara na kama haitoshi anahubiriwa kwamba mbinguni haendi kwa sababu ya ufukara wake!
 
Upo sahihi kabisa hata ukisoma warumi kuna sehem kabisa inasema mungu hakuweka agano na masikini.kwa maana ukiweka agano na masikini ni rahisi sana kulubuniwa.ni wakati sasa watu wanatakiwa wasome biblia na kuielewa vzuri.hata yesu alifanya huduma kamilifu ya kiroho na kimwili sasa wahubiri wengi wanabase kwenye kiroho ambayo ni makosa makubwa uyo mtu akiwa hana chakula atakuja kusali,.ukisoma matendo yoote ya yesu utaona mfano kisa cha mama mjane na mafuta,ulimwengu ni nuru na chumvi nk.watu saiv lazima wajue kufanya huduma kamilifu
Yesu alikuwa na pesa trillion ngapi? Magari, mashamba mangapi? Je; maskini Lazaro (Luka 16:19-26) hakwenda mbinguni?
 
Wewe lazima uwe mfuasi wa Mwingira wa EFATHA! Ndivyo wanaefatha wanavyohubiriwa na mitume wao wa pesa, pesa wanazopata kwa kuchangiwa na hao hao waumini fukara. Anayetoa pesa anazidi kuwa fukara na kama haitoshi anahubiriwa kwamba mbinguni haendi kwa sababu ya ufukara wake!
Kwahiyo unaona mimi pesa yangu haina kazi mpaka niipeleke kanisani? Huyo Mwingira hata simfahamu, hebu nifahamishe ni nani huyo?
 
Hahaha hata Mungu anapenda na kupokea sadaka iliyonona...Kumbuka kisa cha Kain na Abel
 
Siku hizi shilingi 100 kanisani hawaitaki,alafu fukara anauonaje ufalme wa mungu? Make hata sadaka tunayotoa haitoshi
 
Back
Top Bottom