DUBULIHASA
JF-Expert Member
- Nov 26, 2016
- 4,299
- 7,851
Tayari Rais Magufuli ameteua viongozi wa tume ya uchaguzi hususani mwenyekiti wa tume pamoja na makamu wake. Ningependa niwaulize machache wanaccm, wapinzani pamoja na wasio na vyama maswali machache, unapojibu swali/ maswali unaweza ukasema au usiseme uko kundi gani kutoka katika makundi hayo matatu. Maswali yangu ni kama ifuatavyo
-Je kuna ulazima wowote rais kuchagua tume ya uchaguzi bila kuwashirikisha upinzani kama wadau wakubwa kwenye tume? Na kwa nini?
-Je wale waliochaguliwa na rais kwenye tume hawawezi kumpendelea rais na chama chake? Toa sababu.
-Je ni vipi wapinzani wataweza kushinda uchaguzi kihalali chini ya tume iliyochaguliwa na rais ambaye pia naye ni mshindani kwenye uchaguzi?
-Je wapinzani wamechukua hatua gani kuhakikisha kunakuwepo na tume huru ya uchaguzi?
-Je iwapo kama hawatakubaliwa kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi wapinzani watafanya nini?
TAFADHALI JIBU KISTAARABU KWA SABABU DHUMUNI NI KUJENGA SIO MASHINDANO.