Majuzi Hollyman alifungua thread ya aina hii.Nia na lengo lake lilikuwa ni zuri,namshukuru.Nimeamua nifungue mwenyewe hii thread ili iwe ni uwanja wa kudumu wa kuniuliza maswali,kutaka ufafanuzi na pia kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya mpira wetu.Kwa ruhusa ya moderators ninaomba uwe ni ukurasa wa kudumu hapa jf.
Jamal Malinzi
Rais wa TFF
Dar es salaam 04/Feb/2014
uko sahihi kabisa na hoja zako ni za msingi.Wakati wa contract reviews yote haya tutayazingatia.
Kwa style hii RAIS utafanikiwa kujua mengi ni watendaji wako tu kuchapa kazi tulio wengi tunapenda kuona mabadiliko makubwa kwenye uendeshaji wa soka letu mimi binafsi naunga mkono baadhi ya maamuzi yako hasa suala la soka la vijana.
Ila niwe muwazi najua upo karibu na watu kama KABULU GEOFREY mwambie kabisa apunguze unazi wake wa wazi wazi kama ameamua kuwa ndani ya chombo kinachosimamia mpira kitendo alichoonesha mechi ya mtani jembe kinaleta taswira mbaya ameamua kuwa TFF apunguze unazi wa hadharani hawa ni watu wanaweza kuharibu taswira ya uongozi wako mapema.
Pia tunaomba uangalie jinsi ya kuandaa utaratibu wa kureview mikataba ya watangulizi wako hasa mikataba ya udhamini wa ligi kuu kwa maana mkataba na vodacom na azam kuna makungufu ni kuna kila dalili kuna robbing fulani ilifanyika pande zote hazikushirikishwa ipasavyo.
Mokoyo kwa vyovyote vile tutaongeza timu za premier league na kuanzisha mashindano mapya ili vijana wetu wapate angalao mechi 40 za kucheza kwa mwaka.Mabadiliko haya yatakuja msimu ujao.Je ndugu mwenyekiti Jamal Malinzi hauoni umuhimu wa kuongeza idadi ya timu kwenye ligi kuu ya Vodacom? Ligi yetu ina timu chache sana kiasi kwamba kunakuwa na mapumziko ya muda mrefu ambayo yanashusha viwango vya wachezaji na kuathiri vilabu pamoja na national team?
Naomba ufafanuzi kuhusu kuhamisha ofisi za TFF na kujenga kitega uchumi pale Karume.
Ufafanuzi na uwazi ni muhimu ili wadau wa soka wajue kinachoendelea.
Tumeona jinsi ufisadi ulivyoingia kwenye maeneo kama hayo. Chukua mfano wa UVCCN na UWT. Hivi kweli jumuiya hizo zimenufaika?
TFF wasije kuwa wapangaji kwenye eneo lao wenyewe. Nani alitoa uamuzi huo? Kamati ya utendaji au mkutano mkuu.
Nahisi suala hili linahittaji baraka za mkutano mkuu kama ajenda muhimu
Nani mwekezaji? Yapi makubaliano na TFF? Gharama yake na vitu kama hivyo
Jamal...Mokoyo kwa vyovyote vile tutaongeza timu za premier league na kuanzisha mashindano mapya ili vijana wetu wapate angalao mechi 40 za kucheza kwa mwaka.Mabadiliko haya yatakuja msimu ujao.
Jamal Malinzi
Naomba kujua kuhusu mashindano ya Kombe la Taifa, Je mtayarudisha lini?
Kiukweli nilikuwa mshabiki wa kombe hili sana maana lilikuwa likiibua vipaji vingi na ningependa mtakapo lifufua mruhusu liwe ni la Vilabu na sio Mikoa na mruhusu timu yeyote hata kama ni ya Mchangani ishiriki kama ilivyo kwa kombe la Carling/Capita one Cup huko uingereza ambapo mashindano ni ya mtoano na yana shirikisha timu zote nchi nzima no mata ni kubwa kiasi gani.
Naamini wazamini wapo wengi wali tayari kudhamini na Kuonyesha haya mashindano naamini hata Makampuni ya soda/Maji/ simu/ na mengineo yalio kosa nafasi kwenye Ligi kuu, itakuwa ni nafasi yao kushindania na huku waweze kujitangaza.
Na ni hivyohivyo kwa makampuni ya Tv. Kama Zuku, Dstv, Startimes, Ting, Continetal/Digitec wanaweza kupata fursa pia ya kugombania tender ya kuonyesha hii michuano pia.
Na kama utakubaliana na mimi nina ushahuri zaidi wa jinsi ya kupata mapato na kuendesha hii ligi ya Mtoano na iwe ya Ufanisi.Maana kwenye Kombe kama hili tunaweza tukashuhudia timu yangu ya mtaani ikicheza fainali au hata robo fainali na Yanga/simba au ata Timu yeyote ya Ligi kuu.
ahsante kwa ushauri. Mikataba ambayo nimeikuta wajibu wangu ni kuiheshimu hadi kipindi chake kimalizike na ndipo tuiboreshe,ingawa mingine kwa kweli inabidi ifanyiwe kazi haraka kwa usalama wa watazamaji.
uko sahihi kabisa na ninaomba nikuhakikishie muda si mrefu tutaanzisha mashindano kama FA cup ya Uingereza.
Ligi yetu KUU ina teams nyingi sana za MAJESHI(JK Ruvu na Mgambo zikicheza team iliyo ktk hatari ya kushuka daraja likely ikanufaika na mazungumzo ya kiafande;Polisi Moro vs Polisi Dodoma)
Kwa nn isije sheria kwenye top league idara moja iruhusiwe kuwa na team moja tu?
Ndugu rais nachojua mimi ata kabra mkataba haujafikia mwisho pande mbili za mkataba zinaweza kukaa na kufanya review ya mkataba ili kuuboresha kulingana na mahitaji na mnaandaa mabadiliko hayo ya mkataba (Adendum) je uone kuna haja ya kufanya hivyo sasa hasa mkataba wa vodacom na azam tv.
awali ya yote nikupongeze kwa ujasiri wako,kuamua kukubali challenges,then nijaribu kutoa mawazo yangu................
wadau wengi wasisitiza kuwa bila ya academy za soka ili kuandaa vijana, tanzania haitapiga hatua ktk soka la kimataifa.hofu yangu kuwa utafiti unaonyesha uingereza,ufaransa,ujerumani na wengine wana academy nyingi sana lakini ukiitazama uingereza hawafanikiwa vya kutosha,ufaransa wanabebwa na mamluki(foreigner) nawaza endapo tutaendeleza academy halafu tukashindwa itakuwaje?the way forward...........
pamoja na uwepo wa academy ishu kubwa ni exposure TFF ikae meza moja na serikali kama kuna vijana wanapelekwa ulaya na amerika kusoma fani nje ya kwanini tusiteue vijana bila upendeleo wenye vipaji halisi wakapelekwa kama vile spain,france,portugal kwa idadi maalumu hasa washambuliaji na mabeki wengi ila viungo wachache wakawe trained kiasawasawa naamini baada ya miaka 5 tutakuwa na mabadiliko japo kidogo then 10 yrs to come its amazing.......
lingine TFF iunde national supporters group ambalo kazi yao itakuwa ni kushangilia tu mwanzo mwisho kama ilivyokuwa kidedea kwa Simba SC au mdumange,Hawa supporter wewe trained na taasisi ya sanaa bagamoyo au JKT wafundishwe nyimbo za uzalendo ili wao ndio watakuwa waanzilishi ktk kushangilia pale Taifa Star inapopeperusha bendera ndani au nje au timu yoyote itakayo kuwa inawakilisha taifa,iwe simba,yanga,azam ,mtibwa au mbeya city.
mwisho nakushauri unapouunda kamati tafadhali achana na mazoea jaribu kukisumbua kichwa tafuta watu makini ambao wataweza kukusaidia kufikisha mpira wa TZ pale unaamini utatupeleka,TZ hivi sasa wasanii ni wengi kuliko unavyofikiria achana na wale wanotaka kushine majina ili wakagombee ktk siasa hawana malengo ya kukuza mpira,wao ni tantarila tu.pia jitahidi kuto elimu kwamashabiki wa soka hasa vilabu vikubwa watambue kuwa wachezaji wanastahili kupata malipo halisi kutokana na jasho laowajanja wachache wasiendekezwe kuendelea kudhulumu haki zao...tulisimamie hilo la wachezaji ili endapo watapata haki yao sahihi watasaidia kupambana ktk kuendeleza mpira.....
naomba kuwasilisha.
Bwana Malinzi hebu pitia tena mgawanyo wa mapato ya viwanjani. Haiwezekani gharama za uwanja zitofautiane. Kuna baadhi ya mechi gharama ya uwanja mfano taifa inakuwa 20m zingine 50m wakati maji hakuna vyoo vichafu viti vichafu. Kwani gharama halisi ya kukodisha uwanja wa taifa ni kiasi gani???
Ni kweli ulilolisema,majadiliano yanatakiwa yaanze mid way kwenye mkutaba.Tunajipanga kupitia vitengo na kamati zetu husika.