Maswali muhimu sana kwa utumishi

hewa

Member
Oct 27, 2012
35
70
Poleni sana na kazi za kila siku za kuhakikisha kuwa sisi watanzania wenzenu tunapata ajira.
Mimi ni mtanzania ninaeishi mkoa wa Mara, ninapenda kuuliza maswali yafuatayo:
Hivi huwa mnajisikiaje kuita watu kwenye usaili kuja Dar es salaam huku mkitambua kwa hakika usumbufu na umasikini tuliyonayo sisi watanzania?
kwani hamjui kuwa:
-watafuta kazi walio wengi tunaishi mikoani vijijini kwetu kwa hiyo wengi hatuna ndugu huko Dar es salaam?
-Hiyo pesa ya kunikalisha huko Dar es salaam kwa siku zote za usaili nitatoa wapi?
-Je nyie hamtambui kuwa jiji la Dar es salaam kwa sasa lina idadi kubwa sana ya watu inayotokana na kulundikana kwa taasisi zinazotoa huduma muhimu kama hii ya kwenu?
-Nyie kama taasisi ya watanzania na siyo taasisi yawana Dar es salaam mna mikakati gani ya kuhakikisha kwamba katika mchakato wa kutoa ajira kwa watanzania unakuwa ni wa haki ukizingatia kwamba watafuta kazi wengi sana wanashindwa kuhudhuria usaili kutokana na sababu nilizozitaja hapo juu?
-kama mnashindwa kugawa vitengo vyenu kikanda kutokana na baadhi ya watendaji mlionao kukataa au kugoma kwenda mikoani mbona wapo watanzania ambao siyo wa Dar es salaam lakini bado wanasifa na wanaweza wakafanya kazi nzuri huenda kuliko hata hao?
MWISHO- je ni sahihi kwamba mtu yeyote anayetafuta kazi ni lazima atafute mahali pa kujishikiza Dar es salaam au awe na ndugu ama pesa zitakazo muwezesha kuhudhuria usaili unaofanyikia huko? Hamuoni kwamba mwishoni mtajikuta kwamba mnaajiri tu watu wa Dar es salaam kutokana na sisi wa mikoani kushindwa kuja huko kwa sababu ya michosho ya mchakato mzima katika mchakato wa ajira?
 
hewa

Member
Oct 27, 2012
35
70
kama ni hivyo wakae basi wakijua kwamba kuna baadhi ya watanzania ambao ni masikini wananyimwa haki yao ya msingi kabisa, kwani hata hivyo usaili ni kitu kinachoweza kufanyika mahali popote Tanzania na kama kufanya hivyo ndiyo kupunguza idadi ya watu basi ni bora hata hiyo tume wasijitambulishe kama wakala wa ajira wa serikali kwa sababu serikali siyo ya mkoa ni ya nchi nzima,
Wewe kama ni miongoni mwa wale wenye ndugu na mahali pa kufikia basi una bahati na hili wazo langu halikuhusu, hili wazo linalenga kusisitiza juu ya usawa katika mchakato mzima wa ajira serikalini pamoja na kupunguza idadi kubwa ya watu wanaoingia kila siku Dar es salaam. kama wanashindwa kufanya kikanda ni bora wakubali tu kuwa hiyo kazi ni mgumu na ni bora wale watakokuwa na uwezo wa kufanya hivyo wapewe ili hao wanaoshindwa wakatafute kazi nyingine itakayowafanya wakae tu huko Dar es salaam.
 
Papa-oti

Member
Oct 14, 2014
47
0
mm naona bora usaili ufanyike kila mkoa. wameniudhi xana wakati flani wameniita then nimekaa wiki na hela ya kujikimu hawajanipa
 
dumejike

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
325
195
kama ni hivyo wakae basi wakijua kwamba kuna baadhi ya watanzania ambao ni masikini wananyimwa haki yao ya msingi kabisa, kwani hata hivyo usaili ni kitu kinachoweza kufanyika mahali popote Tanzania na kama kufanya hivyo ndiyo kupunguza idadi ya watu basi ni bora hata hiyo tume wasijitambulishe kama wakala wa ajira wa serikali kwa sababu serikali siyo ya mkoa ni ya nchi nzima,
Wewe kama ni miongoni mwa wale wenye ndugu na mahali pa kufikia basi una bahati na hili wazo langu halikuhusu, hili wazo linalenga kusisitiza juu ya usawa katika mchakato mzima wa ajira serikalini pamoja na kupunguza idadi kubwa ya watu wanaoingia kila siku Dar es salaam. kama wanashindwa kufanya kikanda ni bora wakubali tu kuwa hiyo kazi ni mgumu na ni bora wale watakokuwa na uwezo wa kufanya hivyo wapewe ili hao wanaoshindwa wakatafute kazi nyingine itakayowafanya wakae tu huko Dar es salaam.
Mbona umepanic soma uelewe kwanza
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom