Maswali mengine usimuulize!

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,440
Reaction score
38,437
Habari wapendwa wa JF!

Jumamosi ya mwisho imenifundisha kuwa kuna maswali mengine siyo ya kumuuliza mke/mume, mpenzi ama mwenza wako!

Kwa sasa hivi hatuna dada wa kazi, tangu aondoke dada yetu wa kazi, ratiba zangu zimebadilika na natumia muda mwingi kuwa home na mam-sap nikimsaidia vijikazi vya hapa na pale! Jumamosi tulidamka alfajiri na kuanza shughuli ya kufua kabla mtoto wetu mdogo hajaamka na kuanza utundu wake (yule ambae nilipost kuomba msaada kuhusu kuwa mtundu)!

Basi baada ya zoezi la kufua na kazi zingine za hapa na pale, yf akaendelea na hatimaye tukawa mezani katika T! Tukiwa mezani kukawa na mazungumzo ya hapa na pale, nyingi zikiwa ni story zetu kuhusu our past! Tukakumbushana mbali, tulipotoka na hapa tulipo sasa hivi! Tukakumbushana magumu tuliopitia kila mtu kabla hatujajuana na baada ya kujuana, na baadae magumu ndani ya ndoa yetu! Kwa kifupi nilifunguka! Na yeye akafunguka sana tu!

Baadae (ilikuja akilini from nowhere, na wala sikuwa na dhamira yyt) nikamuomba yf anikumbushe mtoko wetu wa kwanza tulioufanya mwanzoni mwa uhusiano wetu (kabla ya ndoa), kwamba tulienda wapi? MAKUBWA! yf akiwa makini kabisa tena fasta! seriously, aliitaja sehemu ambayo hatukuwai kwenda hata, japo naijua hiyo sehemu! Mimi sikuwai kwenda nae! NILICHOKA!

Nikapotezea na story zikaendelea, sikutaka kumuonyesha kuwa nimeguswa (huwa anaumia sana akijuwa amenikwaza). Kuna wakati akawa ananielezea namna alivonisumbua mwanzoni mwa relation, kipindi tunaanzana, kipindi ambacho tunasomana!

Katikati ya story akanielezea kuwa siku ya kwanza mimi na yeye kulala, alininyima papuchi! Mimi nikamuambia si kweli, siku ya kwanza kulala alinipa papuchi, nikamkumbusha kuanzia namchukua meeting point, tulipoenda, alivovaa, alivotengeneza nywele, pichu color mpaka na idadi ya round nilizopiga! Yeye akabisha, akadai siku ya kwanza nilitoka kapa! Mimi nikamuomba arudishe nyuma kumbu kumbu afu anambie ni nani huyo alieenda nae chimbo afu hakumpa k**a, maana sikuwa mimi! Na yeye akanigeuzi kibao nimwelezee vzr ni nani huyo niliekwenda kumchukua pale ******* restaurant Magomeni Mapipa japokuwa anakiri kutengeneza nywele ktk style niliomuelezea, anaikubali idadi ya round, ila anakataa mavazi niliotaja!

Yote kwa yote w.end bado ilikuwa nzuri na hatukufikia mahali pa kukwazana, tulibadilisha mada na kugeukia maigizo yanayoendelea Dodoma, though nilijifunza umuhimu wa kuweka kumbu kumbu za mahusiano vzr! Nikajifunza kuwa kuna baadhi ya vitu sio vya kuuliza uliza ama laa kukumbushia!

Na wewe angalia usije ukadadisi mpaka ukalikoroga, likakushinda! Nakaribisha the like-experience!
 
kuna times unaweza kukuta mwenzako anaongea vitu awkward hadi we mwenyewe

unabaki unashangaa tu na pozi la kuendelea kuuliza linaisha
 
Kati ya wewe na mkeo nani alikuwa amepoteza kumbukumbu?
 
kwenye "likakushinda"......kama mtu ulianzisha lazima utajua jinsi ya kumalizia..


Eeeeeh ss nimekusoma, coz hata kutokuamua pia ni uamuzi na mwisho mbaya nao pia ni mwisho!
 
na kweli hata Mungu hapendi kuuliza kitu ambacho hata ukikijua hakitakusaidia..

nakumbuka kipindi hiko tuko wachumba na mr nilimuuliza mara ya mwisho kufanya ilikuwa lini na nani, akaniambia mwaka mmoja uliopita lkn hakunitajia na nani..mimi hapo nilikuwa virgin bado
baada ya kuoana nikarudia tena kumuuliza swali hilo hilo akaniambia alifanya two months kabla ya ndoa..hapo keshasahau alivonijib mwanzoni, nikasema nikimuuliza tena siku nyingine ataniambia two months baada ya kuoa, mwisho nife na prsha bure..nikaachana na maswali yasiyo na kichwa wala miguu
 

Kutaka kujua alifanya na nani hapo naona ulikuwa kweli unatafuta presha.
Maana anaweza kuwa mtu unayemjua halafu kitakachofuata utataka kujua uwezo wa mpinzani lol.
 
mmekutana wote kumbukumbu F...lol
basi tabu tupu...kapimeni hako katoto kenu...kanaweza kakawa memoryless kabisaa
walimu wakachapaa weee kumbe origin ni nyie
 
Wewe amini tu hakuna kitu kinachoitwa 'the whole truth'..
basi utaishi kwa raha sana.
Hakikisha kabisa una moyo wa shaba kabla hujayachokonoa mambo yaliyopita
 
ningependa nipate mke ambae anajutia na kuumia pale anapoona amemkwaza mumewe hasa pale anapoona kuwa katenda kosa kweli.. mengineyo tutarekebishana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…