Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 601
- 2,508
MASWALI MATANO KUHUSU MSAJILI v/s CUF.!
[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; Ukisoma barua ya Maalim Seif aliyomwandikia Spika tar.29/07/2017 hakutuma nakala kwa Msajili. Alituma nakala NEC, LHRC na CHRAGG. Lakini Msajili amekua wa kwanza kujibu. How comes? Unajibuje barua ambayo hujawa copied? Kwa ninavyofahamu kama hujawa copied means hujui na hupaswi kujua chochote katika hiyo barua. Sasa Msajili amejuaje yaliyoko kwenye barua ya Maalim Seif kwenda kwa Ndugai, hadi akafikia kujibu?
Aliyepaswa kjibu ni Ndugai aliyeandikiwa barua. Yeye kajibu kama nani? Kama Secretary wa Ndugai or kama nani? Bado haijaeleweka wazi ni kwanini aandikiwe barua mtu mwingine halafu aibuke mtu mwingine kujibu ambaye hata hajawa copied. Kama hujawa copied means barua haikuhusu, sasa unajibu nini mambo yasiyokuhusu? Ni sawa na Bakhresa amwandikie Mzee Mengi barua kuhusu biashara zao, halafu mjumbe wa mtaa wa Buguruni Malapa akazane kujibu wakati hata hajawa copied. Unajibu nini? Umeulizwa?
[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]; kwanini Spika yupo kimya hadi sasa? Tangu July 29 hadi leo, siku 5 zimepita kwanini hataki kujibu barua ya Maalim Seif? Ikumbukwe barua ya Lipumba kwenda kwa Spika ilipotumwa, Spika alikua Nigeria. Lakini usiku huohuo akajibu kwamba ameipokea barua ya Lipumba na kwamba anaitafakari (tafakuri kutokea Nigeria usiku wa manane). Watu wakahoji, barua imetumwa ofisi ya Spika Dodoma, Spika yupo Nigeria ameipataje? Tukasema huenda katumiwa kwa soft copy. Ofisi ya Spika ilijibu usiku huohuo kuwa Spika anaitafakari. Kwanini aliharakisha sana kutafakari barua ya Lipumba, lakini hii ya Maalim Seif amekaa nayo almost wiki moja sasa hajasema kitu??
[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]; Kwanini kuna double standard kwenye kushughulikia suala la CUF? Jambo likitoka kwa Lipumba linashughulikiwa haraka, lakini likitoka kwa Maalim Seif linacheleweshwa na kushughulikiwa bila kufuata utaratibu. Kwa mfano chama kikimvua uanachama mbunge wake, utaratibu ni kwamba kinamuandikia Spika. Then Spika akijiridhisha kuwa utaratubu uliotumika kumvua uanachama huyo Mbunge ni sahihi, ofisi ya Spika inaandika barua kwa NEC kujulisha kuwa nafasi hiyo ipo wazi. Kama ni viti maalum, NEC wanateua aliyekua anafuatia kwenye orodha. Na kama ni jimbo NEC inaandaa uchaguzi mwingine. Hapo Msajili anakuwa copied tu.
Hata Lipumba alipodai kuwavua uanachama wabunge 8 wa chama hicho alimuandikia Spika na Spika akawaandikia NEC. Lakini Magdalena Sakaya alipovuliwa Uanachama Spika hakuchukua hatua yoyote licha ya kwamba alijulishwa kwa barua tar 28/08/2016. Kwanini Magdalena na mwenzie Maftsha walipovuliwa uanachama Spika alikaa kimya licha ya kujulishwa kwa barua? Lakini hawa wa Lipumba hakutaka zege ilale? Ameact faster kutokea Nigeria usiku wa manane. Kwanini?
[HASHTAG]#Nne[/HASHTAG]; Baraza kuu la uongozi la CUF chini ya Maalim Seif ni lilelile msajili aliloliidhinisha tangu mwaka 2014, hata kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Lakini baraza kuu l uongozi chini ya Lipumba limeundwa majuzi tu kwa kuokoteza watu mtaani na kuwapachika vyeo. That means baraza lenye uhalali ni lile la Maalim Seif maana hata Msajili kafanya nalo kazi tangu mwaka 2014. Sasa kwanini asiendelee kulitambua baraza hilo, badala yake anatambua hili la Lipumba ambalo limeundwa bula kufuata utaratibu?
[HASHTAG]#Tano[/HASHTAG]; Msajili anasema hamtambui Maalim Seif kama Katibu Mkuu CUF, badala yake anamtambua Sakaya aliyekaimishwa nafasi hiyo. Lakini kwenye barua yake amemuadress Maalim Seif kama Katibu Mkuu. How comes? Yani unakataaje kumtambua mtu kwa kumtambua?? Msajili amemuadress Seif kama Katibu Mkuu (rejea barua yake) halafu kwenye barua hiyohiyo akasema hamtambui Seif kama Katibu mkuu. Contradiction.!!
Malisa GJ
Sent using Jamii Forums mobile app