MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
1.Enzi za Hayati Mwalimu Nyerere mpaka utawala wa awamu ya tatu alama za ufaulu kumruhusu mwananzi wa kidato cha sita au wa stashahada kujiunga chuo kikuu zilikua juu kwa sababu ya uhaba wa vyuo au kuimarisha kiwango cha elimu?
2.Zamani mtoto kufaulu kutoka shule ya msingi kwenda sekondari walikua wakichchukua mtoto ,mmoja, wawili,watatu au hakuna kabisa anayechukiwa kabisa kuendelea na sekondari kwa baadhi ya shule! Tatizo lilikua ni uhaba wa shule au ilikua ni kuimarisha kiwango cha elimu?
3.Ile ndoto ya shule za msingi kufundishwa na walimu wenye shahada ya chuo kikuu itatimia baada ya miaka mingapi?
4.Utitiri wa shule za sekondari za kata nchini kwa ufaulu wa sasa kutakua na uwiano wa walimu wangapi angalau wenye shahada ya chuo kikuu hasa masomo ya sayansi?
5.Tunakadiriwa kua na idadi ya vyuo vikuu nchini kufikia 50, Je kwa alama za ufaulu point 4(DD) kidato cha sita na GPA 3.5 kwa stashahada hasa masomo ya sayansi tuna wanafunzi wangapi kuwatawanya kwenye hivi vyuo? Au ndio vifo vya hivi vyuo vimewadia?
6. Kwa nchi kama China ambayo uchumi wake unakua kwa kasi ya ajabu alama zao kidacho cha 6 ni point 2(EE) na stashahada GPA yao ya kuanzia ni 2.0 kwenda chuo kikuu, na ndio wafadhili wetu wakubwa katika miradi mbalimbali, Je, wao hawakuona umuhimu wowote wa kupandisha madaraja ya ufaulu mpaka sasa?
7.Hawa kidato cha sita waliofaulu nchini ya point 4 wanaambiwa wakasome stashahada. Je, Stashahada hizo zitasomwa bure?