Maswali kwa Ikulu na Rweyemamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali kwa Ikulu na Rweyemamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Inkoskaz, Mar 9, 2012.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Wanajamii
  Ikulu kama taasisi ya juu katika uongozi wa taifa hupaswa kutoa taarifa na ufafanuzi wa masuala mengi ya kitaifa na yanayogusa wananchi wake na hasa panapokuwa na mikanganyiko ama ububu kutoka katika idara au ofisi husika

  Pia malamiko na vilio vingi vya mwananchi wa kawaida ni nadra kuifikia taasisi hii kutokana na taratibu na ukiritimba uliojengeka
  Nakumbuka kipindi cha nyuma TBC1 waliandaa kipindi kikiongozwa na Tido na Suzan kuwakilisha maswali ya wananchi yaliyowasilishwa kwa live calls,sms na emails,japo hakikufanikiwa sana kutokana na mjibu maswali kutumia muda mrefu kujibu maswali na kutumia takwimu zaidi kujibu maswali lakini nia ilikuwa ni njema na muda haukutosha

  Kwa kuzingatia muda,uhuru wa kuuliza na pia privacy ya muulizaji nadhani wigo huu wa wananchi kuuliza maswali yenye KERO SUGU na AHADI zisizotimia na ambazo wahusika wanazifumbia macho na kuziba masikio ungeendelea na kujibiwa na msemaji wa mwisho ama kupitia kwa wasaidizi wake na kurugenzi husika ya bwana SALVA

  Kwa kuanzia hapa JF tunaweza kupost maswali yetu na iwepo filtration ya utumbo na kebehi na bwana salva ayatafutie majibu hata mara moja kwa wiki
  Pia hata Mkuu ule muda anaokuwa FB na Tweeter sio mbaya akija hapa na kujibu direct kama anaona inabidi
  Tunaishi katika ulimwengu wa Teknolojia hebu twende kiteknolojia
  NAWASILISHA
   
 2. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  hivi kama Ikulu inaweza kuwa na email address ya yahoo ni kwa nini isiwe na ID hapa JF??

  Inakuwa sio vizuri hawa wakuu kuingia hapa kwa ID za siri, ni kwa nini wasiwe kama Mh. Regia (Mungu ailaze peponi roho yake), Zitto, Myika, Dr. Slaa nk. Kama raisi anakuwa na account facebook na tweeter, ni kwa nini isiwe hapa jf! Maana hapa kuna members zaidi ya 66,000 na wengi sana wasio members nao wanakuja hapa ...ni gazeti gani tz linauza nakala zaidi ya 66,000?? Hii ni kuonyesha kuwa hiki ni chombo potential kwa kuwasiliana.

  Kwa hiyo mkuu Inkoskazi naunga mkono wazo lako lakini hata tukiweka maswali hapa hawa jamaa kwa dharau na upuuzi wao nifikiri hawatayajibu.
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180


  Mkuu Lukindo Asante sana!
  hata kama kwa dharau zao watasoma na hawatajibu lakini tutakuwa tumetimiza wajibu wetu na dhamira pia hata itakapofika siku yake tutawaambia we asked so and so na mkatuignore
  unajua hata Jambo Forum ilipoanza wala hawakuwa wakiisoma lakini imefikia hatua ya kujadiliwa kwenye vikao vyao vya juu hivyo kwa lugha nyingine message sent and delivered
  Imagine ahadi zile za uchaguzi mkuu tungeuliza hapo na mengineyo hata hivi mkutano umeahirishwa mdugu Salva angetupa official answer kuliko kama sasa kila mtu anaguess kivyake
   
 4. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ushauri utakuwa umefika.......uamuzi sasa!!!!!!!!!!!!!???????????????????
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180

  OLESAIDIMU
  katika jambo gumu kwa watanzania kuanzia huko juu ni MAAMUZI. yani kukamilisha kazi huwa ni kugumu kuliko kazi yenyewe
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  hivi Ikulu haiwajibiki kulitoliea ufafanuzi suala la kuibiwa vifaa Waziri mdogo wa Nishati na Madini, Adam Malima katika mazingira yasiyoeleweka yaliyopelekea wananchi watano kuwekwa ndani!?

   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  hiyo ni siri sirini..watateswa hao mateja lakini huo ukweli kamwe hatutoujua
   
 8. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  wewe mbona huweki jina lako hapa?

  Anyhow, Watanzania wangapi wanaingia JF kupata taarifa na kutoa dukuduku zao?
   
 9. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Anheuser
  Verified User wengi ni wanasiasa na wale ambao forum hii na nyinginezo ni kwa ajili ya kupanua wigo wao wa kupata maoni na pia kufafanua hoja zao.na pia wenye misimamo na kutetea kile wanachokisema.wao pia ni public figures na popular..mimi hata nikijiandika hapa ALLY HUSSEIN hutanijua bado ni nani wala career yangu
  Wanaosoma jf ni wengi kuliko hata hao members japo ujumbe unatakiwa kuwafikia hao mabwana wakubwa wachache
   
 10. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa uelewa wangu mdogo uloniwezesha nami kuwepo ktk jamvi hili nadhan Ikulu si jukumu lao kulitolea ufafanuzi suala la Mh.AM mwenye jukumu hilo ni yeye mwnyw tena kwa kuzingatia yupo hai na ndicho alicho kifanya Bw. AM
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  hata wao wanaweza kufafanua zaidi kama mtaoa taarifa hakua ametoa maelezo ya kutosha,wanayo overide power
   
 12. SR senior

  SR senior JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 342
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  ....unajua wanafahamu mapungufu yao, wanaogopa maswali yatakayowaua kwa haraka, wanaona bora wafe taratibu kuliko haraka, wapuuzi wakubwa wasiotambua mateso ya wananchi wao.....mtumishi aipendaye ccm hakika ni kichaa, mishahara midogo gharama za maisha zipo juu......ewe kijana amka leta mabadiliko walau tujiridhishe kiroho, KAMA WALIVYOJIRIDHISHA ARUMERU.
   
 13. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Hakika kilichobaki ni kuwaumbua
   
Loading...