Sidhani kama ni busara kumsakama mama wa watu kwa tuhuma zisizokuwa na ukweli ndani yake. Kwanza huyu mama hakuna mahali tumesikia katamka kwamba anataka kugombea urais 2015, ingawa ana haki ya kufanya hivyo akitaka kwani katiba inaruhushu kufanya hivyo na zaidi sana tukizingatia kuwa Dr. Asha-Rose ni mwanasiasa kama wanasiasa wengine. vinginevyo ninachokiona hapa ni kwamba huyu mama bila shaka inaonekana ni tishio katika harakati hizo za 2015 ndio maana anaundiwa zengwe ili kumkatisha tamaa.
Ndio, nasema hivyo kwani sioni mantiki kumsakama mama huyu ambaye kwa mujibu wa taarifa rasmi za UN amesifiwa sana kwa uadilifu na utendaji kazi wake kiasi cha Bw.Moon hata kuamua kuamteua kuwa mwakilishi wake maalumu barani Afrika katika masuala ya UKIMWI. Hii ni kuthibitisha ni kwa namna gani UNSG anavyomkubali huyu mama kwa utendaji kazi wake . Mimi nimepata neema ya kuishi katika mataifa mbalimbali yaliyoendelea ikiwemo Marekani ambako niliwahii kukaa huko kwa miaka 4. Nawajua hawa ndugu zetu, hawana unafiki kama huku kwetu kwenye nchi za dunia ya tatu. Wenzetu kama umeharibu wanakuambia wazi umeharibu na hawana kabisa unafiki wa kusisifia na kukupamba wakati wanajua umeaharibu,hata kidogo.
Lakini tunachokiona kwa Mh.Mama Migiro ni tofauti kabisa. Sifa za utumishi wake uliotukuka zinazotolewa na vigogo na hata watumishi wa kawaida aliowahi kufanya nao kazi pale UN.
Naomba nieleweke, sina maslahi yoyote na mama huyu. Bali kama mtanzania nakereka sana na shutuma zisizo na ukweli wowote anazopewa mtanzania mwenzetu huyu ambaye kiukweli amelipatia taifa letu heshima kubwa sana Duniani. Kwa wale waliobahatika kushiriki/kujichanganya na watu makini Duniani wataelewa nazungumza nini.
Natambua,Dr.Asha-Rose Migiro kama binadamu anaweza kabisa kuwa na mapungufu yake. Hilo silipingi hata kidogo. Lakini kumlundia shutuma za kupandikiza kama vile za udini na udhaifu wa kiutendaji kazi, ni kutomtendea haki. Maana nimeshangazwa na mdau mmoja humu kusema eti mama huyu alikuwa mtu wa kuvaa maushungi tu pale UN, jambo ambalo si la kweli kabisa. Natambua, kwa mujibu wa imani yake wala haikuwa tatizo kwake kuvaa ushungi. Hatahivyo, mimi kama mfuatiliaji mkubwa wa masuala mbalimbali ya UN,sikupata hata mara moja kumuona kavaa ushungi. Isitoshe, hata huku nyumbani kabla ya kwenda UN,sikuwahi kumuona akivaa mavazi hayo labda kwa siku alizokuwa akienda kwenye ibada. Nameona niliseme hili kuthibitisha ni kwa namna gani kuna watu wanaonesha dalili za wazi kabisa za chuki binafsi kwa mama huyu.Haipendezi hata kidogo. Kwa kusema haya si maana ya kumshawishi kila mtu amsifie mama huyu maana najua tunatofautiana kimtizamo. Lakini hoja yangu ni kwamba ni bora mtu ukaa kimya kuliko kuzusha tuhuma pandikizi.
Dr.Asha-Rose Migiro, karibu nyumbani mama na watanzania makini tunatambua mchango wako mkubwa katika nyanja ya diplomasia ya kimataifa kiasi cha kutufanya kujisikia fahari kubwa kila tutembeapo sehemu mbalimbali za ulimwengu huu.
Mungu ibariki Tanzania!!!!
Nchi ina vituko hii, huyu mama nae anautaka Urais! yaani baada ya haya yooote bado kweli mtu kama huyu anawaza kuwa Rais! pamoja na udhaifu woote huu...
.... Nikajiuliuliza tena, rose migiro anafanya kazi gani? Ni mama wa ofisini tuu? Nilimsikia
alipoteuliwa kuwa kaimu katibu mkuu [un] sikumsikia tena hadi hivi sasa ninapomsikia akiwa kamaliza
muda wake wa miaka mitano. Swali kubwa: Muda wote huo akiwa un, migiro alikuwa anafanya nini?
Sidhani kama ni busara kumsakama mama wa watu kwa tuhuma zisizokuwa na ukweli ndani yake. Kwanza huyu mama hakuna mahali tumesikia katamka kwamba anataka kugombea urais 2015, ingawa ana haki ya kufanya hivyo akitaka kwani katiba inaruhushu kufanya hivyo na zaidi sana tukizingatia kuwa Dr. Asha-Rose ni mwanasiasa kama wanasiasa wengine. vinginevyo ninachokiona hapa ni kwamba huyu mama bila shaka inaonekana ni tishio katika harakati hizo za 2015 ndio maana anaundiwa zengwe ili kumkatisha tamaa.
Ndio, nasema hivyo kwani sioni mantiki kumsakama mama huyu ambaye kwa mujibu wa taarifa rasmi za UN amesifiwa sana kwa uadilifu na utendaji kazi wake kiasi cha Bw.Moon hata kuamua kuamteua kuwa mwakilishi wake maalumu barani Afrika katika masuala ya UKIMWI. Hii ni kuthibitisha ni kwa namna gani UNSG anavyomkubali huyu mama kwa utendaji kazi wake . Mimi nimepata neema ya kuishi katika mataifa mbalimbali yaliyoendelea ikiwemo Marekani ambako niliwahii kukaa huko kwa miaka 4. Nawajua hawa ndugu zetu, hawana unafiki kama huku kwetu kwenye nchi za dunia ya tatu. Wenzetu kama umeharibu wanakuambia wazi umeharibu na hawana kabisa unafiki wa kusisifia na kukupamba wakati wanajua umeaharibu,hata kidogo.
Lakini tunachokiona kwa Mh.Mama Migiro ni tofauti kabisa. Sifa za utumishi wake uliotukuka zinazotolewa na vigogo na hata watumishi wa kawaida aliowahi kufanya nao kazi pale UN.
Naomba nieleweke, sina maslahi yoyote na mama huyu. Bali kama mtanzania nakereka sana na shutuma zisizo na ukweli wowote anazopewa mtanzania mwenzetu huyu ambaye kiukweli amelipatia taifa letu heshima kubwa sana Duniani. Kwa wale waliobahatika kushiriki/kujichanganya na watu makini Duniani wataelewa nazungumza nini.
Natambua,Dr.Asha-Rose Migiro kama binadamu anaweza kabisa kuwa na mapungufu yake. Hilo silipingi hata kidogo. Lakini kumlundia shutuma za kupandikiza kama vile za udini na udhaifu wa kiutendaji kazi, ni kutomtendea haki. Maana nimeshangazwa na mdau mmoja humu kusema eti mama huyu alikuwa mtu wa kuvaa maushungi tu pale UN, jambo ambalo si la kweli kabisa. Natambua, kwa mujibu wa imani yake wala haikuwa tatizo kwake kuvaa ushungi. Hatahivyo, mimi kama mfuatiliaji mkubwa wa masuala mbalimbali ya UN,sikupata hata mara moja kumuona kavaa ushungi. Isitoshe, hata huku nyumbani kabla ya kwenda UN,sikuwahi kumuona akivaa mavazi hayo labda kwa siku alizokuwa akienda kwenye ibada. Nameona niliseme hili kuthibitisha ni kwa namna gani kuna watu wanaonesha dalili za wazi kabisa za chuki binafsi kwa mama huyu.Haipendezi hata kidogo. Kwa kusema haya si maana ya kumshawishi kila mtu amsifie mama huyu maana najua tunatofautiana kimtizamo. Lakini hoja yangu ni kwamba ni bora mtu ukaa kimya kuliko kuzusha tuhuma pandikizi.
Dr.Asha-Rose Migiro, karibu nyumbani mama na watanzania makini tunatambua mchango wako mkubwa katika nyanja ya diplomasia ya kimataifa kiasi cha kutufanya kujisikia fahari kubwa kila tutembeapo sehemu mbalimbali za ulimwengu huu.
Mungu ibariki Tanzania!!!!
Hijjat Asha Migiro ni empty vessel kabisa. Ni mdini sana huyo!
Nyamaza pambaf huyu mama kaaribu sana UN na hiyo miushungi yake
Hivi una maaana gani kusema huyu mdini? naomba funguka zaidi mkuu