Mkuu, Mshana jr, mimi natofautiana na wewe, with due respect, nasema kwamba Uchawi/Magic ni tawi moja la Elimu ya sayansi lakini kwa kipindi hiki ni elimu ambayo haipo wazi kwasababu inakiuka morality ya ubinadamu ili ifanye kazi na pia principle ya kiubinadamu ni kwamba chochote chenye manufaa huwa kinapata maendeleo, (whatever useful must be developed and won't be kept a secret over long time).
Mfano, wachawi hutumia dawa/ nguvu ya kutokuonekana pindi wanapofanya mambo yao ya "kihalifu" (invisibility power), inakuwa vipi??, mimi sijui wanatumia vitu gani kujipakaza mwilini, lakini ni kwamba mchanganyiko materials wanazotumia kujipaka mwanga unapogusa (strike) hizo material mwanga unaorudishwa (reflected ) unakuwa umebadilika mawimbi yaani maeimbi hayo yanakuwa nje ya ile inayoitwa visible spectrum ya uwezo wa macho ya mtu kuona na ndiyo maana kuna viumbe wengine wanaweza kumuona mchawi wa aina hiyo kwa sababu wao visible spectrum yao ni kubwa kuliko ile ya mtu.
Nadhani unajua ni jinsi gani sisi binadamu tunaweza kuona vitu.
Mfano huu unafanana na stealth fighter jet ambayo radar inashindwa kuiona/ku-detect kwa sababu inameza mawimbi ya radar au inayarudisha katika mawimbi mengine kuweza kutambuliwa na radar.
Hapa swali ni mchanganyiko wa material zipi zinafanya mchawi asionekane??!;, ukiuliza unaweza kuambiwa huo mchanganyiko na ukashangaa na ukajuta kwanini uliuliza.