Masuala muhimu kwanza halafu haiba ya mtu

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Watu wanauliza hivi tumeanza mchakato wa kumtafuta mrithi wa JK sasa! Alama ya mshangao ni kwa wale waliobebwa na mazingira na si kwa wale ambao wana tawala mazingira yao. Ukigundua umekosea mtihani na hauna jinsi ya kurekebisha makosa yako, unaanza mara moja kujiandaa kwa mtihani mwingine. Elfu mbili na tano tulichagua tabasamu, elfu mbili na kumi tulitumia huruma iliyojificha katika kazu na mbebo ya udini. Safari zote hizi hatukupata zao la kisiasa ambalo litatufikisha katika nchi ya ahadi. Ni wajibu wetu kujiuliza kwa nini si bahati kwetu Watanzania kupata nuru ya bwana katika kufanya maamuzi ya kisiasa?

Ni vema kujiuliza mapema ili tuepuke kuruhusu hoja za kujaza tumbo kutuongoza kupata kiongozi katika kipindi kijacho. Sasa Jamii forum tutengeneze hiyo suti ya hitaji la kisiasa ili wanaopenda kutuongoza wajipime humo wapo ambao itawabana na wapo ambao itawapwaya na mmoja au wawili kati yao itawatosha na hao ndio tuwapeleke wakashindane ili tupate moja. Wataalamu hatuwezi kusubiri kufanyia mazoezi ya kushinda mechi wakati timu ziko uwanjani kwa maandalizi ya mechi kuanza. Hayo mambo ya muhimu ndio vyama vipambane kuyaandallia ilani zao kwa ajili ya kutuuzia. Wanaharakati tuchore picha ya tanzania tuitakayo miaka 30 ijayo katika kila sekta ili wanasiasa waseme watatufikishaje huko kwa kutumia ilani zao. Ilani nzuri haiwezi kuandikiwa mezani inaandikiwa field na kwa maono ya mahitaji ya wanachi, kama walivyoigusia hali ya makaazi ya vijini CDM na mtu anayetaka kutuongoza ilani yake lazima iwe kichwani, huwezi kuwa Rais mambo ya ilani yako mpaka usome kwenye kitabu, hujui utatatuaje tatizo la umaskini nk.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom