ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,532
- 21,533
- Thread starter
- #21
My people,
Katika huu ulimwengu ambao watu hatuthamini maneno tunayoyatamka au ahadi zetu,ni tabia ambazo tumejijengea na karibia jamii yote inaona sawa tu.
Ni kawaida sana kumwambia mtu kwamba utamlipia tiketi ya onyesho la mpira labda next month lakini huku ukijua hautatimiza unacho kisema
Unaazimia kwamba kuanzIa sasa utaanza kufanya mazoezi ili kuweka mwili wako safi,lakini hautimizi maazimio yako au malengo yako
Unaazimia kwamba kuanzia sasa utakuwa mtu mwema na mwenye upendo kwa jamii yako,lakini kwa upande wa pili huyaishi hayo unayo yakusudia
Unajiahidi kwamba from now you will be a good husband or a good wife lakini mwisho wa siku hauyaishi hayo unayojiahidi,unaazima utakuwa a responsible parent lakini hautekelezi hayo maazimio yako
Haya na mengine mengi ambayo unataka yawe,hayawezi kutokea kama hauna Filosofi imara
Lazima uamue kwa moyo wa dhati kabisa kwamba kuanzia sasa nitakuwa na strong philosophy ya kuyaendea mambo yangu na nitahakikisha nayaishi na kuyatekeleza
Baada ya kuamua kwa dhati na kuamua kuyaishi basi the rest itakuwa kama kunywa maji tu,na ikiwezekana jiwekee adhabu mara pale unaposhindwa kuishi kutokana na filosofi yako,mfano unaweza kujipa adhabu ya kujizuia kufanya yale mambo ambayo huwa unayapenda sana,mfano huwa labda kila wikiend huwa unafanya mtoko fulani basi jipe adhabu ya kutotoka,na mfano wa mambo kama hayo
Hii itakuwezesha kurudi kwenye mstari na kuendelea pale ulipoishia,kwahiyo kadri jinsi siku zinavyozidi kwenda utajikuta unakuwa mwanachama mwaminifu wa filosofi yako mwenyewe
Kumbuka vile vile ukiwa mtu ambaye huwa unaahidi watu mambo ambayo huwa huyatekelezi,au unakuwa muongo muongo mwisho wa siku unashusha heshima yako na kudharauliwa kabisa
Poteza vyote lakini sio heshima yako.
Ni hayo tu!