Master plan ya Lowassa ni ipi?

Hata uwe na katiba bora kiasi gani kama hakuna busara na weledi na utashi wa kutekeleza yaliyomo itakuwa kazi bure.
Pia katika hali ya kawaida katiba haiwezi ikawa bora na ikasimamia kila kitu kwa matakwa ya kila mtu au kila kikundi. Hivyo katiba iliyopendekezwa na tume ya katiba sio SULUHISHO la matatizo yetu bali ni mwanzo mwingine.
Itakiwa yeyote anayesema atairudisha katiba au rasimu hiyo atueleze ni kitu gani atakachosimamia na kutekeleza.
 
Mabadiliko yepi hayo, yaani uchukue nguo chafu uifue kwenye maji machafu alafu uwaambie watu utapata nguo safi? dawa ya uchafu ni sabuni, Lowasss ni mchafu hawezi kutumikà kama sabuni kuifanya nguo iwe safi zaidi zaidi anaongeza uchafu
 
sasa mbona lowassa huyu huyu alikua anapinga rasimu mpya ya katiba, au alipokatwa ccm akaona inafaa?
 
unataka master plan kwani unataka kucopy kitu gani mkuu.
Jiulize tumekuwa na master plan ngapi tangu uhuru. Je tunasonga ama tunatudi?
Usikute hhata hata master yaafamiliamyako yako.
sitaki kukopi chochote nataka nione alafu nipime ndio nijue nitampigia kura nani kwenye urais
 
Lowassa akiwa Morogoro
😃😃😂😂😂👇🏿

"tutaimarisha reli kwa kiwango cha lami"...

☝🏿☝🏿☝🏿😃🙌🏿
 
elimu..elimu..elimu..kilimo..afya..mawasiliano..na kama hauna uccm kwa sasa tanzania tunahitaji vitu kama hivyo..itasaidia vijana kujitambua na kuacha kuongea pumba humu jf ili akapate buku 5 pale lumumba..
ok, elimu, elimu, elimu.. Mbona hajaelezea elimu itaiboreshaje sasa, tuna wahitimu ambao hawawezi kuajiriwa kwenye nchi yao ila wanaletwa wageni kisa wazawa hawaaminiki na elimu yao mr lowassa atalifanyaje hili?
 
kwanza kabisa haina haja ya kutukana tunajadiliana ili tujue rais bora ni yupi, pili kuhusu katiba mpya lowassa alikua hana mpango kabisa na rasimu ya warioba hadi alipokatwa ccm ndio akaenda ukawa ambayo tayari ilikua na ilani yake
 
nashukuru kwa kujibu bila kejeli au matusi,jf inatakiwa kuwa hivi sio kama genge la wahuni
 
shukrani kwa mchango wako
 
unadai umefuatilia ila ulivyoandika inaonyesha kabisa hujafuatilia
imejaribu ila sijaona kama wewe unajua zaidi yangu tuelimishane lengo langu sio ushabiki
 

Ukweli Lowasa anahitaji kutoa ahadi inayoeleweka jinsi ya namna atakavyoshughulikia katiba. Sijamsikia akizungumzia jambo hili ambalo kimsingi ndio roho ya Tanzania yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…