Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,374
- 38,248
Wabongo tunajua sana ku-copy na ku-paste!
Ona mifano hii kutoka tasnia mbalimbali, ruksa na wewe kuongezea alie-copy na ku-paste:
Ona mifano hii kutoka tasnia mbalimbali, ruksa na wewe kuongezea alie-copy na ku-paste:
- Daz BABA: Huyu ni memba wa lililokuwa kundi la DAZ Nundaz. Kwa USA, Daz ni jina la jamaa anaitwa Daz Dillinger, alikuwa mtu wa karibu sana na marehemu 2Pac.
- B12: Kwa hapa bongo huyu ni presenter, lakini kwa USA, B12 ni msaii mkubwa sana.
- Young D: Kuna wasaniii wengi sana USA wana majina yanayoanza na Young, akiwemo Young Buck. Kwa hapa bongo, dogo anasema jina lake lina maana ya Young Dar es salaam, inawezekana!
- 2 Proud: Ni mheshimiwa kwa sasa. Alivuma sana kwa jina hili enzi hizo 2pac Shakur anavuma USA na dunia kwa ujumla.
- Soggy Doggy: Huyu nae aliwika katika zama zake. Jina lake halina tofauti sana na mkali wa USA, Snoop Doggy Doggy
- Mad ice: Huyu ni kama vile ameboresha jina la Ice cube.
- Chid benz: Kule USA kuna msanii anaitwa Benzino
- Bambataa: Hiki ni kipindi kilichovuma sana enzi za uhai wa Amina Chifupa, kabla hajaingia ktk siasa, sasa hivi hakipo tena. Kwa waliokuwa wapenzi wa burudani, hili ni jarida maarufu sana kule USA.
- Diamond platinum: Kwa USA, platinum ni chati za juu kabisa za mauzo ya album ya music kwa msanii husika, kibongo bongo hili ni jina la msanii!
- 20%: Huyu alijiwekea jina baada ya kubeba tuzo 5 kwa mpigo ktk KiliAwards. Kule USA kuna mkali anaitwa 50 CENT
- Queen Darleen: Huyu karibu kila kitu; uvaaji na aina ya uchezaji wake, anafanana na Queen Latifa
- J – Mo: USA wanae J – Lo, kwetu huku tunae Juma Mchopanga
- Fanya yako: (Do ur thing): Kwa wapenzi wa kituo cha burudani BET, huu ni msemo maarufu sana kwao, hapa kwetu unasemwa ktk lugha ya Kiswahili!