Maskini Ronaldinho sasa Ajipendekeza kwa Messi


Companero

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Messages
5,498
Points
1,250
Companero

Companero

Platinum Member
Joined Jul 12, 2008
5,498 1,250
Masaa machache kabla ya 'La Pulga', yaani 'The Flea' ama 'Kiroboto' kama anavyojulikana Messi, kuvunja rekodi ya Muller ya kupachika mabao, veterani Ronaldinho amesikika akijipendekeza. Mkongwe huyo anayezidi kuisha na kusahaulika katika medani ya kabumbu ametumia ile janja Waingereza wanayoiita 'famous by association', yaani 'umaarufu kwa kuhusiana', kudai kuwa mrithi huyo ya Maradona ana nafasi muhimu moyoni mwake. Mchezaji huyo Zilipendwa ambaye matumaini yake ya kuonekana kwenye uwanja wa kihistoria wa Maracana mwaka 2014 kwenye kombe la dunia yanazidi kufifia kama mwanga wa kibatari kilichoisha mafuta licha ya kuteuliewa kwa kocha wake wa zamani, Big Phil, kuiongoza Selecao anataka walau akumbukwe na manazi wake kina Gang Chomba kwa kumpa pasi Messi siku alipofunga goli lake la kwanza. Eti yeye Gaucho alikuwepo siku ilipoanza safari ya kuelekea kwenye umaarufu ya mpiga chenga na mabao huyu machachari ambayo mchezaji mwenzake wa timu ya Barca, Gerald Pique, amekiri kuwa anacheza mpira usio wa asili ya kibinadamu. Hebu jisomee mwenyewe kujipendekeza huku:

As Messi closes in on Gerd Muller's record of 85 goals in a calendar year, Ronaldinho paid tribute to his former Barcelona team-mate. "For me Messi is the best in the world," he added. "For the last few years he has played at a level of football we have never seen before. "I'm very proud to speak of him, because I was there when he started off and now he is the best in the world, it makes me so happy. "The game I remember the most is when he scored his first goal, because it came from my pass and I remember this game most vividly because he was just getting started. "I had the chance to be there and live that moment. I'm very happy that his first professional goal came from a pass from me. Messi knows that there will always be a place in my heart for him" - Ronaldinho: Neymar will be the world's best - ESPN FC
 
Gang Chomba

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
9,123
Points
2,000
Gang Chomba

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
9,123 2,000
Only Ronaldinho can win a man of the match without touching the ball and without being in filed
 

Forum statistics

Threads 1,285,557
Members 494,675
Posts 30,866,727
Top