Dr.Menuka
Member
- Aug 10, 2013
- 14
- 2
Nini kifanyike nchi inapokosa wa kuisemea?? Tumeambiwa nchi imesimama haiendelei tena hali vijana wake wapo bize na malumbano ya kidini na siasa! Ndg zangu,yapo mambo mengi yanazungumzwa sasa ktk mitandao mbalimbali lakini kwa bahati mbaya wazungumzaji wote wanatofautiana mawazo(hawana umoja) kulingana na dini ama chama cha siasa!
Itoshe kusema kuwa wote hatuelewani lugha kwa kuwa kila mtu anavutia kwake ,halafu kwa mlengo huo tunasema kuwa tunataka kuijenga nchi yetu!Kwa kawaida nchi haiwezi kujengwa ktk utofauti wa wajenzi wenyewe ktk itikadi na ubaguzi wa imani.
Wana JF wakati umefika tujue kuwa hatima ya nchi yetu ipo mikononi mwetu bila kujali tofauti zetu,tunatakiwa kuijenga nchi hii! Ni ujinga sana na utumwa wa kifikra kutetea jambo la hovyo eti kwa kuwa limesemwa na kiongozi wako ama wa dini au siasa" Ujinga huu tuukatae! ukweli usemwe wazi na uovu ukemewe wazi na sote bila kujali tofauti za imani ama itikadi ili tujenge nchi ambayo sasa haina wa kuisemea.
Nchi ni vijana na wao ni sisi,utumwa wa fikra ni mauti ya taifa.Lazima tujiulize kuwa nani katufikisha hapa? Tutatokaje hapa? Nani atatutoa hapa? na lini tutatoka hapa?
Mimi nasema 'NCHI YANGU KWANZA'