Maskani Fama Gusta-Mikoroshini - Temeke...

Maskani Fama Gusta-Mikoroshini - Temeke...

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,638
Maskani FAMA GUSTA-MIKOROSHINI - Temeke...
Hili ni eneo maarufu sana kwa Temeke Mikoroshini Gusta hapa palikuwa hatari enzi hizo mwisho kutembea ilikuwa saa 12 baada ya hapo unatafuta lawama na watu. Kama kuna mwenye picha ya miaka ya 90 na 80 atuletee... Kuna wimbo mmoja wa Mchiriku walitaja sana sehemu hii.. Sikumbuki wimbo gani.. Nani anaukumbuka?
 
Duuu asee kitambo sana. Fama Gusta sijui manake nini ila ilikuwa maarufu sana enzi hizo palikuwa na wahuni vibaka Wa hatari.
 
sio tu FAMA GUSTA-MIKOROSHINI bali temeke yote ilikuwa hatari kipindi hicho na mpaka leo kipindi cha mbwa mwitu
 
Tulikuwaaa Maskaanii
Maskaanii Famagustaa

Kukaa kidogo kaja mtu...
Kaaja anatuuliza
Eti Kipaka kafa saa ngapi...

Watu wote tukashangaa..!
Tulikuwa hatuna habari

Kwenda kuuliza kumbe kweli!

Siiyo yeye peke yakeee
Safari hii yetu soteee
Yeye ametangulia...
Hata iwe vp na ww utakufa tu
Aiseee
 
nimemkumbuka mchapanya na nduguye magomba. wakabaji wa tandika na temeke mikoroshini miaka ya 90.

hivi bado wapo hai hao jamaa?
 
Duuu asee kitambo sana. Fama Gusta sijui manake nini ila ilikuwa maarufu sana enzi hizo palikuwa na wahuni vibaka Wa hatari.
Kuna baharia mmoja alinambiaga Cyprus kna sehemu inaitwa hivyooo....

Ova
 
Kwa sasa eneo moja tu la Zamani limebaki kuwa Soweto, hapa hadi sasa ukipita mida mibovu unajitafutia lawama na watu.

Utakwapuliwa ama Kukabwa watu wanakutizama...!!
 
Pia kulikuwa na daladal moja la Temeke Stesheni liliandikwa fama gusta lilikuwa na music wa kufa mtu.aina yake Benz
 
nimemkumbuka mchapanya na nduguye magomba. wakabaji wa tandika na temeke mikoroshini miaka ya 90.

hivi bado wapo hai hao jamaa?
Magomba kafariki mwaka 2016 na sadam amefariki 2019
 
Back
Top Bottom