kabiriga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 1,101
- 1,154
Nilimuona kwa mara ya kwanza mwaka Jana maktaba ya chuo nikapendezwa nae ,niliona Kama anafaa kuwa mke wangu baadae,Nilifanya kila juhudi kuongea nae ,hatimae nikakutanishwa nae na dada mmoja rafiki yake kwenye mgahawa mmoja karibu na campus yetu.
Alikubali kunisikiliza kwa makini na utulivu mkubwa,Kisha akaniambia "Nimekuelewa kaka lakini naomba unielewe siwezi ".Ni baada ya kumwambia hadhima yangu ya kutaka kumuoa awe mke wangu.Nili heshimu mawazo yake nikaagana nae .maisha yakaendelea.
Mapema mwaka huu nilihitimu masomo yangu na kurudi nyumbani .Ni juzi tu nili shangaa kuonana na msicha huyu nyumbani kwetu,ingawa moyo wangu ulikuwa tayari umemsahau.
Sikujua kama alikuwa ananifatilia na tulikuwa tunaishi mji mmoja.Ni dhahiri kuwa nae alikuwa akinifatilia na alinipenda ,kwani ali alifanya juhudi kubwa mpaka kufika nyumbani.
Ndipo akanieleza kiini cha habari hii:" T nikwambie ukweli nimefanya Kazi kubwa ya kuzuia moyo wangu lakini nimeshindwa naomba mkwambie na kupenda pia lakini nilikataa ombi lako kwa kuwa nilikuwa na sababu maalum ambayo ndiyo sababu iliyonifanya nikatae kwa wakati ule ,nilitafakari sana nikaona pamoja nawe tuta tatua jambo hili Kisha tuanze maisha ya ndoa ,unajua Mimi nilianguka mtihani wa darasa la 12 na baba akaniambia hana uwezo wa kunisomesha fani yeyote,nilikaa hapo nyumbani kwa muda wa mwaka mmoja na nikakata tamaa na nikaona maisha yangu yataishia mikononi mwa wanaume ingawa sikuwa tayari kuolewa bila kuwa na kazi yangu.
Nilikutana na Baba mmoja mtaani kwetu akahaidi kunisaidia ingawa alikuwa anaishi mji mwingine wa jirani,akaniambia hapendi kutangaza msaada wake hivyo alinitaka nitafute shule nirudie masomo ya kidato cha nne ata lipa ,nilimshukuru nikatatuta shule nje ya mji hivyo ilipasa kuhamia huko kwa kupanga maana shule haikuwa ya bweni na alinipa pesa ya pango.baada ya miezi 6 alinipigia simu tukutane kwenye hotel moja aweze kunipatia pesa ya Ada na matumizi,nilienda huko na matokeo yake aliishia kunilazimisha kufanya nae mapenzi na ikawa ndio mwanzo wa mahusiano na baba huyo wa familia.Nilifanya mtihani wa mwisho na kupata daraja la tatu na kusoma kidato cha tano mpaka 6 kwa pesa ya huyo baba,ndipo nikafanikiwa kwenda chuo,sasa namaliza masomo mwakani na siitaji kuwa na mahusiano na huyo baba na ni kikwazo kwa maisha yangu ,kwani nahitaji mme wa kwangu peke yangu kwani Yule ana mke wa ndoa sitaki kuwa kimada.Naomba unisaidie niondokane na hili tuwe mke na mme na ata kama unitaki basi nipe ushahuri nifanye je kuachana nae.Chonde kaka wewe tu ndo nakwambia Siri hii na nadhani nitapata suluhu ya kudumu kwa jambo hili"
Niliishiwa nguvu baada ya maelezo yake na nikaona kabisa anahitaji ushahuri wa kina na ukaribu wa kipekee kabla ya ushahuri .Niliona sio vizuri kumpa jibu lolote kwa haraka,Binafsi napata ugumu nini nimshahuri ukizingatia kuna uwekezaji wa pesa za huyo baba na kuna maisha ya huyo binti kwani baba huyo ana mke na watoto. Wana janvi naomba ushahuri wenu .tafadhari kama huna ushahuri wewe pita tu maana kuna watu humu uwa siwaelewi.