Masikini anahitaji siasa nyingi au ubunifu ili maisha yake yabadilike?

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Ni kweli kabisa uhuru wa mawazo na maoni huchangia katika kuifanya jamii iweze kufaidika na kila kipaji cha anayeishi kwenye jamii hiyo.

Ni kweli kabisa kila kipaji kinachoumbwa na Mungu kwa kusudio la kukiwezesha kubadilisha maisha ya wote wanaomzunguka aliyejaliwa kipaji hicho.

Ni kweli kabisa demokrasia haikamiliki pasipo kuwepo kwa uhuru wa mtu mmoja au kundi fulani la watu , kutoa maoni na uhuru wa kusikilizwa.

Lakini katika umasikini huu wa Tanzania, demokrasia peke yake inatosha kuwa kichocheo cha maendeleo ya wote?.

Uanaharakati na nguvu za ushawishi wake, unatosha kweli kutegemewa katika kupiga vita umaskini wa nchi hii?.

Tutawezaje kupiga hatua za kimaisha kama kila linalofanyika linaongozwa na siasa za majibizano, mikwaruzano?.

Maisha yote ni siasa, lakini kuna kipindi kinafika maisha hayo hayo yanatazamwa katika mtazamo wa kubadilisha hali mbaya ya kiuchumi ya watu.

Huwezi kuendelea kutegemea nguvu ya ujengaji hoja wakati nchi inayo changamoto ya ukuzaji wa sekta ya viwanda.

Hao wanaojinyima kwa ajili ya bajeti zetu ziweze angalau kuyafikia matarajio yetu, wanatutazama na kutudharau sana, pengine tunawakera pia, kwa sababu wao katika ule muda wanaofanya kazi sisi tunautumia katika mikutano na harakati za kukomoana kisiasa.

Ni kweli tunahitaji siasa kuanzia January mpaka Desemba?. Ni kweli hakuna miezi ambayo tunapaswa kupiga kazi ili maisha yetu yaweze kuboreka?.
 
Back
Top Bottom