Mashirika ya Uma yabane Matumizi

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
803
472
Tumeona serikali ya awamu ya tano chini mh. JPM ikijipambanua kama serikali inayobana matumizi, cha kushangaza mashirika ya umma yameshindwa kwenda na kasi ya awamu hii ya tano, kubana matumizi.

1. Wamekuwa na matangazo mengi kwenye vyombo vya habari, matangazo ambayo mara nyingi yamekuwa hayana tija, kumeingia tabia ya mashirika ya umma kununua muda wa matangazo ya nusu saa (30mins) kila week kwenye luninga TV huku wakiwa hawana content ya kutosha, mara zote vipindi vyako vinapwaya sana unajiuliza kwa nini basi wasinunue muda wa dakika kumi na tano (15mins) au chini ya hapo.

2. Mashirika yote ya serikali huwa yana kitengo cha habari, tena mengine yakiwa na wafanyakazi hadi kumi lakini cha kushangaza yamekuwa yanatoa mikataba kwa wanahabari/watangazaji binafsi ili kuandaa na kutangaza vipindi vyao.

Tunapoamua kubana matumizi kwa maslahi ya Taifa tusiwe na double standards.
 
Back
Top Bottom