Leo tarehe 7 Novemba 2025, sisi Mashirika ya Kiraia (CSOs) tuliosaini kwa pamoja taarifa hii, tunalaani kwa nguvu zote ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliojitokeza kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 nchini Tanzania. Ukiukwaji huu unahusisha mauaji ya raia wasio na hatia, ukamataji kiholela, utekaji, kupotezwa kwa watu, kukandamizwa kwa uhuru wa vyombo vya habari, kuzimwa kwa intaneti kwa siku sita, na kunyimwa haki za kisheria.
Kumekuwa na matumizi makubwa ya nguvu, ikiwemo risasi za moto na mabomu ya machozi kwa waandamanaji wasiokuwa na silaha, na vifo vya raia wasiohusika kabisa na maandamano. Familia na jamii zimeathirika sana, na baadhi ya watoto kushuhudia wazazi wao wakipigwa, kukamatwa au kuuawa.
Waandishi wa habari wameuawa na kujeruhiwa, wakiwemo: Master Tindwa (Clouds Media), aliyeuawa nyumbani kwake Temeke, Kelvin Lameck Mwakangondya (Baraka FM, Mbeya) – aliyeuawa akiwa kazini, Mwandishi wa Azam Media aliyejeruhiwa vibaya, Godfrey Thomas (Ayo TV) na Alphonce Kusaga wa (Sunrise Radio) na waliokamatwa Arusha. Pia Sheikh Msopa, kiongozi wa dini, alipigwa risasi na kuuawa nyumbani kwake Mabibo Mwisho, Dar es Salaam.
Zaidi ya hayo, mamia ya wananchi, hasa vijana, wamekamatwa na kushikiliwa bila dhamana katika vituo mbalimbali vya polisi kote nchini, kinyume cha Katiba na sheria. Kwa siku sita mfululizo tangu Oktoba 29, intaneti ilizimwa nchi nzima, na hivyo kuzuia upatikanaji wa taarifa, kufuatilia mchakato wa uchaguzi na kuripoti ukiukwaji wa haki za binadamu.
Tunatoa wito kwa Serikali ya Tanzania,
1. Kuwaachia wote waliokamatwa au kuwafikisha mahakamani mara moja.
2. Kuruhusu familia kupata na kuzikia wapendwa wao.
3. Kuruhusu uchunguzi huru na wa wazi kuhusu mauaji.
4. Kuwawajibisha waliohusika.
5. Kulinda uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari.
6 Kufanya maridhiano ya kitaifa na uponyaji wa muda mrefu.
7. Kutoa fidia kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.
Imesainiwa na: LHRC, Twaweza, FCS, JamiiAfrica, Msichana Initiative, Centre for Strategic Litigation, na Internet Governance Tanzania Working Group.