Mashine za TRA hazitumiki

Tanzania Mpya

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2012
Posts
252
Reaction score
145
TRA walianzisha ulipaji kodi kwa mfumo wa mashine. Lakini wafanya biashara wengi wanaiibia serikali kwa kukwepa kuzitumia mashine hizo. Binafsi nimeshuhudia ktk maduka, vituo vya mafuta ya gari, licha ya uwepo wa mashine hizo lkn wahazitumii. Kuna wakati mmoja mmoja sana wanazitumia kwa wateja wachache na kisha huziweka pembeni na kuendelea kupokea hela bila kukata risiti kutoka ktk mashine hizo.

Swali: hivi TRA wenyewe hawajui hili? Kwani wao si miongoni mwa wa-tz wanaopata huduma za mafuta na mahitaji mengine ktk madika ya hapa nchini? Mbona hatusikii watu wamekamatwa kwaa wizi huu? Fedha nyingi zinapotea...
 

Cash register hutumia umeme, vinginevyo kama wana zinazotumia beteri, hapo hoja inaeleweka kama zinatumia umeme, basi hakukuwa na umeme sasa tufanyeje?
 
Mbona kazi rahisi sana kukamata mwizi kama huyu,
Kwenye marejesho ya kodi si kuna sehemu inaonyesha mauzo? Na pia kule aliko nunua, huyo aliyemuuzia si anaonyesha kamuuzia kiasi gani. Ila na sisi raia hatuna tabia ya kudai risiti kwenye baadhi ya malipo ndio maana mianya hii haitaisha.
 
kuna siku nilidai risiti nikaambiwa kama wataka risiti ongeza elfu5, ni kweli kilikuwa kinauzwa bei rahis sana kile ktu pale dukani tofauti na sehemu nyingine sikuwa na ujanja, nikasepa tu bila risiti, na hii inawakuta watu wengi pindi pale wanapodai risiti.


 

Ndio tatizo la wafanya biashara wezi. Lakini km serikali ikiamua itaweza kukomesha tabia hii, na njia rahisi ni wao kujifanya wanunuzi na kuwakamata hawa. Wakishawaadhibu tu wengine wataogopa.
 
Ndio tatizo la wafanya biashara wezi. Lakini km serikali ikiamua itaweza kukomesha tabia hii, na njia rahisi ni wao kujifanya wanunuzi na kuwakamata hawa. Wakishawaadhibu tu wengine wataogopa.
mpaka rushwa iishe ndi tatizo litakwisha, hata yeye akijifanya mnunuzi si atapewa ktiu kidogo tu atanyamaza!
 
Ndio tatizo la wafanya biashara wezi. Lakini km serikali ikiamua itaweza kukomesha tabia hii, na njia rahisi ni wao kujifanya wanunuzi na kuwakamata hawa. Wakishawaadhibu tu wengine wataogopa.

Vigumu mno kwani po pote duniani wafanya biashara wanaiibia serikali mapato kwa mtindo huu. Njia pekee ambayo serikali hufanya ni kupima ukubwa wa biashara ilivyo na pato la kodi lisipofikia kiwango kile hawezi ku-renew leseni hake hadi pengo lile lilipwe.
 
Mimi nataka kuning'iniza Mhindi mmoja, kanipa risiti ya TRA iko tofauti na pesa niliyolipa. Wajanja wanatuandikia risiti ya safari na ile kwa ajili ya kumbukumbu za dukani! Kwa kweli serikali inaibiwa sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…