Mashine ya Kutengeneza maji yagunduliwa

SNAP J

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
7,117
Reaction score
8,096
Maji ni uhai. Naamini kila mmoja anakubaliana na usemi huo kwani bila maji hakuna kiumbe chochote kinachoweza kuishi. Tunapokuja kwa upande wa sisi binadamu, kusema tu maji ni uhai haitoshi, bali maji safi na salama ndio sahihi zaidi.

Ili kuthibitisha hili, Ripoti za Ummoja wa Mataifa (WHO) zinaonyesha yapata watu Milioni 780 duniani hawana access ya maji safi na salama, na kila mwaka watu milioni 3.4 hufariki kutokana na magonjwa yanasobabishwa na matumizi ya maji yasiyo safi na salama.

Katika kulitafutia ufumbuzi hili, kampuni ya Kiizraeli iitwayo Water- Gen imegundua mashine yenye uwezo wa kuzalisha maji kutoka katika hewa.

Namna ifanyavyo kazi

Mashine hiyo ya kustaajabisha ijulikanayo kwa jina la Atmospheric water-Generation unit inafanya kazi kwa kupooza hewa na kugandisha unyevu unyevu (water vapor) uliopo katika hewa.

Baada ya maji kupatikana, hupitishwa katika vichujio (filters) maalum ambazo zina uwezo wa kuondoa takataka za aina yoyote ile, zikiwemo kemikali na vijidudu vidogo kabisa (microorganisms).

Baada ya maji huyo kuchujwa, hufikia katika hata ya mwisho ambapo huifadhiwa katika matanki maalum,tayari kwa matumizi.

Hutumia nishati ndogo sana

Moja ya vitu vinavyoifanya mashine hiyo kuwa ya kipekee zaidi, na kuifanya Kampuni hiyo ya Water-Gen kuzipiku Kampuni zingine zilizojaribu kutengeneza aina ya mashine kama hii ni kuwa na uwezo wa kutumia nishati ndogo kabisa kwa kuweza kutumia hewa iliyopoozwa iliyozalishwa ndani ya Atmospheric water-Generator ambayo huweza kupooza hewa nyingine inayoingia ndani yake.

Kiasi cha maji yanayozalishwa

Kwa kutegemeana na kiwango cha nyuzi joto na kiasi cha unyevu unyevu (humidity) kilichopo katika hewa, Water-Gen generator mashine inauwezo wa kuzalisha Lita 250 hadi 880 ( sawa na Galoni 65 hadi 210 za maji) kwa siku.

Madhumuni ya ugunduzi wa mashine nini

"Hapo mwanzo, mashine hii ilitengenezwa maalum kwa ajili ya Israel Defense Force (IDF). Lakini Jamii kwa ujumla inaweza kunufaika na mashine hii". Anasema CEO wabkampuni ya Water-Gen, Arye Kohari.
-----------------------------------------------------------------------------------



Source:CNN Tel Aviv, Israel
 

Baadhi ya picha zikionyesha mashine hiyo na wanajeshi wa Israeli wakinywa maji yaliyopatikana kutoka ktk hewa
 

Attachments

  • 1398776787684.jpg
    9.8 KB · Views: 177
  • 1398777410747.jpg
    9.1 KB · Views: 525
  • 1398777423945.jpg
    10.3 KB · Views: 174
  • 1398777585289.jpg
    18.5 KB · Views: 161
Ndio maana ya kwenda shule. Utafiti na maendeleo haviachani. Bahati mbaya tafiti zetu hapa bongo ni za kisiasa tu. miaka 50 ya Uhuru watanzania tumegundua nini cha kuwainua wananchi? Tungeweza kuvuna wanyama pori tukahifadhi kwenye makopo! Tunaweza kutengeneza tiba za asili kwa kuprocess mizizi, magome na majani kisasa ili dawa ikae muda mrefu. na mengineyo mengi tu....tatizo uongozi bora hakuna!
 


Je wanazungumzia lolote juu ya negative side of it? kama vile kukausha mvua baada ya miaka kadhaa ikiwa mashine hizi zikizalishwa kwa wingi kupita kiasi? najaribu kurejea yaliyotokea Ihefu miaka ya 2007>>08,
 
Je wanazungumzia lolote juu ya negative side of it? kama vile kukausha mvua baada ya miaka kadhaa ikiwa mashine hizi zikizalishwa kwa wingi kupita kiasi? najaribu kurejea yaliyotokea Ihefu miaka ya 2007>>08,

Hapana,sijafahamu madhara yanayoweza kuletwa na over usage za mashine hii. Naendelea kulifuatila hili kwani ni jambo la msingi, then nitawajuza zaidi
 
Hao wanataka process ya water cycle ambayo ,rainfal(mvua) huundwa kwa process za Vaporisation,condensation and cooling isifanyika ipasavyo
 
Technology hiyo ya zamani mkuu wangu, nilipita Arusha mwaka 2010 nikaziona pale duka la BrazaAfric hizo water dispensers ambazo zinatengeneza maji ya kunywa kutokana na hewa, lakini zenyewe zina uwezo wa kutengeneza mpaka litres 36 kwa masaa 24 kutegemeana na hali ya humidity ya sehem iliyopo..kama sikosei zilikuwa zinauzwa Sh 2.5m ...tuliwakuta pale walikuwa wakifanya demonstration yake..
 

Sijaaema kuwa hiyo ni tech mpya,la,nimesema kuwa Water Gen company imeweza kugundua mashine ambayo ni more efficient na yenye uwezo kubwa wa kuzalisha maji,huku ikitumia nishati ndogo kabisa. Rejea kusoma tena hiyo habari.
 
Baadhi ya picha zikionyesha mashine hiyo na wanajeshi wa Israeli wakinywa maji yaliyopatikana kutoka ktk hewa

Kikwete and co juzi wana tuonesha ma boza ya maji yanayo tegemea kuchotwa mtoni ,,halafu wanatuambia wana vifaa wa kisasa ,,teh teh teh jk bwana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…