Mashine ya kukandia unga wa ngano

Mashine ya kukandia unga wa ngano

zelia

New Member
Joined
Dec 19, 2015
Posts
4
Reaction score
253
Habari za wakati huu? Leo nimekuja kwenu nikiwa mjasirimali mdogo wa kuuza maandazi baada ya kuanguka.

Nakumbuka niliomba mtaji kutoka kwenu na kuna baadhi walioonyesha moyo wa kunisaidia, nadhani waliingiwa na roho ya uoga baada ya nafsi zao kuwakataza. Nashukuru Mungu niliweza kupata mtaji niliokua najhitaji na nilianza kufanya biashara. Hakika inanilipa kiasi chake japo biashara bado ni changa ila inaonyesha matumaini.

Kama ilivyo kwenye kila biashara huwa changamoto hazikosekani. Kwenye biashara yangu changamoto pia zipo. Changamoto ninayoiona kuwa ni kubwa na inahitaji kutafutiwa ufumbuzi kwa haraka, ni hii ya kukanda unga wa ngano. Kwakweli imekua ikiniumiza sana maana kila siku lazima nikande unga wa ngano kilo tatu. Kama una roho nyepesi, unaweza ukachoka. Ila kwakua hii biashara imeonyesha kuwa na return nzuri, basi natafuta mashine ya kukandia ngano ya kilo 3 kwa sasa.

Nimejaribu kutafuta mitandaoni, lakini sioni majibu ya kujiridhisha. Sasa kwakua JF ina watu wa aina nyingi na ninafahamu kabisa katu ya watu hao wanaojishughurisha na haya mambo.

Kwahiyo ndugu zangu naomba kwa wenye ufahamu mnielekeze ni wapi nitapata mashine ya kukandia unga wa ngano kilo 3 na bei zao ziwe rafiki maana ndio kwanza naanza kusimama na hii biashara yangu.

Natanguliza shukrani zangu
 
Karibu .... Naagiza vyombo kutoka Zanzibar nauza kwa njia ya mitandao. Kuona Sampo za mixer za kukandia unga wa ngano karibu WhatsApp 0718828294 Namakha Kitchenware.

Luv
 
Habari za wakati huu? Leo nimekuja kwenu nikiwa mjasirimali mdogo wa kuuza maandazi baada ya kuanguka.

Nakumbuka niliomba mtaji kutoka kwenu na kuna baadhi walioonyesha moyo wa kunisaidia, nadhani waliingiwa na roho ya uoga baada ya nafsi zao kuwakataza. Nashukuru Mungu niliweza kupata mtaji niliokua najhitaji na nilianza kufanya biashara. Hakika inanilipa kiasi chake japo biashara bado ni changa ila inaonyesha matumaini.

Kama ilivyo kwenye kila biashara huwa changamoto hazikosekani. Kwenye biashara yangu changamoto pia zipo. Changamoto ninayoiona kuwa ni kubwa na inahitaji kutafutiwa ufumbuzi kwa haraka, ni hii ya kukanda unga wa ngano. Kwakweli imekua ikiniumiza sana maana kila siku lazima nikande unga wa ngano kilo tatu. Kama una roho nyepesi, unaweza ukachoka. Ila kwakua hii biashara imeonyesha kuwa na return nzuri, basi natafuta mashine ya kukandia ngano ya kilo 3 kwa sasa.

Nimejaribu kutafuta mitandaoni, lakini sioni majibu ya kujiridhisha. Sasa kwakua JF ina watu wa aina nyingi na ninafahamu kabisa katu ya watu hao wanaojishughurisha na haya mambo.

Kwahiyo ndugu zangu naomba kwa wenye ufahamu mnielekeze ni wapi nitapata mashine ya kukandia unga wa ngano kilo 3 na bei zao ziwe rafiki maana ndio kwanza naanza kusimama na hii biashara yangu.

Natanguliza shukrani zangu
Mashine ya nini sasa
 
Back
Top Bottom