Watanzania tunaongoza kwa kukatisha tamaa wanamichezo wetu. Nimepitia page za Wakenya naona wanawapongeza hata wale waliofanya vibaya, wanaamini kuna wakati watashinda.
Watanzania tunaombeana sana njaa, wengi habari ya Simbu kushindwa inawafurahisha kuliko mkisikia ameshinda. Taifa gani hili?
Naamini hakuna mchezaji anayepokea bendera ya Taifa aende kwenye mashindo makubwa kama hayo acheze chini ya kiwango. Hicho mnachoona ameonesha ndio uwezo wake wote.
Hamjawahi hata kusikia changamoto wanazopitia kuanzia maandalizi hadi ushiriki wao kwenye mashindano ila mnakuwa wa kwanza kuwakejeli wakishindwa.