Mashindano ya kisiasa na hatima ya Soka letu

Mashindano ya kisiasa na hatima ya Soka letu

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,356
Kutoka katika Mwananchi, Jumatatu 28 Julai 2014

Na Mphamvu Daniel
Mashindano ya soka ya Mbunge, kwa kimombo Mbunge Cup sio jambo geni machoni pa Watanzania wadau wa siasa na michezo. Mwezi jana yalimalizika yaliyoratibiwa na Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya huko mkoani Mara na yakapewa 'airtime' ya kutosha na vyombo vya habari.

Mwezi huu tunangoja kwa hamu (nawasemea washabiki) mashindano ya Jimbo la Sengerema ambayo yanadhaminiwa na mbunge wa huko, William Ngeleja na mengine ni yale yanayohusisha jimbo la Chalinze kwa mbunge Ridhiwani Kikwete.

Haya ni yale ambayo yanamulikwa sana na vyombo vya habari vya kitaifa, lakini kuna utitiri wa mashindano ya soka ambayo huratibiwa na madiwani na viongozi wa Serikali za Mtaa, wakati fulani Wilaya ya Kinondoni walishafika hatua ya kuandaa mashindano ya Meya, ambayo nadhani yaliandaliwa na ofisi ya Meya wa Manispaa.

Kwa kawaida mashindano haya hutumia fedha nyingi ambazo hutoka kwenye mfuko wa kiongozi husika wa kisiasa, achilia mbali uwezekano wa viongozi hawa kuomba misaada kwa makampuni, watu binafsi au mifuko ya jamii kwa jina la michezo.

Walakini unakuja endapo hawa kweli wana malengo ya kukuza michezo wanaporatibu mashindano haya. Ni nadra kwa mwanasiasa yeyote kutoa pesa zake bila kuwa na uhakika wa kunufaika kisiasa. Si ajabu kuona uzinduzi na sherehe za kufunga mashindano haya zikitawaliwa na wingi wa waandishi wa habari ambao wamelipwa fedha ili kuyatangaza mashindano haya.

Sherehe za ufunguaji wa Bulaya Cup mwaka huu zilitawaliwa na hotuba zenye kila dalili ya siasa. Maneno ya kunadi chama tawala na kuponda wapinzani yalitawala, kinyume na utamaduni wa michezo ambao ni kujenga umoja na mshikamano na miongoni mwa wanamichezo na washabiki.

Siasa haijaanza tu na mashindano haya. Wanasiasa hujipenyeza katika michezo katika kila ngazi ili kutengeneza majina. Timu za taifa hukumbatiwa na wanasiasa pale ambapo kuna dalili ya kufanikiwa katika mashindano, lakini si wakati zinawahitaji.

Mbunge wa Singida Mjini alipita Simba kipindi fulani, akajenga jina kisiasa na akawa mbunge baadaye. Ajabu ni kuwa aliponunua timu ya Mbagala Market na kuibadili kuwa African Lyon ikamshinda miaka michache tu baada ya kuinunua. Inashangaza 'eti' mtu aliyeipatia mafanikio Simba timu ambayo ni mali yake mwenyewe imshinde.

Ndio, hawa ni wanasiasa na huenda kwenye mchezo ambao una wapenzi wengi na utakuza jina lao. Ni mara chache kusikia wanasiasa wamechangia mchezo mwingine zaidi ya soka kwa kuwa huko hakuna maslahi sana kwa mustakabali wao wa kisiasa.

Sifahamu kiasi cha fedha wanachotumia kudhamini mashindano haya lakini si haba. Fedha hizi hugharamia zawadi kwa washiriki, gharama za maandalizi, kulipa wasimamizi na kutangaza mashindano.

Namna mashindano haya yanavyoenda sio kwa kukuza vipaji. Huchochea ushindani kwa ahadi ya zawadi, timu hukodi wachezaji kutoka mbali na wakati mwingine hutumia wachezaji wa ligi kuu. Rejea sakata la wachezaji wa Yanga na Azam kuadhibiwa msimu uliopita kwa tuhuma za kucheza mechi nje ya timu, maarufu kama 'ndondo'.

Wachezaji chipukizi na wenyeji hawana nafasi kabisa katika mashindano haya na uwezejkano wa kung'aa ni mdogo kwa kuwa ushindani unaotengenezwa na wachezaji wa nje ni mkubwa sana.

Mathalani, mshindi wa Mashindano ya Meya wa Manispaa ya Mbeya mwaka jana aliondoka na bajaj yenye thamani ya sh. Milioni 4 na fedha taslimu sh. Milioni moja. Achilia mbali zawadi kwa washindi wengine na gharama za jumla za kuandaa mashindano ambazo zilibebwa na kampuni ya Pepsi tawi la Mbeya.

Ni wazi kuwa fedha hizi haziwezi kusaidia chochote katika maendeleo ya timu. Katika mazingira ambayo jiji la mbeya lina uwanja mmoja, tena usiokidhi viwango, ofisi ya meya inafanya mchakato wa kuandaa mashindano ya aina hii.

Fedha ambazo zinatumika kugharamia mashindano haya, zingeweza kutumika kama msingi wa kuweka miundombinu ya soka kama vile kituo cha mafunzo au upandaji wa nyasi katika viwanja vya mtaani. Badala yake wanasiasa wamelenga kupeleka ambako kuna manufaa kwao na sio kwa jamii.

Upandaji nyasi bandia huweza kugharimu kama milioni mia moja hivi. Maana hapa ni kuwa kwa gharama ya shilingi milioni kumi inaweza kutosha kuanza mchakato wa upandaji nyasi bandia katika uwanja mmojawapo kitongojini, au walau kusaka mdhamini wa kufanya hivi.

Ofisi ya mbunge au diwani kwanini isitumie fungu walilo nalo kuanza mchakato kama huu. Mbunge au diwani ambae anadhamini mashindano ambayo anajua yatapewa jina lake hawezi kufikiria kufanya kitu kama hiki kwa maendeleo ya soka.

Maeneo bunge na kata wanazotoka wabunge na madiwani hawa zipo timu za soka tayari, au hata vituo vya watoto lakini wanajifanya wapofu hawavioni na ni kama hawajui kama vinahitaji sapoti kutoka kwao.
Timu ya soka ya Championi ya Mikocheni A mwaka jana ilifuzu kucheza ligi daraja la nne mkoa wa Kinondoni, si mbunge wala diwani wao aliyejitokeza kuwapiga chapuo katika kampeni zao za kupanda daraja, matokeo yake wakatlewa katika hatua hizo.

Diwani huyu huyu ambaye pia ni meya wa Manispaa ya Kinondoni anathubutu kufuata mkumbo ule ule kwa kuanzisha Kombe la Diwani kwa jina lake Mwaka ujao kwenye kampeni atapanda jukwaani na kusema kjuwa yeye na chama chake wanapenda michezo.

Ni mapema sana kusema kuwa uwezo wa wanasiasa kufikiri lakini uelekeo ni huo. Upo uwezekano wa wao kufanya ammbo yenye manufaa katika michezo na bado wakayatumia kujijenga kisisasa lakini wao wameamua kufungamana na mbinu zile zile za miaka ya tisini.

Watanzania si wazembe tena, wanajua kuchambua mbivu na mbichi na wanaona endapo hii ni hatua ya kweli au ya kisiasa.
 
Tumeshindwa Kila kitu.

Hatuna viongozi ila tuna watawala
 
Mphamvu kwa kiwango fulani ninaomba nitofautiane na huyu mwandishi.Ili mpira uendelee unahitaji vitu vinne vipaji,maeneo ya kuchezea,makocha na vifaa.Hili la nne,vifaa,ni pengo kubwa linalozibwa na madiwani na wabunge.Inawezekana wakaanzisha mashindano haya kwa sababu binafsi/za kisiasa,lakini mwisho wa siku wanatusaidia kusambaza vifaa vya michezo kona zote za Tanzania hususani mipira na jezi,huu mchango tusiubeze ni mkubwa sana.Ndio maana ninapoona diwani/ mbunge/mwananchi anazuiwa asifanye mphamvu cup nakuwa sipendezewi,tunachotaka sisi mpira uchezwe nchi nzima.
 
Last edited by a moderator:
Mphamvu kwa kiwango fulani ninaomba nitofautiane na huyu mwandishi.Ili mpira uendelee unahitaji vitu vinne vipaji,maeneo ya kuchezea,makocha na vifaa.Hili la nne,vifaa,ni pengo kubwa linalozibwa na madiwani na wabunge.Inawezekana wakaanzisha mashindano haya kwa sababu binafsi/za kisiasa,lakini mwisho wa siku wanatusaidia kusambaza vifaa vya michezo kona zote za Tanzania hususani mipira na jezi,huu mchango tusiubeze ni mkubwa aana.Ndio maana ninapoona diwani/ mbunge/mwananchi anazuiwa asifanye mphamvu cup nakuwa sipendezewi,tunachotaka sisi mpira uchezwe nchi nzima.

Kama lengo Lao ni kutoa vifaa vya michezoan sasa Tangu hapo walipoanza kutoa hivyo vifaa hadi leo wamesaidia nini katika maendeleo ya michezo Tanzania kiujumla? We unajibu kisiasa siasa tuan sisi ni wakushindwa tu kila kona na kuandaa luuundo la visingizio
 
Last edited by a moderator:
Mphamvu kwa kiwango fulani ninaomba nitofautiane na huyu mwandishi.Ili mpira uendelee unahitaji vitu vinne vipaji,maeneo ya kuchezea,makocha na vifaa.Hili la nne,vifaa,ni pengo kubwa linalozibwa na madiwani na wabunge.Inawezekana wakaanzisha mashindano haya kwa sababu binafsi/za kisiasa,lakini mwisho wa siku wanatusaidia kusambaza vifaa vya michezo kona zote za Tanzania hususani mipira na jezi,huu mchango tusiubeze ni mkubwa sana.Ndio maana ninapoona diwani/ mbunge/mwananchi anazuiwa asifanye mphamvu cup nakuwa sipendezewi,tunachotaka sisi mpira uchezwe nchi nzima.

Jamal Malinzi, bahati nzuri mwandikaji ni mimi mwenyewe.

Ninacholenga mimi sio vifaa peke yake. Nimejaribu kupima thamani ya wanacholeta kwanye jamii vs wanachochota (manufaa ya kisiasa). Mpira sio bidhaa 'cheap' kiasi hicho hata mtu aende bungeni kwa mgongo wa jezi na vimilioni kadhaa alivyotoa kwenye Whosoever Cup.

Hawa watu (wanasiasa) wanao ushawishi mkubwa na wanaweza kuutumia kwa nia nzuri na soka bila kuumia chochote. Ni mapema kuwashukuru kwa jezi na bibs wakati hizo zimewapa makubwa kutoka kwetu.

Mwisho tujiulize baada ya kutoa hivyo vifaa mwendelezo ni upi, jezi na bukta moja vitamfaa nini mchezaji kwa kipindi cha miaka mitano ambayo mbunge na diwani wanakula kodi ya wajinga?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom