PostGE2025 Masheikh wa BAKWATA acheni kupotosha, kudai haki sio kuvunja amani

PostGE2025 Masheikh wa BAKWATA acheni kupotosha, kudai haki sio kuvunja amani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,240
Reaction score
90,297
Masheikh wa BAKWATA wamekomalia propaganda ya kwamba raia wakidai au kuzitka haki za msingi za kijami wakati huu ni kuvunja amani amani ya nchi. Huu ni uongo mtupu, propaganda chafu na ubinafsi. Watu wanaodai haki sio wavuruga amani wa nchi bali ni watu wanaotaka nchi bora na yenye usawa kuliko tuliyo nayo sasa.

Wapigania haki au wanaozidai haki wanataka;

1. Wafanyabiashara wafanye biashara zao na kufanikiwa bila kulazimika kujikomba na kuwa chawa kwa CCM. Wasilazimike kuchangia shughuli za CCM au za mwenge au kutundika picha za Samia katika biashara zao ila kupata unafuu wa kibiashara.

2. Wafanyakazi wa umma wafanye shughuli zao kwa bila mashinikizo ya CCM

3. Raia wachague viongozi wao kwa uhuru na haki, kura zihesabiwe na ziwe na maana

4. Ufisadi, Rushwa na upendeleo serikalini vikomeshwe.

5. Rasilimali za umma zisiuzwe kiholela au kutolewa kwa mikataba ya hovyo

6. Wakosoaji na wapinzani walale majumbani mwao bila hofu ya kutekwa, kupotezwa , kuuwawa au kufunguliwa kesi za mchongo.

7. Ajira nzuri na unafuu wa maisha

Ni yapi kati ya madai haya ni kuvunja amani au kinyume cha uislamu wa BAKWATA??
 
Masheikh wa BAKWATA wamekomalia propaganda ya kwamba raia wadai haki za msingi za kijami ni wavunja amani. Huu ni uongo mtupu, propaganda chafu na ubinafsi. Watu wanaodai haki sio wavuruga amani wa nchi bali ni watu wanaotaka nchi bora na yenye usawa kuliko tuliyo nayo sasa.
Wapigania haki wanataka;

1. Wafanyabiashara wafanye biashara zao na kufanikiwa bila kulazimika kujikomba na kuwa chawa kwa CCM. Wasilazimike kuchangia shughuli za CCM au za mwenge au kutundika picha za Samia katika biashara zao ila kupata unafuu wa kibiashara.

2. Wafanyakazi wa umma wafanye shughuli zao kwa bila mashinikizo ya CCM

3. Raia wachague viongozi wao kwa uhuru na haki, kura zihesabiwe na ziwe na maana

4. Ufisadi, Rushwa na upendeleo vikomeshwe

5. Rasilimali za umma zisiuzwe kiholela au kutolewa kwa mikataba ya hovyo

6. Wakosoaji na wapinzani walale majumbani mwao bila hofu ya kutekwa, kupotezwa , kuuwawa au kufunguliwa kesi za mchongo.

Ni yapi kati ya madai haya ni kuvunja amani au kinyume cha uislamu wa BAKWATA??
Trying to reason with these mazafakas may be just a waste of time. Their integrity is completely compromised!
 
Ni pesa zinatembea wameshashikishwa mabilioni, kuua hawaoni ishu tena yote kulinda matumbo yao.
Nyerere alisema maadui wetu ni ujinga, maradhi na umaskini ni kweli kwa sababu rushwa inatumia udhaifu wa umasikini kutukandamiza. Sema tuweke sheria kama ya China ile kuhusu rushwa tofauti na hapo hatutoboi miaka 1000.
 
Back
Top Bottom