Mashairi ya Nyoko.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
NYOKO.

1.Ukweli napo usema,mwenzenu sina nyimivu
Maneno napo yatema,vyema uwe msikivu
Cheche zikianza hema,kuni huzaa majivu
Nakiri Nyoko ni shibe,ni shibe ya kuonana.

2.Ukiona wapo pamwe,jua wameficha kovu
Ila nakwambia kamwe,waliyapita maovu
Kushikana kutazamwe,hakuzai yao bovu
Nakiri Nyoko ni shibe,ni shibe ya kuonana.

3.Mwana akiita nina,mama humbusu shavu
Ukitazama kwa kuna,jodari hutega nyavu
Wanywanywa wakilumbana,mzuka hupandwa ndovu
Nakiri Nyoko ni shibe,ni shibe ya kuonana.

4.Walio tazama ruya,wakiri kweli pakavu
Mchuzi wameutiya,wapate macho angavu
Maoni Hadi kuliya,huo ni ubongo pevu
Nakiri Nyoko ni shibe,ni shibe ya kuonana.

SHAIRI-NYOKO.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Mkuu kwa makabila mengine Nyoko ni tusi, uwe unafanya research plz
Nawe pia ungefanya utafiti kabla ya Ku comment ili uelewe shairi niliandika ni la kikabila au la kiswahili.
Piki Piki ungefanya utafiti ugundue neno NYOKO Lina maana yani.
Tatu,nakushauri yfanye utafiti uone ni maneno mangapi ya kiswahili ambayo ni matusi katika lugha by in fine.
Pia,karibu sana hapa JUKWAA LA LUGHA.
 
Kwa kibantu NYOKO ni mama.
 
Back
Top Bottom