Mashabiki watano wa yanga wamwagwa manoti kwa Toto Africa

makalango

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
448
252
Katika hali isiyo ya kawaida mashabiki wa yanga ambao wako watano kwa pamoja wameamua kuingilia mchezo wa toto Africa dhidi ya simba utakaofanyika Leo pale uwanja wa ccm kirumba, mashabiki hao wametoa sh million 30 ili toto waifunge simba na endapo watatoa sare basi wachezaji hao watapewa sh.ml 20
Chanzo :muungwana blogu Leo.
 
Simba mmeanza kuweweseka...tulieni muipate dozi...msiwe na kiholo,bado masaa machache tu... mnatafuta ground za kujitetea mkipigwa...hahaa!!!
 
Haya mambogamboga FC yanatoa hela kwa toto huku kuna wachezaj wao wanadai malimbikizo ya mishahara kwa miez mitatu. Bora hiyo million 30 yangeenda kuondoa mafuriko kwenye uwanja wao jangwani
 
Kwanini wasimlipe chirwa kwanza ambaye amegoma kwenda Algeria. Bashte kweli ni wengi
 
Siyo hivyo pia naskia mwesigwa na malinzi wamezindua kampeni ya kurudisha pointi za kagera hicho kikao kitafanyika pale posta tarehe 18/04/2017 kwa sababu yeye hakuwepo na lengo likiwa moja tu la kurudisha pointi za kagera Kwa kuwa mwesigwa alikuwa yanga pia malinzi yanga zitarudishwa msijali
Chanzo:salehe jembe kila kitu kimeandikwa huko
 
Kwahiyo wazee wa mchangani ndio mmeanza kujijengea mazingira ili mkifungwa iwe 'mlilijua' hilo mapema?
Chezeni mpira nyie,na leo ni aidha mfungwe au mtoke sare...
Viva Toto Africans
 
Katika hali isiyo ya kawaida mashabiki wa yanga ambao wako watano kwa pamoja wameamua kuingilia mchezo wa toto Africa dhidi ya simba utakaofanyika Leo pale uwanja wa ccm kirumba, mashabiki hao wametoa sh million 30 ili toto waifunge simba na endapo watatoa sare basi wachezaji hao watapewa sh.ml 20
Chanzo :muungwana blogu Leo.
Hiyo ni rushwa kama rushwa nyingine. kwenye nchi ambazo rushwa haikubaliki na ambako pia mchezo wa soka unaheshimiwa tendo kama hilo linatosha kumpeleka mtu jela na kuishusha timu ambayo imefaidika na rushwa hiyo. wanabahati kwakuwa tupo Tanzania, ila muwaambie waende wakaulize kilichompata aliyekuwa katibu mkuu wa yanga Issa Makongoro.
 
Kwahiyo wazee wa mchangani ndio mmeanza kujijengea mazingira ili mkifungwa iwe 'mlilijua' hilo mapema?
Chezeni mpira nyie,na leo ni aidha mfungwe au mtoke sare...
Viva Toto Africans
Upo nifar? Sijakuona hapa tangia ile mechi ya mbao
 
Hiyo ni rushwa kama rushwa nyingine. kwenye nchi ambazo rushwa haikubaliki na ambako pia mchezo wa soka unaheshimiwa tendo kama hilo linatosha kumpeleka mtu jela na kuishusha timu ambayo imefaidika na rushwa hiyo. wanabahati kwakuwa tupo Tanzania, ila muwaambie waende wakaulize kilichompata aliyekuwa katibu mkuu wa yanga Issa Makongoro.
Mkuu naskia rais wao kaja na kazindua kampeni ya rejesha pointi kagera hii nchi ya ajabu kweli mwesigwa na malinzi wanataka kurudisha pointi kwa shinikizo la yanga Kwa vile walikuwa viongozi wa yanga mhhhhh kazi sana
 
Back
Top Bottom