utaratibu haujaanza TFF
wanasema system ya uwanja wa taifa na system ya machine za CRDB
haziendani kwaiyo bado unatafuta suluhisho
Hivi utaratibu wa kukata tiketi kwa mashine umeanza,si nilisikia round ya 4
Tangu TFF ianze utaratibu wa kutangaza mapato uwanja wa taifa, mechi za simba zimekuwa zikiingiza fedha kidogo kulinganisha na Yanga, hata ukiudhuria mechi za simba utaona watu si wengi sana kama mechi za yanga.
Msimu uliopita watu waliokuwa wanaudhuria mechi za Simba uwanja wa taifa walikuwa wachache tukasema kutokana na mwenendo wa timu kufanya vibaya, sasa msimu huu tatizo liko wapi? Wakati timu inafanya vizuri? Pamoja na timu kusaini mikataba ya udhamini na TBL na Azam Tv lakini bado mapato ya mlangoni yataendelea kuwa chanzo kikuu cha fedha, kwaiyo wanasimba wenzangu naomba tuwe tunaudhuria kwa wingi uwanja wa taifa kuisapoti timu na kutunisha mfuko pia.
SIMBA NGUVU MOJA
Mkuu kama umefuatilia vizuri utagundua kwamba asilimia kubwa ya washabiki wa Simba hawachagui mechi, lakini wale wa upande wa pili wanachagua mechi na mara nyingi mechi za Simba na timu nyingine hawaendi wengi lakini kwa wale wa Simba hata kama ni mechi za Yanga na timu nyingine wanaenda wengi hivyo kufanya mechi za Yanga kuwa na watu wengi kwa sababu mashabiki wa pande zote mbili wanakuwa wengi kuliko zile mechi za Simba maana mashabiki wa Yanga wanakuwa wachache sana.
Duh.!!
kwa hiyo mashabiki wa msimbazi wanajaa kwenye mechi zisizo zao, lakini kwenye mechi yao hawaendi hapa kunatatizo.
Labda ungesema timu yao haina mvuto na morali wa ushindi.!!
Mkuu ni vigumu kukuamini kuwa mechi za Simba zinakosa mapato sababu mashabiki wa Yanga wanaoingia ni wachache.Hujanielewa, ni kwamba kwa sababu mashabiki wengi wa Simba hawachagui mechi na inapokuwa mechi ya Yanga na timu zingine wanaingia wengi na kwa sababu mashabiki wa Yanga wengi huingia mechi za Yanga tu hivyo idadi ya walioingia inakuwa ni kubwa ukilinganisha na mechi ya Simba ambayo itakuwa na mashabiki wa Simba wengi na wachache wa Yanga ambao hawachagui mechi.
Kama unajua hesabu ngoja nikuwekee kihesabu pengine utanielewa. mfano mashabiki wa simba ni 1000, na wa Yanga ni 1050(under assumption kwamba wote wataingia uwanjani kwenye mechi zinazowahusu), lakini wa simba wasiochagua mechi ni 700(wanaingia mechi yoyote) na wa yanga wasiochagua mechi ni 200(wanaingia mechi yoyote), mechi ya Yanga ikichezwa itakuwa na watazamaji 1050+700=1750 lakini ya Simba ikichezwa itakuwa na watazamaji 1000+200=1200. umenielewa sasa?
Tangu TFF ianze utaratibu wa kutangaza mapato uwanja wa taifa, mechi za simba zimekuwa zikiingiza fedha kidogo kulinganisha na Yanga, hata ukiudhuria mechi za simba utaona watu si wengi sana kama mechi za yanga.
Msimu uliopita watu waliokuwa wanaudhuria mechi za Simba uwanja wa taifa walikuwa wachache tukasema kutokana na mwenendo wa timu kufanya vibaya, sasa msimu huu tatizo liko wapi?
Mkuu ni vigumu kukuamini kuwa mechi za Simba zinakosa mapato sababu mashabiki wa Yanga wanaoingia ni wachache.
Na mechi za Yanga zinamapato makubwa sababu mashabiki wa Simba wanaingia kwa wingi.
Unahitimisha hoja kuwa mashabiki wa Simba ndio wanaojaaa Zaidi uwanjani na hawachagui mechi.
lakini huonyeshi chanzo cha taarifa yako.!
Msome mleta mada hapa yeye halaumu mashabiki wa timu pinzani kuwa ndio chanzo bali anawahamasisha wanasimba kwenda uwanjani, kwa hayo maelezo tatizo lipo na wanasimba wenyewe.
Mkuu sababu nimeshataja hapo juu, kama tungeweza kuhesabu watu waliokaa kushoto na wale wa kulia ungekubaliana na mimi ninachosema.