Mashabiki wa simba dar ni wanafiki

Mashabiki wa simba dar ni wanafiki

Kama rage anang'ang'ania uongozi sasa atashirikiana na nani wakati kamati nzima ya utendaji haipo tayari kufanyakazi nae tena?
 
wadau nikiangalia mwenendo wa uongozi uliopo na vurugu zinazotokea katika club yetu naweza sema kuna unafiki mkubwa na ulafi wa madaraka unaoendelea katika club yetu ya simba

Iweje aden rage huyu huyu ambaye ameonekana ana utendaji mbovu apokelewe na watu wale wale ambao kutwa kucha wanashinda vijiweni wakimlaani kama si kiongozi bora? Au nguvu ya VIROBA IMETUMIKA?

Tukiangalia mwenendo wa timu katika mzunguko wa kwanza timu yetu ilikua ipo kati na kati iweje mashabiki hawa wafanye vurugu wakimaanisha hawa rhdhishwi na uongozi wa timu?
Rage huyu alitufanyia maigizo katika suala la uwanja wa timu kiasi mpaka leo halipo tena katika utekelezwaji
rage huyu huyu amekua na siasa nyingi mdomoni kuliko vitendo ana longolongo nyingi lakini kuna baadhi yatu hatutaki maamuzi magumu WHY?
Utashangaa hiyo tarehe moja mashabikI hawa hawa wa dar wanapiga chereko na vifijo kukubaliana na huyu MWANASIASA
KAMA MNAENDESHWA NA NGUVU ZA VIROBA NYIE WATU WA DAR TAFADHALI SIKU YA MKUTANO MKUU MSINYWE MUDA WA KUIFANYA SIMBA ITULIE NI ATOKE MTU HAPA!

ACHENI UOGA WA KITOTO

Hao ni wanunuliwa wa muheshimiwa, kumbuka ni mwanasiasa yule na hashindwi kutumia pesa kwa maslahi yake.
 
habari moja imeripoti kuwa washabiki waliofika ni wachache 120 walifika na magoli 3 ya kukodi na wengi walionekana sio wanachama wa simba mwingine anaripoti waliofika ni 200 na magari sita ya kukodi nafikiri utakuwa unawaonea mashabiki wa simba kwani waliokuja wengi wameletwa na njaa zao na sio simba kama unavyofikiri ushahidi wa washabiki wengi wa simba hawampendi rage ni kupungua mahudhurio ya watazamaji katika mechi za simba lakini umewasahau na waandishi wanafiki ambao kwa njaa zao wanatumia kalamu zao kuonyesha rage bado anakubalika
 
Wanaomlaani na waliokwenda kumpokea ni tofauti sio walewale.mashabiki simba wako wengi sana
 
...Rage sijui ana nini ndani ya Club; sawa atakama utaratibu wa kumsimamisha haukufuata Katiba ya Club...lakini kwa jinsi hali ilivyo na mwenendo mzima wa Timu jinsi ulivyo kwasasa, inabidi ifike hatua ya kusema sasa RAGE basi; haiwezekani aendelee kugonganisha vichwa watu alafu akafumbiwa macho. Inabidi yeye binafsi atambue kuwa hapendwi tena kuendelea kuwa mwenyekiti wa Club; na kama ni kweli Rage anaitakia mema SIMBA hanabudi kuachia ngazi.
 
...Rage sijui ana nini ndani ya Club; sawa ataka utaratibu wa kumsimamisha haukufuata Katiba ya Club...lakini kwa jinsi hali ilivyo na mwenendo mzima wa Timu jinsi ulivyo kwasasa, inabidi ifike hatua ya kusema sasa RAGE basi; haiwezekani aendelee kugonganisha vichwa watu alafu akafumbiwa macho. Inabidi yeye binafsi atambue kuwa hapendwi tena kuendelea kuwa mwenyekiti wa Club; na kweli Rage anaitakia mema SIMBA hanabudi kuachia ngazi.

Hivi unajua maana ya GAMBA wewe?Halina mshipa wowote wa aibu wala halipitishi damu na kwa hiyo lipo lipo tu.Bila kung'olewa litaendelea kukomaa hapo hapo.Jamaa anapenda uswahili swahili sana na unaweza kuona waswahili wenzake walivyompokea!watu wa maneno maneno mengi bila vitendo

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
umefika wakati wa kuzia haya yanayotokea sasa

Ni vigumu, tawi la Mpira Pesa walijaribu kupimana ubavu na mheshimiwa, nadhani unakumbuka kilichowakuta. Washabiki wanaweza kususa kwenda uwanjani kabisa kuonesha kukerwa kwao na haya, maaana hata mkikaza kihivi itatokea mipumbavu michache kama hiyo iliyoenda uwanjani jana kumpokea mwenyekiti wao.
 
watanzania wengi unafiki ndio maisha yao ya kila siku. iwe kwenye michezo au siasa. watalalama weeeee mwisho wa siku wanakichagua tena kwa kishindo chama cha kijani na njano, hili sakata la rage linathibitisha
 
Back
Top Bottom