Mashabiki wa simba dar ni wanafiki

Mashabiki wa simba dar ni wanafiki

scatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
1,671
Reaction score
940
wadau nikiangalia mwenendo wa uongozi uliopo na vurugu zinazotokea katika club yetu naweza sema kuna unafiki mkubwa na ulafi wa madaraka unaoendelea katika club yetu ya simba

Iweje aden rage huyu huyu ambaye ameonekana ana utendaji mbovu apokelewe na watu wale wale ambao kutwa kucha wanashinda vijiweni wakimlaani kama si kiongozi bora? Au nguvu ya VIROBA IMETUMIKA?

Tukiangalia mwenendo wa timu katika mzunguko wa kwanza timu yetu ilikua ipo kati na kati iweje mashabiki hawa wafanye vurugu wakimaanisha hawa rhdhishwi na uongozi wa timu?
Rage huyu alitufanyia maigizo katika suala la uwanja wa timu kiasi mpaka leo halipo tena katika utekelezwaji
rage huyu huyu amekua na siasa nyingi mdomoni kuliko vitendo ana longolongo nyingi lakini kuna baadhi yatu hatutaki maamuzi magumu WHY?
Utashangaa hiyo tarehe moja mashabikI hawa hawa wa dar wanapiga chereko na vifijo kukubaliana na huyu MWANASIASA
KAMA MNAENDESHWA NA NGUVU ZA VIROBA NYIE WATU WA DAR TAFADHALI SIKU YA MKUTANO MKUU MSINYWE MUDA WA KUIFANYA SIMBA ITULIE NI ATOKE MTU HAPA!

ACHENI UOGA WA KITOTO
 
Umemaliza mkuu,nahisi kuna pesa imetumika kuwavalisha watu jezi za simba,in short hao si mashabiki wa simba,wengi wamepewa pesa na jezi,usishangae ujafanyika ujanja siku ya mkutano mkuu wakingizwa na kupindisha maamuzi ili huyo boya aendelee kubaki.
 


Mwenyekiti wa Simba aliyesimamishwa, Ismail Aden Rage amerejea nchini na kuahidi kumwaga ugali kwa kuwa waliomsimamisha wamemwaga mboga.

Rage amerejea nchini Saa 1 na ushee usiku akitokea nchini Sudan na kusisitiza kwamba atazungumza kesho saa saba mchana kwenye makao makuu ya klabu hiyo.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MASHABIKI WACHACHE WALIOJITOKEZA KUMPOKEA[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Rage alipokelewa na mashabiki wapatao 120 waliokuwa katika mabasi matatu ya kukodi, ambao walikuwa wakiimba nyimbo za kuonyesha wamekwenda kumpokea.
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Hata hivyo ilionekana wazi mashabiki hao wengi hawakuwa wanachama wa Simba, na idadi yao haikuwa kubwa kama ambavyo ilitarajiwa awali.


Baada ya kutoka alizungumza na waandishi wa habari halafu akaingia kwenye gari aina ya Toyota na kuondoka zake hadi klabu ambako alitoa ahadi hiyo ya kumwaga ugali kesho.


Rage alisimamishwa kwa madai ya kutoshirikiana na viongozi wenzake ikiwemo kamati ya utendaji na maamuzi ya mambo mengi alikuwa akifanya mwenyewe.


Pamoja na hivyo suala la kumuuza mshambuliaji Emmanuel Okwi kwa Etoile du Sahel ya Tunisia, hadi leo Simba inadai dola 300,000 na haijalipwa kitu.


Lakini aliingia mkataba na Azam TV ili Simba TV iwe inaonyeshwa na kulipwa Sh milioni 330 kwa miaka mitatu ikiwa na maana kila mwaka Simba itapata Sh milioni 110, wakati kampuni ya Zuku ilikuwa tayari kutoa dola 300,000 kwa mwaka na walikuwa bado kwenye mazungumzo.
 
angalia vizuri kichwa, yaani kila mshabiki wa simba dar ni mnafiki?
 
baadhi ya mashabiki wa simba.....................tena naongeza wazandiki
 
ukimuudhi mfuga mbwa...................tukimkorofisha Hans Pope tumekwisha
 
Na Mahmoud Zubeiry, JNIA
MWENYEKITI wa Simba SC, Ahaj Ismail Aden Rage amewasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam usiku huu akitokea Sudan na kusema kwamba; "Mimi bado Mwenyekiti wa Simba SC,".
Rage aliwasili kwa ndege ya shirika la Kenya saa 1:40 usiku na kutokea mlango wa Watu maalum (VIP) ambako alilakiwa na wanachama zaidi ya 200, waliokuwa kwenye mabasi sita aina ya Coaster.
"Umati huu uliokuja hapa ni kielelezo tosha sana kwamba kiasi gani wanachama wa Simba wana imani na Mwenyekiti wao, sasa leo sitasema mengi, nitakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari kesho saa saba mchana makao makuu ya klabu(Msimbazi),"alisema Rage.[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Rage akiinua mikono juu kishujaa wakati anatoka Uwanja wa Julius Nyerere, Dar es Salaam usiku wa leo[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Alipoulizwa kuhusu kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Jumatatu na kutangaza kumsimamisha, Rage alisema; "Kwa mujibu wa Katiba ya Simba, Kamati ya Utendaji haina uwezo wa kumsimamisha Mwenyekiti, usinimalizie utamu Zubeiry, njoo kesho mchana Msimbazi,"alisema.
Watu zaidi ya 200 walifika Uwanja wa ndege tangu saa 11 na ushei jioni ya leo kumsubiri Rage wakiimba nyimbo mbalimbali za kumbeza Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang'are ‘Kinesi' na kumpamba Rage huku wakicheza ngoma.
Na alipowasili walimlaki kwa shangwe na kucheza naye. Ilikuwa bonge la picha na waliofika kumlaki Rage walikuwa watu wa rika na jinsia tofauti, hadi wazee.
Rage baada ya kuzungumza kwa kifupi na Waandishi wa Habari alisema anaelekea makao makuu ya klabu, ambako wanachama wengine walikuwa huko wanamsubiri.
Jumanne wiki hii, Kinesi alisema, Kamati ya Utendaji ilimsimamisha Rage katika kikao chake cha Jumatatu usiku kwa sababu anaendesha klabu kwa kufanya maamuzi yake mwenyewe bila kushirikisha kamati ikiwemo kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji kwa mujibu wa Ibara ya 31 (a).
 
2.jpg
 
Woga ni sumu ya maendeleo-lema
wadau nikiangalia mwenendo wa uongozi uliopo na vurugu zinazotokea katika club yetu naweza sema kuna unafiki mkubwa na ulafi wa madaraka unaoendelea katika club yetu ya simba

iweje aden rage huyu huyu ambaye ameonekana ana utendaji mbovu apokelewe na watu wale wale ambao kutwa kucha wanashinda vijiweni wakimlaani kama si kiongozi bora? Au nguvu ya viroba imetumika?

Tukiangalia mwenendo wa timu katika mzunguko wa kwanza timu yetu ilikua ipo kati na kati iweje mashabiki hawa wafanye vurugu wakimaanisha hawa rhdhishwi na uongozi wa timu?
Rage huyu alitufanyia maigizo katika suala la uwanja wa timu kiasi mpaka leo halipo tena katika utekelezwaji
rage huyu huyu amekua na siasa nyingi mdomoni kuliko vitendo ana longolongo nyingi lakini kuna baadhi yatu hatutaki maamuzi magumu why?
Utashangaa hiyo tarehe moja mashabiki hawa hawa wa dar wanapiga chereko na vifijo kukubaliana na huyu mwanasiasa
kama mnaendeshwa na nguvu za viroba nyie watu wa dar tafadhali siku ya mkutano mkuu msinywe muda wa kuifanya simba itulie ni atoke mtu hapa!

Acheni uoga wa kitoto
 
Ni kweli kabisa, mashabiki wa simba dar siwafagilii kabisa
 
Back
Top Bottom