Mashabiki wa Lowassa, mmeyafikiria haya?

Mashabiki wa Lowassa, mmeyafikiria haya?

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
NAOMBA nikiri kwamba pamoja na kuwa mfuatiliaji sana wa mambo ya siasa, nchini na duniani kwa ujumla, si kawaida yangu kuandika hasa kuhusu siasa kwenye magazeti. Nimeaamua kuvunja kawaida yangu baada ya kuona mushkeli mkubwa kuhusu namna ambavyo siasa zetu zinakwenda katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.

Liko vuguvugu kubwa limezaliwa sasa nchini, wananchi wengi wanasikika wakitaka mabadiliko, hii ni haki kabisa kwa sababu chini ya jua hakuna kitu cha kudumu isipokuwa mabadiliko. Hiyo kiu ya mabadiliko ni haja ya kawaida kabisa kwa binadamu yeyote. Lakini kitu kinachonitisha kuhusu mabadiliko ya wanayoyatamani baadhi ya Watanzania, ni aina ya mabadiliko wanayoyataka, na mtu wanayeamini ataleta mabadiliko hayo.

Aliyekuwa mtia nia wa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, ambaye sasa ni mgombea wa Urais kupitia Chadema, akiungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ndiye anayeonekana kuwa mbeba bendera ya mabadiliko hayo. Sina tatizo binafsi na Lowassa, lakini kinachonitatizo ni vitendo vyake kuelekea katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Najiuliza ni kwa kiasi gani wafuasi wa Lowassa, walioko Chadema na Ukawa na wale wanaomfuata alikohamia kutoka CCM, wanachukua hata dakika moja kutafakari aina ya mtu wanayemuunga mkono kwa nguvu zote namna hiyo. Hayo mabadiliko wanayoyaimba kila siku yataletwa naye wanajua ni mbadiliko ya aina gani?

Sitaki kuwahukumu, lakini sina uhakika kama wanatafakari kwa makini aina ya mabadiliko wanayotaka na mtu wanayemtumaini kuongoza mabadiliko hayo. Dalili zinaonyesha uko uwezekano mkubwa wanafanya hivyo kwa sababu wameamua kuwa mashabiki tu ili kuridhisha nafsi zao.

Duniani kote viongozi wanaoongoza mabadiliko au mapinduzi yaliyoleta manufaa kwa jamii zao, kwanza ni lazima wawe na falsafa wanayoisimamia, wawe tayari kuifikia falsafa hiyo, na zaidi sana wawe na msimamo unaoaminiki, kiasi kwamba yeyote anayemfuata anakuwa na uhakika na kauli na vitendo vya kiongozi huyo.

Kuwa na kigeugeu haijawahi kuwa sifa ya kiongozi wa dhati anayesimamia mabadiliko ya kweli kwenye jamii.
Nikimtazama Lowassa, kwa dhati ya moyo wangu, sioni kama ni kiongozi wa kuaminika, sioni ndani yake uongozi wenye uwezo wa kusimamia kauli zake kwa dhati, bila kujali zinaweza kumgharimu kiasi gani ili mradi anaamini katika msingi ya aina fulani.

Siyasemi haya kwa sababu nina chuki binafsi naye, lakini nayasema kwa sababu ni mambo yaliyo dhahiri kwa kila mtu. Mei 30, mwaka huu 2015, wakati anatangaza nia kuomba kuwania urais kupitia CCM, jijini Arusha haya ndiyo aliyotuambia Watanzania.

"Kiuchumi, tumeshuhudia ukuaji mzuri na kuongezeka kwa mapato ya ndani ya Serikali na uimarishaji wa mfumo wa uwajibikaji na ulipaji kodi. Kwa upande mwingine, Serikali ya Rais Benjamini Mkapa na Rais Jakaya Kikwete zimefanya kazi kubwa katika uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi asilia ambapo kiwango kikubwa cha gesi asilia kimegunduliwa.

"Tanzania sasa imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazovutia uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo ambayo inatajwa kwamba inaweza kuja kubadilisha kabisa maisha ya Watanzania.

"Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kipindi chake na kama ambavyo amekuwa akisisitiza mara kwa mara katika hotuba zake za karibuni ni kwamba yeye ametekeleza wajibu wake. "Pia amesema anamwachia atakayemkabidhi uongozi wa nchi yetu baada ya yeye kumaliza muda wake kuendeleza pale atakapoachia".

"Serikali za awamu zilizotangulia zimeyajadili na kujaribu kuyatafutia ufumbuzi. Mimi pia nimekuwa sehemu ya jitihada hizi wakati wa utumishi wangu katika chama na serikali huko nyuma".

Ilipofika Agosti 10, mwaka huu 2015, baada ya kuchukua fomu ya uteuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, alituambia Watanzania kwamba;"Rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete kauharibu uchumi wa nchi, lakini sitaki kutoa mashtaka nataka kuzungumza kwa data, mwaka 2005 wakati Rais Benjamin Mkapa alipomaliza muda wake kilo moja ya sukari ilikuwa shilingi 650 lakini sasa hivi kilo moja ni Sh. 2,300, mchele umepanda hadi Sh. 2,220, sembe ni Sh. 1,200 na kibiriti ilikuwa Sh. 50 lakini sasa hivi ni Sh 200," "Katika hali hiyo CCM haina haki ya kuendelea kutuongoza, nawaalika wenzangu waliobaki CCM waje bila haya, waelewe matumaini yapo ndani ya chama chetu, (Chadema)".

Lakini akitangaza nia Arusha huu ndiyo ulikuwa msimamo wake kuhusu CCM; "Najua kwamba Ilani ya CCM ya mwaka 2015 imo katika hatua za mwisho za kukamilishwa na itakapopata baraka za vikao vya chama itakuwa ndiyo msingi wa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano itakayochaguliwa Oktoba mwaka huu." Hapo alikuwa akimaanisha serikali itakayoongozwa na CCM, lakini akaongeza

"Lakini kama alivyotuusia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1995, wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini, Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM! "Sina shaka, CCM tunao uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka".

Wiki chache baadaye msimamo wake ukawa huu; "Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kujidanganya mimi mwenyewe na umma wa Watanzania kwa kusema kuwa bado nina imani na CCM au kuwa CCM ni chama kitakachowaletea ukombozi wa kweli wa kiuchumi, kisiasa na kijamii. CCM niliyoiona Dodoma siyo tena kile chama nilichokulia na kilichonipa malezi na maadili ya siasa yaliyojengwa kwenye misingi ya haki, usawa na uadilifu."

"Ni dhahiri kwamba CCM imepotoka na kupoteza mwelekeo na sifa ya kuendelea kuiongoza Tanzania yetu. Mimi kama Mtanzania aliye na uchungu na nchi yake nasema imetosha na sasa basi! "Hivyo basi, baada ya kutafakari kwa kina nimeamua kuwa kuanzia leo ninaondoka CCM na kuitikia wito wa Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuungana nao katika kuleta mabadiliko ya kweli ya nchi yetu".

Ukiyasoma kwa umakini maneno haya, unaona wazi kwamba ndani ya kipindi cha majuma nane, amekuwa na misimamo miwili mizito inayokinzana kuhusu CCM. Ninachokiamini mimi ni ukweli kwamba CCM inaweza kuwa na matatizo yake makubwa, lakini haiwezekani yakawa yalitokea ndani ya muda mfupi kiasi hicho, yaani kuanzia alipokatwa, na alipohamia Chadema. Kama kupoteza mwelekeo wa kuongoza hakuwezi kuwa kumekuja CCM ndani ya muda wa siku 30 tu, kama huo ubovu upo aliuujua tangu kabala ya kuchukua fomu kugombea Urais.

Sasa kama alitambua hilo, kwanini aliamua kuimwagia sifa CCM na uwezo wa ilani yake kuingoza serikali ya awamu ya tano, lakini alipokatwa ghafla zile sifa ‘nzuri' za CCM zikafutika. Mara ghafla ikawa hakiwezi tena kuingoza nchi, msimamo ambao unakinzana na kauli yake aliyoitoa siku chache zilizotangulia.

Katika hili ni ama akiwa CCM alitudanganya ili apate anachokitafuta, au alisema ukweli na sasa akiwa Chadema, anatudanganya ili apate anachokitafuta, au anasema ukweli lakini awali alidanganya. Vyovyote vile inavyoweza kuwa, ndani ya muda huo wa kuhama kwake, kuna mahali amewahadaa na kuwadanganya Watanzania.

Hapa ndipo ninapopata shida, kwa sababu mtu ambaye kwa muda mfupi namna ile amekuwa na misimamo miwili tofauti inayokinzana kisiasa, unawezaje kumuamini kwamba hiki anachokisema sasa ni kweli na siyo uongo kama ambavyo alituambia Mei na anayotuambia sasa.

Sina uwezo wala mamlaka ya kumchagulia mtu aina ya mtu au chama cha kuunga mkono kwenye siasa, hilo litakuwa ni kuingilia uhuru wa mtu, lakini ninao wajibu kama raia mwema wa taifa hili, kuwakumbusha wananchi kuona kile ambacho inawezekana wengine hawakioni au hawataki kukiona.Tunapotaka mabadiliko lazima pia tuukubali ukweli mchungu kwamba mabadiliko lazima yawe ni kwa manufaa mapana ya jamii yote, na siyo ya kikundi cha watu wachache, kuwatumia wananchi wengi kujipatia maslahi yao binafsi.

Mabadiliko yoyote yale lazima yasimamiwe na watu makini, wanaoweza kuaminika, kutumainiwa kutokana na uthabiti wa maneno ya vitendo vyao, umuazi wa kuwa na misimamo miwili inayotofautina mithili ya mbingu na ardhi ndani ya muda mfupi hivyo kwenye mambo makubwa ya nchi, haiwezi kuwa sifa ya kutumainiwa kuongoza mabadiliko tena

Chanzo: Raia Mwema
 
Mmmmmhhhhh!!
Mi naona ukweli mtupu hapa. Ngoja wengine nao wapite.
 
Lowasa katoka CCM na yuko CDM(UKAWA) huku kuna watu tofauti na mfumo tofauti kiuhalisia yeyote yule atakayegombea kupitia CCM hata awe na bidii vipi hawezi kulikwamua taifa hili na umasikini tulionao kwani tatizo ni mfumo na waliopo huko mfano hai ni jinsi Kikwete alivyobadili mara kadhaa balaza la mawaziri lakini tatizo lilibaki palepale had I anaondoka hajafanikiwa kuwa na baraza bora la mawaziri.
 
Unataka kuwalisha watu matango pori.JK ndio kavuruga kabisa uchumi wa nchi hii,uko hoi bin taaban,halafu mnasifia ujinga.
 
Mwandishi katumwa. Anayefaidika na uwekezaji ni nani?
Ccm imezeeka haifanyi mapindunzi tena, ni propaganda tu na ufisadi.
Wananchi wanataka kufanya mapinduzi yao ya kisiasa, kiuchumi na kifikra.

Walimkata wenyewe wasubiri na wao kukatwa.
 
mkulimawakiteto

Mleta maana unachekesha kweli,.... Mbona Magufuli anamsifia hivyo Kikwete, na amekuwa point of reference kila anapohutubia kwamba kachapa kazi balaa, halafu apo apo anasema anashangaa kwanini pembe za ndovu zinakamatwa ulaya? Madawa yanakosekana hospitali ? Uwepo wa Mafisadi? Kama nayeye sio mnafiki mkubwa ninini?
 
Last edited by a moderator:
KATIKA ufunguzi wa Kampeni za CCM, Leo tarehe 23_August 2015, viwanja vya Jangwani jijini, ile ISHARA KUBWA YA KIFO CHA CCM IMETIMIA.

Katika ufunguzi huo ambao kwa namna isiyo ya kawaida watoto wote wa awamu za CCM walikutana, tukianza na Makongoro anawakilisha awamu ya kwanza (badala ya marehemu baba yake Mwl Nyerere), kisha alikuwepo Mwinyi mwakilishi Wa awamu ya pili lakini pia alikuwepo Mkapa Wa awamu ya Tatu na Jk anayemalizia. CCM Nzimanzima ilitimia na wasimamizi Wa awamu zake zote.

IPO ISHARA moja tumeiishi tukiiamini kwenye maisha ya binaadam kwamba ikitokea ndani ya mwaka mmoja kwa watoto wa familia moja kwa pamoja mkakutana nyumbani kumwona mzazi, basi mjue mzee wenu huyo mwaka huo lazima aitwe na Mola.

Maisha yangu yote nimekuwa nikichunguza na kuchambua ISHARA HII. Nilicho gundua ni kweli. Kila MTU ukimuuliza mzazi wake alivyo fariki atakujibu "ah Tena Bahati tu nilikwenda msabahi kabla hajafa" Hii ni ISHARA ambayo haikwepeki, utakuta automatic mnakutana kumwona mzee wenu na soon anarudisha tarakimu zake.

Hata safari zenyewe za kumwona Mzee wenu huwa za ajabu au kushtukiza au inatokea tu kijisababu kinakufanya at that time uwe home.

Mfano mzuri ni Mkapa, hakuwa na mpango kabisa Wa kuhudhuria ufunguzi Wa kampeni. Walitaka wamweke kwenye timu ya kampeni akakataa. Mwenyezi Mungu akaona ili aiangushe CCM lazima kanuni za ishara zitimie, akatengeneza Tukio, waziri wake mkuu, yule mpinzani Wa Lowassa, aliyesema CCM wakimpitisha lowassa atazunguka nchi nzima kumpinga, Mwenyezi Mungu akaanza nae, akamfungua macho Sumaye, akaona ukweli kwamba sababu zote walizompaka matope Lowassa si za kweli, na kwa kasi ya ajabu akakunja kona na kuingia ukawa.

Baada ya tukio hilo likamchimbua Mkapa, akafura na kuvamia jangwani akimpitia na Mwinyi kwa staili ya kuongeza nguvu kumbe ni Mpango Wa Mungu aiangushe CCM.

Mfano Mwingine ni Makongoro. Makongoro ambaye yuko against na familia yake na jamaa za Nyumba ya babake yeye peke yake ndiye anayejihusisha na CCM ili ale. Mapigo mawili yaani lile la kutupwa nje kabisa kwenye utia nia Wa urais ndani ya CCM na lile la kuondolewa na kutupwa tena hata kwenye Ubunge KAWE vingetosha kumuathiri na kuketi kando na CCM na kuungana na fimilia yake.

Lakini Mwenyezi Mungu bado akamtaka ili atimize ishara siku ya Leo, akamfanya achaguliwe kwenye timu ya kampeni tena kamati ya hela na kuahidiwa ubunge kwenye nafasi kumi za prezda. Kwa matofali hayo jamaa akabakia chamani hadi Leo alipo fanyika nguzo muhimu kutimiza ishara ya kifo.

The Very same to CCM, WATOTO WOTE WA CCM WA AWAMU ZOTE NNE KWA MPIGO WAMEKUTANA KWA MZEE WAO CCM. Wanadhani wamekwenda kwa tukio, au kutia nguvu, au kufanya kampeni kumbe wameitwa maksudi na nguvu ambazo hata wao hawawezi kuzicontrol ili protokali za elimination cycle zitimie na zimetimia.

Hii ni kanuni kubwa sana ya nguvu za maisha. Hakuna linalo weza kufanyika kuokoa CCM baada ya ishara Hii kutimia.

Mtaona ishara zaidi kuanzia Leo, CCM itaanza na kuzidi kudhoofu. Wataanza kutukanana na kusalitiana wenyewe kwa wenyewe. Mtaona na kuamini kwamba ISHARA HII HAIKOSEI.
Ni wajinga tu ambao huenda vitani bila kusoma majira na nyakati za ishara. Zamani wafalme wenye akili wakitaka kwenda vitani walingojea ishara kwanza kutoka kwa nabii. Hakuna mwenye akili aliye thubutu kwenda vitani pasipo subira ya ishara kutoka kwa nabii.

Manabii walikuwa na namna yao ya kusoma ishara za Mwenyezi Mungu. Nabii akiona ishara flani ndipo anamstua mfalme aende vitani na asipoona ishara anamwambia live mfalme kwamba ishara hajaona amavipi aende vitani tu hivyo hivyo kwa risk zake. Na kila mfalme aliyediriki kwenda vitani kwa ubabe wake au ujuzi wake Wa vita au kiburi cha wingi Wa jeshi lake alinyukwa vibaya na kufia vitani. Wadau wa mambo ya dini wanajua sana mambo hizi.

Wafalme wenye akili, hatakama wana jeshi na nguvu kiasi gani, hawawezi kuthubutu kwenda vitani pasipo Ishara. Mamburura, wapuuzi na wajinga ndio huenda kichwakichwa wakafyekwa.

Ushindi Wa chochote huasisiwa na Mwenyezi Mungu, Na Mungu akisha panga kitu chake zipo ishara zitaonekana tu.

Mimi si shabiki wala mfuasi Wa CCM, ni mfuasi Wa mabadiliko. Lakini asilani siandiki haya kwa mvuto wa utashi Wa mapenzi yangu kwenye mabadiliko lakini ni devine fact ambazo ziko hivyo wala sio utashi wangu kuzibadili.

Asilimia zaidi ya 82 ya watanzania wanataka mabadiliko. Lakini nikawa najiuliza bado CCM Inaweza kung'ang'ania kubakia madarakani ama kimabavu, wizi au matumizi mabaya ya vyombo vya Dola. Hivyo mbali na wananchi kutaka mabadiliko lakini CCM wanaweza kudiriki kumwaga maelfu ya Damu ili wabakie madarakani. Hofu Hii nilikuwa Nayo na nadhani watu wengi walikuwa na hofu kama Hii. Lakini baada ya Ishara Hii, CCM haipo. Hakuna umwagaji damu wala nini. CCM HAIPO TENA. MABADILIKO HAYA KUNA MKONO WA MWENYEZI MUNGU. NANI ANAYE WEZA KUSHINDANA NA Mungu?!
 
Ilikuwa plan b yake akikatwa anaenda ukawa, tatizo nini hapo.
 
Habari ndugu,
watakaoelewa na waelewe..na
Ili kunielewa mada yangu naomba usilete ushabiki wa chadema uweke kando kuwa kama mtu mwenye fikra huru..mwanzo nilijua kifungo kibaya kwa mwanadamu ni dini pekee ipo kwa ajili ya wachache kunufaika uwongo mwing ndani yake,nisigusie sana kuhusu dini ili kuepusha kuchokoza watu kiimani
Kifungo cha pili alichoweza kufungwa binadamu ni siasa...tumefanywa mitaji na binadamu wenzetu hivi vyama vinaendeshwa na watu kama sisi na tunajua watu tuna sifa za unafki,tamaa,uwongo kama wewe usivo na huruma na wengne basi tambua hata huyo unayemwona mchapakazi au mkombozi vile vile ni binadamu na anajionea huruma yeye kuliko anavyokuonea wewe
unajua siasa ina mambo mengi wananchi sasa hivi hatufanyi reasoning tumeishia kutumika kama mitaji ya wanasiasa
Leo hii tunawashabikia viongozi wa ccm au wa ukawa tunajifanya hatuoni kama wenyewe wako pale/watakuwepo kwa ajili ya maisha yao,familia zao na koo zao..tupo kama misukule
Inauma sana great thinker amefanywa kama mtumwa chini ya tajiri lowasa au mbowe tunajifanya hatuoni kama wale wanapesa/wanataka pesa kama kweli wangekuwa na nia na huruma na wananch kwanini wasituambia sera zao wazi ni lini rasilimali zetu zitakuwa chini ya serikali watakayounda,tumeishia kuwashabikia.ndugu zangu wale hawana uzalendo
Ukirudi kwa upande wa ccm ndo matatizo matupu najuta kuzaliwa tanzania nchi hi wanafaidika wachache kama kweli kina kikwete na magufuli wangekuwa na huruma wangewezaje kuwatazama maskini wa kutupwa vijijini ilihali hata mlo hawapati..tunaona tumeletewa maendeleo kumbe ndo wananufaika wenyewe mfano eti mtu anaisifia serikali ya ccm imemsaidia yeye sasa iv ana smartphone hajiulizi kama amenunua hvo amenufaisha mtengenezaji na mtengenezaji naye kamuwezesha mwanasiasa kisha anaekewa mifumo inayomkinda..siasa bwana unafurahia serikali ya ccm eti imejenga barabara unasahau kama ni kwa pesa zako unasahau pia kama hzo barabara ni kwa ajili ya kuwarahisishia kupitisha mizigo yao ambayo wanakuuzia tena kwa pesa yako
Tusidanganyane siasa ni mchezo unaocheza na akili ya binadamu,sisi ni watumwa tunashangilia maigizo ya binadamu wenzetu ambao hawatupi elimu ili tuendelee kuwa wapumbavu
Hakuna atakaye kuja kutukomboa only strong ndo wata survive wengne tutaendelea kulalamikiwa na vizazi vinavokuja kwa maamuzi tunayofanya sasa kwa ushabiki..watoto wetu watakuja kushangaa kwa nini tulisikiaga kuwa kuna watu walichota mabilion lakini hawaulizwa?watoto wetu watakuja kushangaa mmoja wapo wa anayesemakana fisadi anashangiliwa kwanini tunajisahaulisha mapema hivi?binadamu tuna tatizo gani?
Ccm mmetupoteza mpaka wasomi na watu wanajiita watakatifu(viongozi wadini)mme wanununua hivo hivo pia kwa upinzani mnadanganya mpaka ma great thinker humu ndani wanawashabikia..jibu ni kuwa na nyie mnadanganya na wazungu (wawekezaji) kwa kupewa uwongo kisha mnatapeliwa ,siasa mfumo wa kijinga sana mtu kweli unajikuta unamshabikia mwizi au yule ambaye sio mwizi unamwona hafai
Taifa hili linachekesha,viongozi wote wanachekesha,wananchi mnachekesha hivi mnadhani wale waarab wanavofanya vita kulinda rasilimali mnadhani wanakosea..walioiba mabilioni wanaonekana wazuri
UKAWA MMEONEKANA MNAWEZA KULETA MABADILIKO WANAYOTAKA WATU LAKINI JE MBONA KUNA MAMBO HAMUWEKI SAWA?NI KIVIPI MTAZUIA MAKAMPUNI KUMILIKI RASILIMAL ILA TAIFA NDO LIMILIKI KILA KITU AU NDO YATAKUWA KAMA CCM KUACHIA WATU WAVUNE MADINI?WAZUNGU WATU WABAYA SANA
Ukawa ningewaona wa maana kama mnge utangazia umma kuwa mkishka nchi rasilimal zitalindwa nyie mnasubiri mpaka siku ya kufungua kampeni ili mkusanye watu wengi lengo ni kuwa lipiza ccm?ETI LEO SIASA ZA TANZANIA ZINABEBWA NA MISAMIATI YA KITOTO MFANO KILA CHAMA KINATAKA KIPATE MAFURIKO siasa za majitaka sana
Embu jiulize kwani kampeni zikifunguliwa kwenye ukumbi mfano mlimani city hazitafunguka?
MY TAKE:NAJUA WENGI MTANIDHARAU KWAMBA NIMEANDIKA ULOFA LAKINI LAZIMA TUJUE KUWA SISI TUNASHABIKIA UTUMWA CHINI YA BINADAMU WENZETU KIPINDI TUNARUSHIANA VIJEMBE JUU VISIVYO NA UMUHIMU KULE WENGNE WANAKULA VIZURI WENGNE VBY
Nimejitoa rasmi kwenye ushabiki nataka niwe mtu huru kichwan nibaki na vitu vya msing vinavyonihusu mimi moja kwa moja
USHABIKI UNAKWENDA KUHARIBU TAIFA MTANIAMBIA
Waasalam
 
People's power. Ngonjera tumechoka. Hata bila kampeni habari ya mwaka huu ni Lowasa-Ukawa-Ikulu-Katiba mpya
 
mi kasema hivi shabiki Eni ila msije toe ufahamu hali ya mzee wetu si shwari tuliomuona vizuri mitaani mungu tu ndio anajua hawezi kusimama hata dk40 hivi tunampaje urais watu tunataka kujua sera zake tola kwenye kinywa chake hivi hizo dk10 zitatosha kweli anyway chadema mmeniangusha kweli kweli hata kamatungekosa kipindi hiki tungeendelea kukijenga chama na viti bungeni vingeobgezeka ila kwa hili chadema tunechemka huyu kaja kuua chama mbatia kafurahi shughuri ile atakuwa anaipata kwa uhakika
 
Maandiko mazuri sana nä yenye elimu inayotaka akili kidogo...
 
Nashukuru mkuu wewe ni mmoja wa watu wasioyumbishwa na matakwa ya homosapiens mwenzako..watu hawajiulizi vipi keki ya taifa itagawanywa sawa kwa hio miaka kumi ijayo,aidha ishinde ccm au ukawa lazima watu wahoji mgawanyo ulio sawa , jiulize kuna wananch vijijini hawana hata viatu je kina lowasa hawakuwepo madarakani je kina magufuli wamewah kufikiria kugawana mali zao na maskini
mimi hoja yangu ni kuwa tushiriki kwenye siasa kudai rasilimal zilindwe kwa nguvu zote

Ushabiki tulio nao sisi ni wa kijinga tunamshabikia mtu mwenye urafiki na kina chenge?
Viongoz wote wabaya tu,hawana nia ya dhati au hata kama wanayo wanawaonea huruma marafiki zao wafanyabiashara kuliko mpiga kura
MY TAKE:TUBADILIKE TUWAHOJI HAWA WANAOTAKA UONGOZI WANA MISIMAMO GANI NA RASILIMALI ZINAZOENDELEA KUPUNGUA
Tujenge utaifa japo tunampenda lowasa lakini pia tuthubutu kumuuliza atafanya nini kumilikisha migodi yote kwa serikali
 
Mfumo..... mfumo umekuwa mfumo.......
Eti mabadiliko, kunguni ni wale wale, wamehama kitanda tu
 
Unataka kuwalisha watu matango pori.JK ndio kavuruga kabisa uchumi wa nchi hii,uko hoi bin taaban,halafu mnasifia ujinga.


Umeisoma vizuri habari yote?
IF IS "YES"

Mbonaunachojibu ni tofauti na maswali uliyoulizw?

Be a great thinker
 
Nimekupuuza baada ya kugundua wewe ni mfuasi wa ccm. Shenzi type

mbaya zaidi hujajigundua kuwa kuwa ww ni bonge la mpumbavu ambaye huna fikra na wala huna mawazo zaidi upo hapa dunian kwaajili ya kufuata mkumbo tu.

Ni hasara kubwa sana kwa nchi kuwa na mwanachi kama ww. Bora kufuga vicheche 20 ndan ya nchi vinaweza kuwa na faida lakn sio mtu kama ww ambaye huna faida
 
Umeisoma vizuri habari yote?
IF IS "YES"

Mbonaunachojibu ni tofauti na maswali uliyoulizw?

Be a great thinker

mkuu hawezi kukuelewa kwasababu waliowengi wanaomshabikia lowasa wanashabikia tu lakn hawaelewi kwann wanamshabikia..

Mm ndio maana nasema heri kufuga vicheche 20 vinaweza kuwa na faida lakn sio kama huyo jamaa
 
NAOMBA nikiri kwamba pamoja na kuwa mfuatiliaji sana wa mambo ya siasa, nchini na duniani kwa ujumla, si kawaida yangu kuandika hasa kuhusu siasa kwenye magazeti. Nimeaamua kuvunja kawaida yangu baada ya kuona mushkeli mkubwa kuhusu namna ambavyo siasa zetu zinakwenda katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.

Liko vuguvugu kubwa limezaliwa sasa nchini, wananchi wengi wanasikika wakitaka mabadiliko, hii ni haki kabisa kwa sababu chini ya jua hakuna kitu cha kudumu isipokuwa mabadiliko. Hiyo kiu ya mabadiliko ni haja ya kawaida kabisa kwa binadamu yeyote. Lakini kitu kinachonitisha kuhusu mabadiliko ya wanayoyatamani baadhi ya Watanzania, ni aina ya mabadiliko wanayoyataka, na mtu wanayeamini ataleta mabadiliko hayo.

Aliyekuwa mtia nia wa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, ambaye sasa ni mgombea wa Urais kupitia Chadema, akiungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ndiye anayeonekana kuwa mbeba bendera ya mabadiliko hayo. Sina tatizo binafsi na Lowassa, lakini kinachonitatizo ni vitendo vyake kuelekea katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Najiuliza ni kwa kiasi gani wafuasi wa Lowassa, walioko Chadema na Ukawa na wale wanaomfuata alikohamia kutoka CCM, wanachukua hata dakika moja kutafakari aina ya mtu wanayemuunga mkono kwa nguvu zote namna hiyo. Hayo mabadiliko wanayoyaimba kila siku yataletwa naye wanajua ni mbadiliko ya aina gani?

Sitaki kuwahukumu, lakini sina uhakika kama wanatafakari kwa makini aina ya mabadiliko wanayotaka na mtu wanayemtumaini kuongoza mabadiliko hayo. Dalili zinaonyesha uko uwezekano mkubwa wanafanya hivyo kwa sababu wameamua kuwa mashabiki tu ili kuridhisha nafsi zao.

Duniani kote viongozi wanaoongoza mabadiliko au mapinduzi yaliyoleta manufaa kwa jamii zao, kwanza ni lazima wawe na falsafa wanayoisimamia, wawe tayari kuifikia falsafa hiyo, na zaidi sana wawe na msimamo unaoaminiki, kiasi kwamba yeyote anayemfuata anakuwa na uhakika na kauli na vitendo vya kiongozi huyo.

Kuwa na kigeugeu haijawahi kuwa sifa ya kiongozi wa dhati anayesimamia mabadiliko ya kweli kwenye jamii.
Nikimtazama Lowassa, kwa dhati ya moyo wangu, sioni kama ni kiongozi wa kuaminika, sioni ndani yake uongozi wenye uwezo wa kusimamia kauli zake kwa dhati, bila kujali zinaweza kumgharimu kiasi gani ili mradi anaamini katika msingi ya aina fulani. Siyasemi haya kwa sababu nina chuki binafsi naye, lakini nayasema kwa sababu ni mambo yaliyo dhahiri kwa kila mtu. Mei 30, mwaka huu 2015, wakati anatangaza nia kuomba kuwania urais kupitia CCM, jijini Arusha haya ndiyo aliyotuambia Watanzania.

“Kiuchumi, tumeshuhudia ukuaji mzuri na kuongezeka kwa mapato ya ndani ya Serikali na uimarishaji wa mfumo wa uwajibikaji na ulipaji kodi. Kwa upande mwingine, Serikali ya Rais Benjamini Mkapa na Rais Jakaya Kikwete zimefanya kazi kubwa katika uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi asilia ambapo kiwango kikubwa cha gesi asilia kimegunduliwa. “Tanzania sasa imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazovutia uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo ambayo inatajwa kwamba inaweza kuja kubadilisha kabisa maisha ya Watanzania.

“Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kipindi chake na kama ambavyo amekuwa akisisitiza mara kwa mara katika hotuba zake za karibuni ni kwamba yeye ametekeleza wajibu wake. “Pia amesema anamwachia atakayemkabidhi uongozi wa nchi yetu baada ya yeye kumaliza muda wake kuendeleza pale atakapoachia”. “Serikali za awamu zilizotangulia zimeyajadili na kujaribu kuyatafutia ufumbuzi. Mimi pia nimekuwa sehemu ya jitihada hizi wakati wa utumishi wangu katika chama na serikali huko nyuma”.

Ilipofika Agosti 10, mwaka huu 2015, baada ya kuchukua fomu ya uteuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, alituambia Watanzania kwamba;“Rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete kauharibu uchumi wa nchi, lakini sitaki kutoa mashtaka nataka kuzungumza kwa data, mwaka 2005 wakati Rais Benjamin Mkapa alipomaliza muda wake kilo moja ya sukari ilikuwa shilingi 650 lakini sasa hivi kilo moja ni Sh. 2,300, mchele umepanda hadi Sh. 2,220, sembe ni Sh. 1,200 na kibiriti ilikuwa Sh. 50 lakini sasa hivi ni Sh 200,” “Katika hali hiyo CCM haina haki ya kuendelea kutuongoza, nawaalika wenzangu waliobaki CCM waje bila haya, waelewe matumaini yapo ndani ya chama chetu, (Chadema)”.

Lakini akitangaza nia Arusha huu ndiyo ulikuwa msimamo wake kuhusu CCM; “Najua kwamba Ilani ya CCM ya mwaka 2015 imo katika hatua za mwisho za kukamilishwa na itakapopata baraka za vikao vya chama itakuwa ndiyo msingi wa utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano itakayochaguliwa Oktoba mwaka huu.” Hapo alikuwa akimaanisha serikali itakayoongozwa na CCM, lakini akaongeza

“Lakini kama alivyotuusia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1995, wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini, Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM! “Sina shaka, CCM tunao uwezo wa kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka”.

Wiki chache baadaye msimamo wake ukawa huu; “Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kujidanganya mimi mwenyewe na umma wa Watanzania kwa kusema kuwa bado nina imani na CCM au kuwa CCM ni chama kitakachowaletea ukombozi wa kweli wa kiuchumi, kisiasa na kijamii. CCM niliyoiona Dodoma siyo tena kile chama nilichokulia na kilichonipa malezi na maadili ya siasa yaliyojengwa kwenye misingi ya haki, usawa na uadilifu.”

“Ni dhahiri kwamba CCM imepotoka na kupoteza mwelekeo na sifa ya kuendelea kuiongoza Tanzania yetu. Mimi kama Mtanzania aliye na uchungu na nchi yake nasema imetosha na sasa basi! “Hivyo basi, baada ya kutafakari kwa kina nimeamua kuwa kuanzia leo ninaondoka CCM na kuitikia wito wa Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuungana nao katika kuleta mabadiliko ya kweli ya nchi yetu”.

Ukiyasoma kwa umakini maneno haya, unaona wazi kwamba ndani ya kipindi cha majuma nane, amekuwa na misimamo miwili mizito inayokinzana kuhusu CCM. Ninachokiamini mimi ni ukweli kwamba CCM inaweza kuwa na matatizo yake makubwa, lakini haiwezekani yakawa yalitokea ndani ya muda mfupi kiasi hicho, yaani kuanzia alipokatwa, na alipohamia Chadema. Kama kupoteza mwelekeo wa kuongoza hakuwezi kuwa kumekuja CCM ndani ya muda wa siku 30 tu, kama huo ubovu upo aliuujua tangu kabala ya kuchukua fomu kugombea Urais.

Sasa kama alitambua hilo, kwanini aliamua kuimwagia sifa CCM na uwezo wa ilani yake kuingoza serikali ya awamu ya tano, lakini alipokatwa ghafla zile sifa ‘nzuri’ za CCM zikafutika. Mara ghafla ikawa hakiwezi tena kuingoza nchi, msimamo ambao unakinzana na kauli yake aliyoitoa siku chache zilizotangulia.

Katika hili ni ama akiwa CCM alitudanganya ili apate anachokitafuta, au alisema ukweli na sasa akiwa Chadema, anatudanganya ili apate anachokitafuta, au anasema ukweli lakini awali alidanganya. Vyovyote vile inavyoweza kuwa, ndani ya muda huo wa kuhama kwake, kuna mahali amewahadaa na kuwadanganya Watanzania.

Hapa ndipo ninapopata shida, kwa sababu mtu ambaye kwa muda mfupi namna ile amekuwa na misimamo miwili tofauti inayokinzana kisiasa, unawezaje kumuamini kwamba hiki anachokisema sasa ni kweli na siyo uongo kama ambavyo alituambia Mei na anayotuambia sasa. Sina uwezo wala mamlaka ya kumchagulia mtu aina ya mtu au chama cha kuunga mkono kwenye siasa, hilo litakuwa ni kuingilia uhuru wa mtu, lakini ninao wajibu kama raia mwema wa taifa hili, kuwakumbusha wananchi kuona kile ambacho inawezekana wengine hawakioni au hawataki kukiona.Tunapotaka mabadiliko lazima pia tuukubali ukweli mchungu kwamba mabadiliko lazima yawe ni kwa manufaa mapana ya jamii yote, na siyo ya kikundi cha watu wachache, kuwatumia wananchi wengi kujipatia maslahi yao binafsi.

Mabadiliko yoyote yale lazima yasimamiwe na watu makini, wanaoweza kuaminika, kutumainiwa kutokana na uthabiti wa maneno ya vitendo vyao, umuazi wa kuwa na misimamo miwili inayotofautina mithili ya mbingu na ardhi ndani ya muda mfupi hivyo kwenye mambo makubwa ya nchi, haiwezi kuwa sifa ya kutumainiwa kuongoza mabadiliko tena

Chanzo Raia Mwema

Sisi tunataka ssm iondoke kwanza mambo mengine tutajua huko mbele! Ni heri nusu shari kuliko shari nzima! watu wameshachoka tunataka heshima ya mwananchi irudi kwanza mambo ya watawala kutufanya malofa na wapumbavu ifike mahali tuheshimiane! Tukimtoa huyu anayejifanya ndo mama wa taifa hili wengine watajifunza hamana atakaye tuchezea tena maana watajua wananchi si wakuchezea kama wanavyo tufanyia sasa hivi

Hamna hata siku moja utafanya mabadiliko yasiyokuwa na risk, lazima tukubali kuchukua risk kama tunataka kufika mahali tunapotaka! mambo ya kuogopa kubadilisha ni ujinga mbona wewe wazazi wako wakifa wewe mtoto unaendelea na maisha kama kawaida! Kwanini tuogope ssm kufa bana? Hata hivyo anayekuja kutawala ametoka ssm hivyo hatatutakuwa tumeondoa ssm ghafla ni kama tunaenda na serikali ya mseto wa ssm na upinzani bana!

Acha kuogopa mabadiliko utabaki hapohapo ulipo miaka nenda rudi, uteendelea kubadilisha marais tu ssm lakini wewe hutabadilika!
 
Back
Top Bottom