Masha akimbilia Takukuru

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Masha akimbilia Takukuru

lC.gif
Mwandishi Wa RaiaMwema Julai29,2009
bul2.gif
Ni sakata la vitambulisho


SAKATA la Vitambulisho vya Taifa limeingia katika hatua mpya baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrance Masha, kulipeleka suala hilo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Raia Mwema limefahamishwa kwamba Masha amepeleka suala hilo Takukuru kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Patrick Rutabanzibwa, uamuzi ambao umeelezwa kuwa huenda ukaibua utata mwingine kutokana na kuelekea kuhoji maamuzi yaliyofikiwa na Baraza la Mawaziri.
Baraza la Mawaziri liliidhinisha kuendelea kwa mchakato wa mradi wa vitamulisho, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha kuwapo kwa mtaalamu mshauri ambaye alikabidhi kazi zake serikalini kwa utekelezaji, mapendekezo ambayo baadhi yamekuwa yakitekelezwa na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Habari za ndani ya Takukuru zimeeleza kwamba tayari watu kadhaa wanaohusika na mradi huo wamekwisha kuhojiwa ikiwa ni pamoja na baadhi ya watendaji wa serikali ambao wameelezwa "kutoa ushirikiano mkubwa" kwa wachunguzi na hivyo kuweza kuibua mambo mazito zaidi.
Alipoulizwa na gazeti hili kuhusu uamuzi wa Wizara hiyo kwa kuzingatia maelekezo yake kushitaki uamuzi wa Baraza Takukuru, Masha alisema; "Siko tayari kuongelea suala hilo. " Alipoulizwa kwa nini alijibu; "basi tu nimeamua. "
Kwa mujibu wa habari za uhakika zilizoifikia Raia Mwema, Waziri Masha ambaye amewahi kutuhumiwa kuingilia mchakato kumpata mzabuni wa kutekeleza Mradi wa Taifa wa Vitambulisho, safari hii anatajwa kuagiza viongozi walioko chini ya mamlaka yake kulipeleka suala hilo Takukuru, kipindi ambacho suala hilo likiwa katika hatua za mwisho za utekelezaji.
Ibara ya 54, kifungu cha kwanza, kinaeleza bayana kuwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri linaloongozwa na Rais, ni pamoja na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa
Zanzibar na Mawaziri wote.
Kifungu cha pili katika ibara hiyo, kinaeleza kuwa Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye atakayeongoza mikutano hiyo, au Makamu wa Rais na kama wote wawili hawapo, Waziri Mkuu ndiye ataongoza mikutano hiyo.
Kifungu cha tatu cha Ibara hiyo ya 54, inaeleza kuwa Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.
Ibara ya 54, kifungu cha tano cha Katiba, inatamka wazi kuwa uamuzi wa baraza haupaswi kuhuchunguzwa hata na Mahakama kwa kuwa hatima ya uchunguzi huo ni kufunguliwa kwa mashitaka.
Kifungu hicho kinaeleza; Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika mahakama yoyote.
Masha amekuwa akituhumiwa kuingilia mchakato wa Mradi wa Vitambulisho vya Taifa na wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka wa fedha 2009/2010, aliwahi kuhoji kuwa kuna nini kwenye mradi huo.
Mwenendo wa Waziri Masha kuhusu mradi huo umekuwa hauwaridhishi wabunge wengi, na wakati fulani Kamati ya Bunge inayohusika na mradi huo iliwahi kumhoji pamoja na watendaji wengine kuhusu kile kilichowahi kuelezwa kuwa ni Waziri kuingilia mchakato wa kumpata mzabuni.
Mmoja wa wabunge hao ni Mbunge wa Maswa, John Shibuda. Katika mazungumzo yake Julai, mwaka huu na gazeti moja la kila siku, Shibuda alikaririwa akimshutumu Waziri Masha akionyesha dhahiri kutoridhishwa na mwenendo wake.
"Mimi najiandaa kuwasilisha hoja binafsi na kumpa Waziri Mkuu, Pinda (Mizengo), nyaraka zenye takwimu zinazoonesha hasara ambazo Taifa linapata kutokana uzembe wa Wizara ya Mambo ya Ndani chini ya Waziri Masha, unajua nadhani uongozi wa waziri unapaswa kuelewa muda wa kuwachezea walipa kodi ya Watanzania sasa umekwisha.
"Yale majibu yaliyotolewa juzi unaweza kusema ni ya kitoto kama alivyosema Mhe. Naibu Spika kwamba Watanzania hawahitaji yale majibu, wanachohitaji ni vitambulisho, hivi sasa kuna walipa kodi si zaidi ya 500,000, lakini tuko watu milioni 40, watu milioni 18 tu wakilipa kodi vizuri kwa mwaka tunaweza kukusanya bilioni 320 na kuacha utegemezi kabisa, hii ndio kiini cha hoja yangu," alisema Shibuda.
Kwa sasa Wizara hiyo inajiandaa kuwasilisha katika Baraza la Mawaziri waraka kuhusu suala hilo la vitambulisho, ikishindwa kufahamika wazi waraka huo utakuwa na mambo gani na nini itakuwa matokeo yake.
hs3.gif

Masha akimbilia Takukuru
 
Last edited:
naona mwandishi wa taarifa hii ana bias, na kutaka kugonganisha watu, kitu kilichopelekwa takukuru sio uamuzi wa baraza la mawaziri , bali ni mchachato wa kumtafuta atakaye pewa hiyo tenda.
Sasa huu ukajanja huu kwa kweli utatupeleka kubaya.
 
"Yale majibu yaliyotolewa juzi unaweza kusema ni ya kitoto kama alivyosema Mhe. Naibu Spika kwamba Watanzania hawahitaji yale majibu, wanachohitaji ni vitambulisho, hivi sasa kuna walipa kodi si zaidi ya 500,000, lakini tuko watu milioni 40, watu milioni 18 tu wakilipa kodi vizuri kwa mwaka tunaweza kukusanya bilioni 320 na kuacha utegemezi kabisa, hii ndio kiini cha hoja yangu," alisema Shibuda.
Kuna kitu kimepinda:

Kama Masha hatakiwi kuingilia mradi, kwanini yeye ndio anabanwa na kuulizwa mradi umefikia wapi?
 
Haiingii akilini kuwa kunawalipa kodi 500000 tu Tanzania

So inaingia wapi kama sio akilini???? Kodi zenyewe ndio anachukua Kingunge Ngombale Mwiru Ubungo terminal!! It looks like negros are skipping tax because it aint doin' nothin' for their lives!
 
Nchi yangu ina mizengwe ? Nini maana ya tukio hili?Kuwasafisha takukuru ama kuna move gani hapa ? Fungueni macho na akili maana any move done by CCM ina manufa kwa ukoo wao .Msilale hadi kieleweke
 
Back
Top Bottom