'Masauni Mwingine' Aibukia Kahama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Masauni Mwingine' Aibukia Kahama!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Buchanan, May 26, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  May 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Shija Felician, Kahama
  BUNDI mbaya wa tatizo la kudanganya umri sasa ameng'ang'ania kwenye tawi la vijana ndani ya CCM baada ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo wilayani Kahama kutakiwa ajiuzulu kwa madai kuwa ana umri mkubwa unaotosha kugombea urais.

  Mwenyekiti huyo wa umoja huo wa vijana wa CCM, Robert Kapera anadaiwa kuwa na miaka takriban 40, umri ambao ni wa chini kwa mtu ambaye anataka kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano.
  Tuhuma hizo zimeibuliwa wiki moja baada ya mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM), Hamad Yusuf Masauni kulazimishwa ajiuzulu kwa madai kuwa hakuwa mkweli katika kueleza umri wake. Ilidaiwa kuwa cheti chake cha kuzaliwa kinaonyesha alizaliwa mwaka 1979 wakati fomu za kuomba hati ya kusafiria inaonyesha alizaliwa mwaka 1973.


  Siku mbili baada ya kulazimika kujiuzulu, watu walio karibu na Masauni walieleza kuwa masuala ya kudanganya umri ni ya kawaida kwenye chama hicho na hufanywa na viongozi wa juu pale wanapomuandaa mtu kwa uongozi wa baadaye.
  Na madai hayo yananza kudhihirika baada ya Kapera kukumbwa na tuhuma hizo na kutoa utetezi unaolingana na watu hao walio karibu na Masauni.


  Kapera anadaiwa kuwa hivi sasa amefikisha umri wa miaka 40 tofauti na taratibu za umoja huo ambazo zinataka viongozi wanaofikisha umri wa miaka 35 waachie ngazi.


  Vyanzo vya habari vililidokeza Mwananchi kuwa umri huo wa Kapera ulibainika katika fomu namba CCM - 007/2005 (C) ya kugombea udiwani mwaka 2005 ambayo aliandika kuwa alizaliwa mwaka 1970.
  Maelezo hayo ya Kapera kwenye fomu hiyo yanaonyesha kuwa alizaliwa maeneo ya Ukune wilayani Kahama mkoani Shinyanga.


  Lakini katika fomu aliyojaza mwaka 2008, fomu namba UVCCM 2 - 2008 ya kuomba nafasi ya mwenyekiti wa vijana wa wilaya ya Kahama, Kapera anaonekana kuwa alizaliwa mwaka 1978 katika kijiji cha Igalula wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
  "Hapa ndipo kwenye matatizo ambayo watu wanataka awajibike kwa udanganyifu huo. Inaonyesha alitumia udanganyifu katika fomu zote hizo kwa lengo la kujipatia madaraka," chanzo cha habari cha wilayani hapo kilieleza.
  Kapera, akizungumza na gazeti hili jana, alikiri kutoa maelezo tofauti katika fomu hizo akieleza kuwa ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa CCM wanapotaka kuwania uongozi.


  "Sikiliza wewe mwandishi, nenda kaandike tu... ninachojua mimi"Ninachojua mimi nina umri wa miaka 32; hii 40 iliyo kwenye fomu ya kuwania udiwani mwaka 2005 ambayo inaonyesha nilizaliwa mwaka 1970, nilijaza tu. Lakini nilizaliwa mwaka 1978."


  Hata hivyo, maelezo yake hayo yanazidi kuweka utata kwa kuwa yanapingana na yale yaliyo kwenye cheti chake cha kidato cha nne yanayoonyesha kuwa alimaliza elimu ya sekondari mwaka 1990, kitu ambacho kimahesabu kinamaanisha kuwa angemaliza akiwa na umri wa miaka 12 kama alizaliwa mwaka 1978.
  Katika cheti hicho, kilichotolewa na Shule ya Sekondari ya Bagamoyo iliyo mkoani Pwani, Kapera anaonekana alizaliwa mwaka 1978.


  Katibu wa CCM wilayani Kahama, Sospeter Nyigoti alisema wakati alipoulizwa kuhusu suala hilo kuwa sheria, taratibu na kanuni lazima ziheshimiwe.


  "Kama mkuu wa chama (mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete) amesema, sisi hatuwezi kumpinga. Tunamsubiri katibu wa UV-CCM wa wilaya ambaye yuko safarini aje achukue hatua za kisheria kwa mujibu wa taratibu zao walizojiwekea,"alisema Nyigoti.


  Baadhi ya wananchama wa UV-CCM walisema hawatakubaliana na udanganyifu huo na kwamba watahakikisha wanajisafisha hadi ngazi ya tawi kwa kuwafichua na kuwachukulia hatua viongozi wote wadanganyifu.
  "Kama hali hiyo itaendelea kufichuliwa itawakumba viongozi wengi kwa kuwa hata Bukombe na Shinyanga kuna tuhuma hizo," alisema mmoja wa wanachama hao.


  Akizungumza kwenye mkutano wa baraza kuu la UV-CCM ambao ulishuhudia Masauni na naibu katibu wake, Mohamed Moyo wakijiuzulu nyadhifa zao kutokana na sakata hilo, Kikwete aliwakumbusha vijana kuheshimu kanuni na taratibu walizojiwekea katika kuwapata wagombea wao.


  Kikwete pia aliwaonya vijana dhidi ya tabia ya kuchimbana ambayo alisema inawafanya waumbuane hadharani na kumuahidi kazi Masauni kwa uungwana aliounyesha wa kuachia ngazi baada ya kutuhumiwa.
  Hata hivyo, kujiuzulu kwa Masauni hakuwa lelemama. Jumuiya hiyo iligawanyika katika makundi mawili, moja likimpinga na jingine likimuunga mkono, hali iliyosababisha kuwepo kwa mtafaruku mkubwa hadi Masauni alipoandika barua ya kuachia ngazi.


  Source: MWANANCHI.
   
 2. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Bado siamini kama kuna watu waaminifu kabisa ambao wamo CCM.Ukiona mtu yuko CCM basi ujue kuna kitu ameficha!.Labda halipi kodi, au anaogopa kuchunguzwa, au..........
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  May 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Unataka kusema kwamba hata JK kuna vitu anaficha?
   
Loading...