Kabla ya kufunga kamera mpya tujuzwe kuhusu kamera zilizofungwa miaka ya 2000, kamera hizo baadhi zipo maeneo ya Polisi Kati mpaka Mnazimmoja pia zilikuwepo Tazara. Tungepewa mrejesho wa hizo kwanza ziliishia wapi, pia tupewe mrejesho wa ule uzinduzi wa kikosi maalum cha kupambana na uhalifu uliofanyika Kinondoni uwanjani wa Barafu na lile gari maalum la msaada ambao polisi walipewa na nchi moja ya ulaya, nalo pia hatujawahi kuona mrejesho wake.