Masai waishika serikali ya Tanzania!!!?

philltaya

Member
Sep 5, 2015
53
11
Pamoja na matamko ya viongozi wakuu wa nchi lakini awa viongozi wa mikoa na wilaya sikujui kama wanafuatilia maagizo ipasavyo!!?kwanini masai bado wanakiburi juu ya kukatazwa kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kuchumgia lakini bado wanachungia,na mkulima akimtaka atoe mifugo yake majibu yanayo toka kwa mfugaji anamuuliza mkulima ng`ombe ikale wapi na kumtishia kumpiga.viongozi wa vijiji inaoneka wanamaslai na wafugaji,ukipeleka kesi polisi,polisi wanakupa rb ili ukamkamate mfugaji,mpaka wewe unaenda polisi unamaanisha umeshindwa na kuchoka,sasa inakuwaje polisi wenyekusimamia hilo wanakupa rb huku wanajua utendaji wa viongozi wa vijiji walivyo!!?mkuu wa wilaya ya mvomero unajua kinachofanywa na wafugaji kijiji cha menge kitongoji cha vianzi chini ya mwekiti wa kijiji Bwana chapakazi?kiukweli wakulima wananyanyaswa na wafugaji je ni kweli hizi taarifa hazipo ofisini kwako?je ujui tatizo kubwa lililopo katika wilaya yako?tafadhali mkuu wa wilaya tatua tatizo tatizo ni zito kuliko hata unavyofikiri.wafugaji wana maeneo yao kwanini wasiende?kwenye hili serikali inapata kigugumizi gani mpaka leo wafugaji kung`ang`ania kwenye mashamba ya wakulima?picha uaribifu unaofanywa na wafugaji
1474862595797.jpg
1474862609035.jpg
1474862620163.jpg
eti huna siraha ukamkamate mfugaji hivi polisi jukumu lao ni nini bado sielewi kabisa dhana ya jeshi la polisi katika hili!!!!!!
 

Attachments

  • 1474862531521.jpg
    1474862531521.jpg
    128.7 KB · Views: 39
Polisi wa Tanzania kazi yao ni kuwazuia wapinzani na kuandika vyeti barabarani.
Wanakuwa serious na matukio ya uhalifu wakupigwa wao..
 
Noti,noti,noti shilingi,bora enzi ya barter trade,wafugaji wepesi sana kutia rupia kwenye uzia.
 
Haya mambo yataisha siku MAzao yatakapopewa uzito sawa na Ng'ombe akilini mwa mfugaji.
Yaani uzito unaochukuliwa mifugo ikiuwawa uwe sawa na ule mazao yakiliwa.
Kuna watu wengi wamekimbia kulima maeneo potential kisa wafugaji. Baraka ya Ngo'mbe mbuzi nakondoo nchini inaweza kugeuka kuwa kichocheo cha kurudisha maendeleo nyuma.
 
HATA SIKU MOJA MKULIMA NA MFUGAJI HAWAWEZI KUKAA SEHEMU MOJA....

OVA
 
hwa jamaa wana ela nyingi sana.... wengine n mifugo ya viongoz wakbwa sana , hii pia inachangia kuwashusha wakulima.....
kwhiyo rushwa na matumizi mabaya ya mamlaka kwa waliyonayo ndo yawaumiza wakulima....
 
Na declare interest kwenye hili, kwasababu nimetokea moja ya jamii za kifugaji. Inawezekana kweli ni nguvu kubwa ya pesa wanayotumia wafugaji, ila pia hata wafugaji tunaamini serikali haithamini mchango wa wafugaji kwenye uchumi wa nchi.
Hatujawahi kutengewa maaeneo ya kwa ajili ya mifugo, wazee wetu eamekuwa waathirika wakubwa wa fine mbalimbali kwenye hifadhi sababu tu maeneo mengi yamebadilishwa kuwa mapori ya akiba.
Ni haki yetu kufuga na pia kutengewa maeneo potential kwa ajili ya mifugo wetu kaka wanavyotengewa wakulima.
Wafugaji hawajawahi kuthaminika, siku zote wanaonekana wao ndiyo waanzisha fujo. Wakulima pia wanavamia maeneo ya wafugaji.
 
MKUU NCHI HII INA MAENEO MAKUBWA SANA WAFUGAJI WAKIAMUA KUJIMEGEA WANAPATA MAENEO MAKUBWA TU,KUHUSU MCHANGO WOTE NYIE WAFUGAJI N'A WAKULIMA MMETOA SERIKALINI,SHIDA KUBWA NI UNAKUTA MFUGAJI ANA MILIKI NGOMBE ZAIDI YA MIA ALAFU KUWALISHA NI MTIHANI UKWELI NDIYO HUU WAFUGAJI WANAMILI MIFUGO MINGI KUWALISHA NI SHIDA NDOMANA MWISHO WA SIKU WANAINGIZA MIFUGO KTK MASHAMBA YA WATU....HAPO UNAKUTA MKULIMA KALIMA N'A ANAKARIBIA KUVUNA MARA MIFUGO INAINGIA SHAMBANI....HAPO LAZIMA TIMBWILI LITOKE
KUNA UKOSEKANO WA USTARABU KATI YA WAFUGAJI N'A WAKULIMA...MIMI NNA USHAHIDI N'A NNACHOKISEMA ILI VURUGU YA KILOSA KATI YA WAFUGAJI N'A WAKULIMA MIMI NLIKUWEPO HUKO N'A NLISHUHUDIA KWA MACHO...SIJAAMBIWA
CHANZO KILIKUWA SAWA N'A NNACHOKUELEZA BAADA YA MFUGAJI KUINGIZA MIFUGO KTK SHAMBA N'A BAADA YA MWENYE SHAMBA KUHOJI AKAAMBULIA KICHAPO TOKA KWA MFUGAJI BALAA LIKAANZA HAPO

OVA
Na declare interest kwenye hili, kwasababu nimetokea moja ya jamii za kifugaji. Inawezekana kweli ni nguvu kubwa ya pesa wanayotumia wafugaji, ila pia hata wafugaji tunaamini serikali haithamini mchango wa wafugaji kwenye uchumi wa nchi.
Hatujawahi kutengewa maaeneo ya kwa ajili ya mifugo, wazee wetu eamekuwa waathirika wakubwa wa fine mbalimbali kwenye hifadhi sababu tu maeneo mengi yamebadilishwa kuwa mapori ya akiba.
Ni haki yetu kufuga na pia kutengewa maeneo potential kwa ajili ya mifugo wetu kaka wanavyotengewa wakulima.
Wafugaji hawajawahi kuthaminika, siku zote wanaonekana wao ndiyo waanzisha fujo. Wakulima pia wanavamia maeneo ya wafugaji.
 
Kulingana na idadi yao awa wafugaji walipewa hekali 3500 na serikal sasa wanachong`ang`ania nini kwenye mashamba ya wakulima?na kama haitoshi wakawakaribisha wafugaji wageni kitoka kilosa!bado nashindwa kuelewa kwann wa wafugaji wasipelekwe kwenye maeneo yao badala ya kutoa tu taarifa ambazo hazina utekelezaji?serikali simamieni hili kama mnania ya dhati watu watakufa kwa njaa kisa wafugaji au mapigano kuendelea warudishwe kwenye maeneo yao wafugaji yaliyotengwa kwaajili yao,wanataka nini kwenye mashamba ya wakulima wakati wao wana maeneo yao
 
Wanatoa RB nani wa kukamata mfugaji?wakati wanajua fika kuwa viongozi wa vijiji c msaada!?hapa uwa kichwa kinauma kipi rahisi kuzuia kutibu tatizo au kilituliza kwa muda?
 

Attachments

  • 1474887492369.jpg
    1474887492369.jpg
    10.3 KB · Views: 24
Mheshimiwa wazir mwenye dhamana tunaomba kuchukulia hatua jambo ili,maana inaonekana hakuna jitihada za makusudi,wala hakuna ufuatiliaji juu ya jambo ili mpaka sasa kuna uharibifu unazidi kuendelea wafugaji wanaingia kwenye mashamba ya wakulima na kufyeka migomba ya ndizi na kuwapa ng`ombe usalama huko wapi!?tunaomba maisha yetu sisi ni kilimo,serikali sikiliza kilio hiki morogoro menge kitongoji vianzi
 
Hivi tukisema ngombe wote wachinjwe mapaka wakaisha myakula nini, kilimo =MIFUGO NEEDS TO BALANCE TRADE-OFF na sio kusema kila wakati wafugaji wanapendelewa
 
Back
Top Bottom