Masaa matatu na Richard Mabala

Ado Shaibu

Member
Joined
Jul 3, 2010
Posts
99
Reaction score
111
MASAA MATATU NA RICHARD MABALA
Taasis za Soma: Leisure Culture and Learning na Kitabu Nilichosoma" zinazojihusisha na kuhamasisha jamii kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu zimeandaa mjadala ambao utawakutanisha wasomaji wa vitabu na mwandishi nguli wa vitabu nchini Richard Mabala.
Richard Mabala atatoa mada kuhusu tasnia ya uandishi wa vitabu nchini. Kwa wapenzi wa vitabu na tasnia ya uandishi wa vitabu kwa ujumla, hii ni fursa adhimu kujumuika na Richard Mabala na kujifunza kutoka kwake.

Pia kutakuwa na mjadala kuhusu kitabu chake kipya cha RUN FREE kilichojinyakulia Tuzo ya Burt ya Fasihi ya Kiafrika. Taasis za Soma Book Café na ‘Kitabu Nilichoma' zitatumia fursa hiyo pia kuwazawadia vitabu washindi mbalimbali wa mashandano yao yaliyopita.
Kitabu cha RUN FREE kinazungumzia changamoto zinazowakabili vijana hasa katika kuchagua njia waipendayo katika kutimiza ndoto zao za maisha. Tumemwalika Masoud Kipanya ( kwa nafasi yake ya uchoraji) na Antony Mtaka ( kwa nafasi yake ya udau kwenye riadha). Njoo uzisikilize simulizi za mbio zao za maisha na za washiriki wengine kisha nawe ueleze uzoefu wa mbio zako!
Siku: Jumamosi tarehe 17/5/2014

Shuka mataa ya Morocco. Rudi nyuma hadi hospitali ya AAR. Kisha fuata barabara inayokwenda Chama cha Wanasharia wa Tanganyika ( TLS). Hapo utaliona bango linalokuelekeza Soma Book Café. Kwa msaada zaidi kuhusu ilipo Soma Book Café piga 0653619906/0785014070
Muda: Saa 4.00 Asubuhi hadi saa 7.00 mchana.
Thibitisha ushiriki wako kwa namba zifuatazo:
0653619906 ( Ado Shaibu )
0785014070 (Soma Book Café)

0717577517 ( Seif Abalhassan)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…