Marriage Yard/Love Connect/Encounter Center

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
2,085
Reaction score
45
Wakuu heshima kwenu.

Katika harakati zangu za ujasiriamali nimekuja na business idea ambayo inahusiana moja kwa moja na hili jukwaa.

Business idea yenyewe imechochewa (inspired) na matatizo makubwa yanayoikumba jamii kwa sasa, ambayo ni watu kushindwa kupata wenza (mme/mke) kwa wakati mwafaka au kwa muda wao wote wa maisha kabisa; na kuvunjika ndoa mara kwa mara kwa sababu ambazo zingeweza kuzuilika. Kumekuwa na wimbi kubwa sana la watu wanaotaka kuoa au kuolewa lakini tatizo ni ugumu wa namna hawa watu wanavyoweza kukutana.

Kutokana na hayo, nafikiria kuungana na wadau watakaokuwa na nia kuanzisha center ambapo watu waliofikia umri wa kuoa kisheria na wenye nia watakuwa wakikutana. Na hii itafanyika kama ifuatavyo:

1. Mtu anayetaka kuoa au kuolewa atatakiwa kuonyesha nia ya dhati (ikiwemo kuapa kwa kutumia kitabu cha imani yake) kisha atajiunga na kuwa mwanachama wa hiyo center kwa kujaza form fulani. Mwanachama lazima athibitishe kuwa hajaoa wala kuolewa, na sio mwanafunzi wa shule ya msingi/sekondari au chuo ambacho hakirusu mtu kuolewa/kuoa kabla ya kumaliza masomo. Lazima atoe vielelezo vya kutosha kuthibitisha hayo. Baada ya mwanachama kuthibitishwa uhalali atatoa kiingilio na kuwa premium member.

2. Mwanachama anachukuliwa picha yake halisi na kuacha biography/CV yake ambayo itaweza kuonwa kusomwa na premium members wengine.

3. Premium member anaruhusiwa kuaccess picha na biography ya wanachama wengine ambazo zimekuwa organized katika mpangilio mzuri (Hapa mwanamke atakuwa na access na database ya picha na biography za wanaume na vilevile wanaume wataccess za wanawake na si vinginevyo).

4. Ikiwa mwanamke au mwanaume amempenda mtu fulani atatoa taarifa kwa wafanyakazi na wafanyakazi watamjulisha mteja ambaye amependwa kupitia picha na biography yake. Mteja atatakiwa kwenda kuangalia picha na biography ya yule aliyempenda. Akiridhika, profiles zao zitakuwa disabled kwa muda wakati wakifanya mazungumzo. Wakikubaliana kuanzisha mahusiano/urafiki/uchumba etc profiles zao zitaendelea kuwa disabled. Wakishindwana profiles zao zinakuwa public tena. Profiles zitafutwa permanently iwapo hao wanachama wataleta taarifa kwamba wameoana.

5. Kumbuka kabla ya kuoana watapatiwa ushauri/counselling kuhusu ndoa na maisha ya ndoa kutoka kwa magwiji, hasa watu wanaohusiana na mambo ya imani kama zao, mfano wachungaji/Imam au psychologists etc. Lengo la hii ni kuzuia ndoa zisivunjike.

6. Wanachama wakiwa katika ndoa watakuwa na nafasi ya kuja na kupata ushauri, mfano kama wamekosana au ikiwa kuna kutokuelewana kwa aina yoyote ile for lifetime.

NB:

@) Haya mambo yatafanyika katika ustaarabu wa hali ya juu na katika hali ya kuaminiwa asilimia 100. Hakuna kutoa taarifa zozote kuhusu watu kwa maana wafanyakazi watafanya kazi chini ya sheria kali. Hapataruhusiwa kamwe vitendo vyovyote vya kihuni/kifuska. Hivyo center itakuwa ni kwa ajili ya mtu kumtafuta mwenza wa maisha tu. Nidhamu na maadili ya hali ya juu ndivyo vitakuwa vipaumbele.

b) Tutafanya matangazo sehemu mbalimbali kama JF, kwenye TVs, radio, Magazeti n.k.

Wakuu naombeni ushauri wenu, na kama kuna mtu anaona hii idea ni nzuri anipm ili tuweze kuliaise pamoja na kuangalia namna ya kuifanikisha. Nia yangu ni kunusuru mioyo mingi inayoumia kwa upweke au kutokana na kuvunjika kwa ndoa.

Wadau tutoe ushauri kwa ajili ya kuboresha hili wazo langu ili tuokoe hiki kizazi! Natanguliza shukrani.

Classics.
 
Imetulia.
Naomba niwe mwanachama namba moja pamoja na Paloma na amu.

classics wazo lako/lenu ni wazo zuri mno, hasa kwa sie madomo zege.
Na hata tuliokuwa na aibu.
Ila tatizo la sisi wa-Tz tutatumia nafasi hyo kugegedana mpaka maana nzima itapotea.
Ila hapa kwa sie wenye Reception mbaya mtakuwa hamjatutendea haki.
Kwani lazima anipende through Picture?
 
Last edited by a moderator:
una visa wewe
 


kama kawa yako hakuna kulala................!!!!

nenda photopoint wakumombofy reception.....mamekapu kibao mbona!!!
 
kama kawa yako hakuna kulala................!!!!

nenda photopoint wakumombofy reception.....mamekapu kibao mbona!!!

Hahaha!
Ma-make-up mwisho saa 5 asubuhi.
Mshale ukivuka tu.
Ngozi ileile.
 
Na status ya kule angaza iwekwe kabisa ila naona kama ni kafecibuku kengine hapo au wadau mwaonaje.
 

Naomba kuwe na limits za kukutana na watarajiwa, kama vile una 5 chances only and then time out...lol... maana kuna uwezekano wa waku-misuse, ukafikiri mtu serious kumbe is just another player or gold digger.
 

Mkuu Madame B ni kweli watu wanaweza kutake advantage kwa ajili ya kugegedana, ndio maana nimesisitiza nidhamu na ustaarabu wa hali ya juu. Ikiwa watu wataanza kuwasiliana kwa makubaliano yao halafua wakaishia kugegedana itakuwa wameamua wenyewe. Itatolewa elimu ya kutosha kwa members wakati wa kujiunga.

Mkuu Picha na wasifu wa mtu - CV nadhani ndio vitatumika kujitambulisha. Mwingine anaweza asikupendee sura ila akapenda wasifu wako.
 
kama kawa yako hakuna kulala................!!!!

nenda photopoint wakumombofy reception.....mamekapu kibao mbona!!!

makeup zilizopitiliza sio nzuri, kwani mtu anaweza kuja kukuona tofauti siku mkikutana live wakati utakapokuwa kwenye original state. Just be simple ili mtu akupende kama ulivyo.
 
MadameX, kuweka limit itakuwa vizuri ili kudhibiti watu wasio kuwa na nia njema. Lakini kumbuka kutoa elimu kwa wahusika kabla ya kujiunga na yeye kutakiwa kuthibitisha nia yake vitasaidia pia.
 
Mkuu kirumanjeta hiyo haitakuwa kama fb kwa sababu itakuwa na lengo maalumu halafu itasimamiwa na maadili ya kitanzania.
 
Paloma, hahahaaa, photos za nani hizo. Too much making up is harmful.
 
Hahahahahahahaha
daa jf raha tupu!
Ideal nzuru utawasaidia wengi
kuwepo na interview kabisa .
Daaaaah
 

Acha maneno yako wewe.
Kwa Mtz wa kizazi hiki eti akubali kuoa au kuolewa na jitu lenye sura nzito, nani kasema.

Mjini Sura na Shepu.
Tabia Kijijini.
 
::
Usisahau kuweka somo la FUNGULIANA MIOYO.
Maana huko ndiko yaliko mafumbo ya upendo na usaliti.
=
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…