Marijani Rajabu vs Mbaraka Mwinshehe : hizi ndio nyimbo zinazo watoa droo

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
567
1,550
Katika Mpambano ambao huwa ni Mgumu ni huu wa Hawa Miamba wawili wa Muziki wa kale. Unapo sikiliza basi akili na amoyo wako vitaegemea kwa unaye msikiliza. Hizi ndio Nyombeo zao zinazo toa Droo na kukosa Majibu. Inagawa kwa mimi Binafsi namuweka Marijani juu kidogo kwa ailimia tano tu yaani 100%:95% sababu Marijani katoa tungo nyingi tata na zenye mafuzo.

Marijani Rajabu:
1.Usia
2.Mwanameka
3.Ndoa ya Mateso
4.Zuwena
5.Masudi
6.Mbaya wangu
7.Pombe sio Chai
8.Mwajuma
9.Rafaa ya kifo

Mbaraka Mwinshehe:
1. Mtaa wa Saba
2.Baba mdogo
3.Mashemeji wangapi
4.Mshenga
5.Shida
4.Mshenga
5.Shida

Kitu cha kukubaliana ni kwa Nyimbo nyingi za Mbaraka zinakuwa za kuchezeka yaani za kujirusha wakati kwa Marijani mule unashiba Ubongo tu unajazwa mausia ya kufa mtu.
Karibuni wahenga tupeane maoni zaidi tumalize huu Mwaka.
Happy new year nyote
 
Marijani. =[KIBA] namsikiliza pale tu ninapotaka kusikia kitu kizuri kutoka kwake
Mbaraka=[platnumz]. Muda wowote ule namsikiliza kwa sababu tu namkubali kiufupi anajua
 
Kwa Marijani Rajabu ongeza:-
10. Dunia Uwanja wa Fujo
11. Mayasa
12. Siwema
13. Walimwengu
14. Nyerere Baba
15. Wapo Wapi Wenye Nguvu
16. Tamaa Mbele
17. Nisikilize Baba Watoto
18. Uke Wenza
19. Mwanameka
20. Sikitiko

Hizi nyimbo zina ujumbe mzuri sana, nimewawekea wimbo wa DUNIA UWANJA WA FUJO.
 

Attachments

  • Dunia Uwanja Wa Fujo ~ MARIJAN RAJABU & DAR INTERNATIONAL ORCHESTRA.mp3
    10.5 MB · Views: 24
Hiyo ngoma MWANAMEKA iliwahi kuja ktk pepa ya KISWAHILI NECTA kwenye USHAIRI! Tulitafutana Chumba kizima hapakutosha!

Namkubali sana MARIJANI japo MBARAKA alikuwa hatari mpk REMMY ONGALA wa Matimila amemtaja ktk ngoma yk ya KIFO!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom