Poa 2
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 1,333
- 1,356
Tulitegemea kwamba wale walioumiza wengine wachukuliwe hatua kwa mjibu wa sheria, au hata kuomba msamaha hadharani lkn ni tofauti ndio kwanza wanapandishwa vyeo.
Tulitegemea kwamba wale walioumizwa watambuliwe, walipwe fidia na wakiri kusamehe.
Tulitegemea kwamba kama taifa zile sheria mbovu na kandamizi zinazotumika zifutwe au kurekebisha lkn zinaendelea kuumiza watu na tunazungumza maridhiano.
Walio umizwa Tanzania sio CHADEMA tu Kuna wafanya biashara, wasanii, viongozi wa dini nk kwa nini maridhiano yawe kati ya Samia na mwenyekiti wangu tu.
Haya maridhiano ni ya kitaifa kweli au ni kati ya Samia na mbowe? Kuna watu wananufaika na haya maridhiano huku wengine waliachwa na maumivu, na vilema vyao.
Kwani hata sisi CHADEMA tumeshindwa kuwa na mkakati wa kuwasaidia hata wanachama wetu wengi walioumizwa Ili iwe mfano mwema?
Kwa dhati kabisa ninaungana na msimamo wa lisu kuhusu haya maridhiano kwani yamejaa hadaa na ulaghai mkubwa sana