Marekani yazidi kushambulia Al Shabaab

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427


Wapiganaji wa Al shabaab wameendeelea kuwalenga wanajeshi wa serikali na wale wa kigeni nchini Somalia
Jeshi la Marekani limesema kwamba lilitekeleza mashambulio ya anga nchini Somalia na kuwaua wapiganaji 12 wa kundi la Al Shabaab. Idara ya ulinzi imesema wapiganaji hao walitishia usalama wa maafisa wa Marekani ambao wanasaidia wanajeshi wa serikali ya Somalia.

Mashambulizi hayo yalitekelezwa Jumatatu na Jumanne ya wiki hii viungani mwa mji wa Kismayo kusini mwa Somalia. Jeshi la Marekani halijaelezea kwa kina tishio la Al Shabaab kwa maafisa wake.



Bado kundi hili linathibiti baadhi ya maeneo ndani ya Somalia
Wakaazi wa maeneo kulikofanyika mashambulio hayo wameambia BBC baadhi ya waliouawa walikua ni raia. Haya ndiyo mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani nchini Somalia dhidi ya kundi la Al Shabaab ambalo linashirikiana na mtandao wa Al Qaeda.

Wiki jana idara ya ulinzi ya Marekani ilisema kiongozi mmoja wa Al Shabaab Hassan Ai Dhoore alikua ameuawa kwenye shambulio la ndege isiyo na rubani. Wapiganaji hao wamekua wakitekeleza mashambulizi makali dhidi ya maafisa wa serikali ya Somalia, wanajeshi wa kigeni sawa na kulenga hoteli na migahawa katika mji mkuu Mogadishu.

Chanzo: BBC Swahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…