Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Rais wa Somalia 67 na Wakenya watano wamefukuzwa nchini Marekani kwa nguvu baada ya kubainika kuwa walikuwa wanaishi nchini humo kinyume cha sheria lakini pia kujihusisha na makosa mbalimbali
Ndege ya kibinafsi iliyowabeba watu hao iliwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Ijumaa asubuhi
Maafisa nchini Kenya wanasema walikuwa wanafahamu kuhusu kurejeshwa kwa raia wa nchi hizo mbili, na tayari raia wa Somalia wamerejeshwa mjini Mogadishu kwa kutumia ndege nyingine ya kukodi
Hatua hii ilitarajiwa kutokana na operesheni inayoendelea nchini Marekani kuwarudisha nyumbani wahamiaji haramu wanaoishi nchini humo lakini pia wageni wanajihusisha makosa mbalimbali
Mwezi Januari, wakenya wawili na raia wengine 90 wa Somalia walifukuzwa Marekani kwa sababu mbalimbali
Rais Donald Trump miezi kadhaa iliyopita, aliamua kuwazuia wahamiaji kutoka mataifa ya Kiislaam kuingia nchini humo, hatua ambayo ilizuiwa na mahakama
Mataifa yaliyolengwa ni pamoja na Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria, na Yemen.