Marekani yaiwekea vikwazo Uganda

fungi

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,539
4,669
110307162322_jp_lra512x288_nocredit.jpg

Marekani imeiwekea Uganda vikwazo kwa kupitisha sheria zinazopinga mapenzi ya jinsi moja katika taifa hilo la Mashariki ya Afrika.

Afisa wa mahusiano anayesimamia maswala ya usalama katika ikulu ya whitehouse Caitlin Hayden anasema kupitia kwa barua kwa wanahabari kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la Uganda mwezi Februari inakiuka haki za binadamu.

Vikwazo hivyo vitajumuishwa marufuku ya wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani.

Miradi itakayoathirika na marufuku hiyo ni pamoja na ushirikiano na polisi wa Uganda Wizara ya Afya.

140331093422_uganda_mabango_512x288_bbc_nocredit.jpg

Sekta ya Afya na usalama wa taifa itaathirika na vikwazo hivyo.

Aidha msaada kwa miradi iliyoanzishwa kwa usaidizi wa marekani pia utapunguzwa mbali na kufutiliwa mbali kwa mazoezi ya kijeshi kati ya majeshi ya uganda na yale ya Marekani.

Sheria hiyo inaharamisha uhusiano baina ya watu wa jinsia moja na wale watakaopatikana wanaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni iliyochukuliwa na Marekani katika ajenda yake ya kupinga sheria hiyo mpya nchini Uganda.
Juma lililopita Seneta mmoja kutoka Marekani ,Kirsten Gillibrand alilalmikia vikali uteuzi wa waziri wa maswala ya kigeni wa Uganda Sam Kutesa kuchaguliwa kuwa rais wa Umoja wa Mataifa kutokana na kuwa anatokea Uganda.

140413103204_uganda_-antigay_512x288_ap.jpg

Marekani imeiwekea Uganda vikwanzo kuhusina na sheria ya wapenzi wa jinsia moja.

Watu 9000 walikuwa wametia sahihi pendekezo la kuitaka Umoja wa Mataifa kumng'oa kitini bw Kutesa aliyechaguliwa licha ya kampeini hiyo.

Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja wameenda mahakamani wakitaka sheria hiyo iondolewe lakini inatarajiwa kupingwa kwani rais Yoweri Museveni aliupitisha maksudi kudhihirishia wafuasi wake kuwa yu huru kutokana na shinikizo kutoka kwa mataifa ya ughaibuni .

Punde baada ya kupitishia kwa sheria hiyo mpya benki kuu ya dunia iliahirisha utoaji wa mkopo wa dola milioni 90 ambazo zilikuwa zinapaswa kutumika kuimarisha sekta ya Afya nchini Uganda .

Mataifa mengi tu ikiwemo Denmark, Norway, Uholanzi na Sweden zote zimekatiza msaada kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Source: BBC
 
Afisa usalama wa anaesimamaia maswala ya ikulu Caitlin Hayden alisema sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la uganda february mwaka huu inakiuka haki za binadamu
 
Afisa usalama wa anaesimamaia maswala ya ikulu Caitlin Hayden alisema sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la uganda february mwaka huu inakiuka haki za binadamu

Washenzi kabisa, haki gani kupita migongoni kwa viumbe wenzao?
 
Tanzania tumeruhusu mapenzi ya jinsia moja kiaina, japo Sheria za nchi zinakataza lakini kwa kuwa nchi inendeshwa kwa kuzungusha BAKULI. Mkakati wa Taifa wa Kupambana/Kudhibiti UKIMIWI unapigia chapuo la matumizi ya vilainishi (lubricants) na haki za Key Populations. Bongoland Kwishney viongozi wetu wengi hawana ubavu wa kutunisha misuli kama M7.

" Many times Dictators are action oriented"

" Many times Democratically elected leaders are promise makers"
 
Marekani imetoa msimamo wake kuikatia Uganda misaada na vikwazo mbali mbali kwa wanaoshabikia (kunyanyapaa) wapenzi wa jinsia moja. Hiyo ndio Marekani!
 
Kwani vipi kuhusu baba ritz alikubali kuoana jinsia moja watanganyika?
 
Unafiki mwingine bwana. Serikali zinapovunja haki za binadamu haziwekewi vikwazo ila watu wakipiga marufuku mambo ya kishetani wanawekewa vikwazo!!! Hiyo kitu sijui ina raha gani mpaka iitwe haki ya binadamu? Madaktari tunawaombe mtangaze athari za huo uchafu ili watu wajue waamue wenyewe kufanya au kutofanya kama ilivyo kwa sigara.

ni muda africa isimame na kujitegemea yenyewe ili ikue... tukijitenda na hizi western countries ndio itakua fundisho na mwanzo wa mafanikio... yani ban hiyo ndo inawapa watu presha, ati wamezuia mkopo wa 90million dollars, hiyo hela aisee hata bongo hapa wanaweza wakaja tukawakopesha, kahela kadogo hako mtu anafata world bank.. african countries kazi ipo ignorance rate ni kubwa kupindukia
 
Nawaombea Uganda wabaki na msimamo wao hadi mwisho.Wamerakani na washirika wao kuwaua wananchi wasio na hatia Iraq,Libya,Angola,na Afghanistan hawaoni ni kutolinda haki za binadamu?
 
Marekani imetoa msimamo wake kuikatia Uganda misaada na vikwazo mbali mbali kwa wanaoshabikia (kunyanyapaa) wapenzi wa jinsia moja. Hiyo ndio Marekani!

Mugabe alishamwambia obama mpumulie kisogoni kwanza alafu kama ni tamu ndo aruhusu zimbabwe sheria kama hiyo. Marekani ama kweli ni shetani mkubwa mno.
 
Tungeungana waafrika wote kupinga huu ushetan wa wazungu wangesalimu amri!

NI kweli ndo maana mimi ninapoona humu JF watu wanatoleana vifua eti kwa sababu ya yesu na muhamad nawashangaa sana. Tunapotofautiana hivyo ndo mzungu naye anatuingia kwa urahisi. Mzungu ishu ya uislam na ukristo haimuusu sana ila tu maslahi.
Sasa tukisimamia uafrika wetu tutashinda. Lakini tukisimamia udini wetu tutasambaratika sana. Mfano mzuri nigeria. Ni nchi yenye nguvu sana, lakini sababu za kidini zinaiporomosha siku hadi siku. na hapo mzungu anapenyeza.
 
Huyu ndo Mugabe na Obama wanaonyesha mfano wa demokrasia.
 
Attachments

  • 1403412421062.jpg
    1403412421062.jpg
    45.5 KB · Views: 159
NI kweli ndo maana mimi ninapoona humu JF watu wanatoleana vifua eti kwa sababu ya yesu na muhamad nawashangaa sana. Tunapotofautiana hivyo ndo mzungu naye anatuingia kwa urahisi. Mzungu ishu ya uislam na ukristo haimuusu sana ila tu maslahi.
Sasa tukisimamia uafrika wetu tutashinda. Lakini tukisimamia udini wetu tutasambaratika sana. Mfano mzuri nigeria. Ni nchi yenye nguvu sana, lakini sababu za kidini zinaiporomosha siku hadi siku. na hapo mzungu anapenyeza.

Wewe kwa akili yako ushoga ni tishio kuliko extremism? be serious please, katika kipindi ambacho watu wameweza kuvent asira zao dhidi ya ugaidi na uitikadi kali ni hizi zama za mitandao ya kijamii, mimi naamini kuna waislam wengi sana humu wameelimika kwani zamani hawakuwa na utamaduni wa kupingana kwa hoja bali wao walikuwa wakikimbilia kusema muhammad wao katukanwa na hivyo kuanza jazba, sasa hivi moyo wa uvumilivu unaanza kuwasaida soon extremism will extinct. suala la maslahi kama kigezo cha kulaumu wazungu ni ujinga tu kwani hizo ni hoja dhaifu za waislam wanaoendekeza mauaji ya udini. watakaosababisha kusambaratika kwetu ni wadini na wewe unafahamu wana misimamo mikali sana si watu wa amani hata kidogo, kwa nini tusiwaseme?Nigeria kwa kujiona wao ndio wasomi zaidi waliruhusu states(kumbuka serikali yao ni federal) kwa hiyo memba state zinaweza kuanzisha sheria za kidini wakasahau kuwa muislam hana ustaaarabu huo!!! sasa kinawatokea puani kwani mpaka kwenye jeshi kuna wanaounga mkono Boko haramu eti kwa kuwa ni waislam wenzao. wacha tuchanane live ndio tutakomaa(wasiwasi ni kwa wazee wa jazba tu, wakristu hawana noma).
 
Mkuu, sijui wewe point yako ni ipi. Lakini nikisoma mistali yako hapa naona kama umeona dini inachoche kugawanyika.
Mimi kama muafrika ninaona issue ya udini ni janga linalotufanya waafrika kupoteza umoja wetu. Tunapoanza kusema wewe mkristu na mimi muislamu hatuchangamani, wazungu ndo wanapopata jinsi yakutugawanya na hatimaye kuiba mali zetu. Wewe umejaribu kuelezea practice ya udini inavyofanyakazi, ambapo ndo hichohicho kinachotufanya tutengane sisi waafrika. Ahsante
 
Back
Top Bottom