Marekani yaituhumu Syria kwa kuchoma wafungwa Gerezani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Marekani imeituhumu serikali ya Syria kwa kujenga sehemu ya kuchoma maiti katika jela ya kijeshi iliyopo karibu na Damascus ili kuficha mauaji ya halaiki ya wanaoshikiliwa na serikali.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeonyesha picha zilizopigwa kupitia njia ya Satelite ambazo imesema ni sehemu ya kuchoma maiti katika gereza lililopo Sednaya ambapo Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema maelfu ya wafungwa wameteshwa na kunyongwa.

Mwanadiplomasia mwandamizi wa Marekani anayehusika na masuala ya Mashariki ya kati, Stuart Jones, amesema kwa siku wafungwa takriban hamsini wanauawa katika gereza la Sednaya.

Ameongeza kusema kuwa, mauaji hayo yanafanyika kutokana Syria kuungwa mkono na Urusi na Iran.

Chanzo: BBC Swahili
 
Assad hana muda mrefu madarakani kwa hizi habari maana hata Saddam na Gafaffi walifnyaga vitu hivi
 
Urus na Irani hawajielewi wanafananya vile kumsupport ili kuonesha usuper power lkn wanafny vbaya kumtetea huyu dicteta...Moscow inasapoti mambo ya kipumbavu ili kuuza silaha na kujipatia sifa
 
Assad hana muda mrefu madarakani kwa hizi habari maana hata Saddam na Gafaffi walifnyaga vitu hivi
Utasubiri sana, Mkuu! Ni wasyria wenyewe tena bila kusumbuliwa na wageni wanaoweza kumtimua Assad Madarakani.
Middle East game is now being won by sensible parties.
 
Wamarekani wangekuwa na huruma ya kweli ningewaunga mkono. Mbona nao wanawauzia silaha wanaopigana ili wauwane?. Na walipowauwa watu Afghan badala ya huzuni wakawa wanalisifia kombora lao lenye jinsia flani eti " mother of all bomb".
 
Marekani huwa haishiwi sababu hata siku moja, akiamua kukuchukia kakuchukia na akitaka kukupoteza anakupoteza. Asad hana kosa hata kidogo.
 
Urus na Irani hawajielewi wanafananya vile kumsupport ili kuonesha usuper power lkn wanafny vbaya kumtetea huyu dicteta...Moscow inasapoti mambo ya kipumbavu ili kuuza silaha na kujipatia sifa

Bush na mtoto wake, obama na the trump Je co madikteta???? Marekani haifai kusapotiwa mkuu
 
wafungwa wenyewe walikuwa ISIS au sio? kama walikuwa ISIS wale wanaochinja raia mchana kweupe, wale wanaochoma wenzao wakiwa wazima kabisa, .....wakati mwingine tusimlaumu sana assad.
 
Back
Top Bottom