comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Marekani inazidi kusaka jitihada za kimataifa za majadiliano ya kidiplomasia kuhusu Korea kaskazini, Rais Trump anakutana na wajumbe wa baraza la seneti baadae leo mjini capitol hill katika mkutano huo usio wa kawaida kuhusu Korea kaskazini, hata hivyo Rais Trump anategemewa kuongea kwa dakika tano katika mkutano huo ndipo baadae ataichia timu za usalama na maseneta waendelee na ajenda, wajumbe wa baraza la seneti la Marekani wakiwa pamoja na Waziri wa ulinzi wa Marekani Jenerali James "Man dog" Mattis, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson, Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa la Marekani Dan coats na balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Nikki Haley wote wamepuuza juhudi za Rais Trump za kutaka kuivamia kijeshi Korea Kaskazini badala yake wamependekeza mazungumzo ya diplomasia za kimataifa kuhusu makombora ya nyuklia ya Korea Kaskazini, vilevile China imefurahishwa na uamuzi wa mazungumzo na kusema yanaleta matokeo chanya
Aidha kumekuwa na mpendekezo mengine yakiwemo Korea kaskazini iharibu yenyewe mitambo yake ya nyuklia au iingizwe kwenye list ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani, pia kuitenga kimataifa nchi ya Korea kaskazini mazungumzo mengine ni kuiwekea vikwazo vya kiuchumi
Al-jazeera English News